Akija Rais atakaye deal na bodaboda nitamshukuru

Mimi naamini polisi na wasimamia sheria wengine wakiamua kufanya kazi yao bodaboda wananyooka ndani ya wiki tu. Polisi na wasimamia sheria wengine ndio wanalea na kukuza huu ujinga.
Wala hakuna haja ya kupiga marufuku. Kupiga marufuku maana yake polisi na wasimamia sheria wengine kazi imewashinda.
 
Hayo yote mnayo wish bodaboda wayafanye haiwezdkani. Kuheshimu tu taa za barabarani hawawezi, polis mpaka wakawa wanakaa na fimbo lakini wakashindwa. Boda ni kitu kingine
 
Hicho kipengere cha bodaboda na wake za watu nimekizungumzia kwa sababu mauaji ya bodaboda mbali na kutekwa kwa ajili ya kunyaganywa chombo ila wengi wao wamekuwa wanauwawa kwa kesi za kutembea na wake za watu na uvujishaji wa siri za mahusiano ya watu
 
Bajaji na Bodada kuna namna inabidi serikali ( idara husika waangalie namna ya kufix baadhi ya mambo ). Ni tatizo
 
Kuongezeka kwa bodaboda ni dalili ya serikali kushindwa kutengeneza mifumo mizuri ya ajira, vijana wanajitafuta kwenye bodaboda, shida tu ni hapo wanapojihusisha na wake za watu na wanafunzi, ijapokuwa wapo wengi tu wanaojiheshimu na kuthamini Kazi zao kiufupi bodaboda ni ajira halali kabisa hivi sasa
 
Zaidi ya 60% ya magari binafsi mijini yana alama za kukwaruzwa na ngao za bodaboda ubavuni kwa nyuma.

1.Barabara ambazo ni njia moja kwao ni njia mbili,tatu etc

2.Wana-overtake upande wowote mradi upenyo tu.

3.Hawaangalii indicators za vyombo vingine,wanapuyanga tu.

4.Wanaegesha kwenye culverts ambazo ni junctions za kuingia na kutoka barabara za lami hivyo mpaka wakupishe ndiyo upite.

Serikali ingezuia kwa sasa kuingia pikipiki nchini wala spares zake,bora hata bajaji.
 
Hivi na wewe mwehu? Uko barabarani ni sawa wengi hawafati sheria za barabarani ....Unahusisha vipi bodaboda na wake za watu?
Asilimia kubwa ya boda wapo rafu wachafu ukiona mpka mkeo anatembea na boda tambua mkeo ndio tatizo.
Acha kuwahukumu hao vijana
 
Mimi siwaelewi kabisa mnapolalamikia bodaboda na wake zenu.
Wake zenu ndio shida wala sio boda
 
Mwenyewe unajiona umeongea point kumbe utumbo mtupu. Mwehu utakuwa wewe unaeaakadiria wanaawake watakuwa namna. Akili zao wanazijua wenyewe.
 
Aione kwenye jalada Mzee Lema.Namnukuu "Bodaboda ni kazi ya laana kizazi hadi kizazi"
 
Mwamba umegongewa mke na boda nini!!?
 
Kwani bodaboda inamfanya mtu awe na tabia mbaya, au kabla ya kuendesha bodaboda alikuwa na tabia hiyo? Hizo tax unazosema zilikuwa na watu wa hovyo sana, ukisikia dereva tax picha ilikuwa inakuja mtu mwenye tabia chafu, kumbe hiyo ilisababishwa na baadhi ya watu.
Wapo hawa wazee wa magari makubwa, nao unasikia sifa mbaya, kwa haraka haraka unaweza kufikiri madereva wote wana tabia mbaya.
Yeyote kwa nafasi Yeyote anaweza akawa na tabia mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…