Akikwambia 'msalimie wifi', imeisha hiyo mtu wangu

Akikwambia 'msalimie wifi', imeisha hiyo mtu wangu

Nyuzi za hv muwe mnaandika mapema sasa!

Mtaa naokaa tuna siku kadhaa maji hamna Jana jioni ikabidi nikatafute hata ya chumvi ili nisurvive, mda narudi na ndoo zangu mbili nkakutana na wadada wakaniuliza mbona unachota maji usiku wifi hayupo?
😂😂
 
Can't provide internet... Nimechek sana hio conclussion[emoji23]... No internet access
 
Dem ndo mmejuana juana siku moja mbili tatu hivi. Hujaweka clear intention yako kwake ila mkikutana au mkipigiana simu mnaongea mnafurahi.

Hata kama mmejuana muda mrefu. Ila hamjuani kiundani hasa katika eneo la mahusiano. Ni workmate wako pengine, ila recently mmekuwa na ukaribu sana na utani utani wa hapa na pale.

Ikatokea siku katika mazungumzo yenu yakutaniana taniana mliyoyaibua juzijuzi, mwishoni akikuaga akakwambia 'Msalimie wifi', bro, wala hata usijihangaishe kuwaza anamaanisha nini. Ameshakuelewa huyo. Anakutengenezea njia upite nae.
Watoto wa siku hizi bwana. Yaani unakuwa duanzi mpaka demu ndiye aanze kukutupia kijembe? Bila shaka hapo anakuwa ameshaona hili li-jamaa kila saa linaniletea story za ''maza yangu ni mkali kweli nikichelewa kurudi nyumbani'' akaona signal uzinduke kwenye uduanzi.
 
mwishoni akikuaga akakwambia 'Msalimie wifi', bro, wala hata usijihangaishe kuwaza anamaanisha nini. Ameshakuelewa huyo. Anakutengenezea njia upite nae.
Unawatafutia watu matatizo nakumbuka niliambiwa hivyo na mtu muhimu sana alafu sikutegemea km atanirushia hicho kimsemo nikamuuliza umesema akaniambia mdogo wako wa kike, duuuh sikuweza kufungua hio code mpaka kesho kumbe ndio hivyo?
 
Back
Top Bottom