Akili ni kama mimba tu, aidha unayo au huna. Hakuna mwenye akili nyingi, wala mwenye akili kidogo

Akili ni kama mimba tu, aidha unayo au huna. Hakuna mwenye akili nyingi, wala mwenye akili kidogo

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,914
Reaction score
168,320
AKILI: NI NYINGI, NDOGO, AU IPO TU?
Bujibuji Simba Nyamaume

Watu wengi husema, "Yule ana akili nyingi, yule ana akili ndogo." Lakini je, ni kweli akili hupimika kwa wingi?

Mjadala huu una pande mbili.

Upande wa Kwanza: Akili ni moja. Unayo au hauna.

Wanaosema hivi wana hoja nzito. Kila mtu aliye hai ana ubongo. Tofauti si akili, bali matumizi ya akili.

Mfano, mtu mmoja anajua hesabu, mwingine anajua kulima. Je, mwenye hesabu ana akili nyingi kuliko mkulima? Hapana. Kila mmoja ametumia akili yake kwa njia yake.

Akili si maji kwenye ndoo - kwamba mwingine ana ndoo kubwa, mwingine ndogo. Akili ni kama moto. Moto ni moto. Mwingine anautumia kupika chakula, mwingine kuunguza nyumba. Moto ule ule, matumizi tofauti.

Kwa mtazamo huu, hakuna mjinga. Kuna mtu tu aliyekataa kutumia akili aliyonayo. Na hakuna mwerevu kupita kiasi. Kuna mtu tu aliyeamua kuitumia akili yake kila siku.

Upande wa Pili: Akili hutofautiana.

Wengine hupinga. Wanasema, kama akili ni sawa, kwa nini mmoja anashika darasani haraka, mwingine polepole? Kwa nini mmoja anabuni ndege, mwingine hawezi kutengeneza hata kiti?

Sayansi inasema uwezo wa ubongo hutofautiana. Kama urefu. Wote tuna urefu, lakini hatulingani. Hivyo ndivyo akili ilivyo.

Hitimisho Langu:

Kusema "akili ni moja" kuna ukweli wa kimaadili. Kunatufanya tusidharau watu. Kila mtu ana thamani sawa.

Lakini kusema "hakuna akili nyingi na ndogo" ni kukataa ukweli wa mbele yetu. Tofauti ipo.

Jibu la kati ni hili: Akili kama mbegu, kila mtu amepewa. Mbegu ni mbegu. Lakini mavuno hutofautiana kutokana na jinsi unavyoilima.

Hivyo, si kwamba mwingine hana akili. Bali ni kwamba bado hajaamua kuilima shamba lake.
 
Asante sana Bujibuji Simba Nyamaume kwa mada hii nzito na yenye kutufanya tufikiri! Ni kweli, mjadala huu una pande zote mbili zenye hoja za msingi na ni rahisi kujikuta ukikubaliana na zote.

Mimi binafsi nimevutiwa sana na hitimisho lako la akili kama 'mbegu'. Linatoa picha halisi kabisa ya jinsi gani kila mmoja wetu ana uwezo wa kipekee, na jukumu letu ni kuilima hiyo mbegu vizuri ili tupate mavuno bora.

Hii inatupa motisha kwamba hata kama hatujafanana katika uwezo wetu wa awali, bado tuna nafasi ya kukua na kuendeleza akili zetu kwa kujifunza, kujaribu vitu vipya, na kutokata tamaa. Hakuna 'akili ndogo' isipokuwa ile isiyotumiwa au kuendelezwa.

Kila mmoja wetu ana mchango wake wa kipekee kulingana na jinsi anavyoitumia na kuikuza akili yake. Tuendelee kujifunza na kutiana moyo!Bujibuji Simba Nyamaume, asante sana kwa mada hii muhimu na yenye kuamsha fikra! Umeiweka vizuri sana na umetoa pande zote mbili kwa ufasaha mkubwa.

Nimependa sana hitimisho lako la kati, la kulinganisha akili na mbegu. Kwa kweli, hii inatoa picha nzuri sana na yenye kutia moyo! Kama akili ni mbegu, basi kila mmoja wetu ana uwezo wa kuikuza na kuzaa matunda yake mwenyewe, kulingana na jinsi anavyoitunza na kuilima.

Hii inatufundisha kutokata tamaa na badala yake, kujitahidi kutumia na kukuza uwezo wetu kila siku. Inatia moyo sana kujua kwamba uwezo wa kufikiri na kubuni hauna mipaka, na kila mtu anaweza kuuendeleza kwa bidii na kujituma. Asante kwa mjadala huu mzuri!
 
Nilitegemea utoe tafsiri ya Akili, Ili tupime Kuna ukweli gani kwenye hili

Sijui unaweza nisaidia tafsiri yake

Maana naona ulicho eleza hapo juu ni Ubongo, siyo akili.
 
Wenye miakili ya kutisha tunasema apo umetumia logical fallacy non sequitur, no proof no claim.
 
Tufanye kila mtu ni zezeta ila tumetofautiana viwango vya uzezeta. Kuna wale ni zezeta mpaka udenda unashuka halafu kuna zezeta anayenyoa nyusi zote apake wanja halafu kuna zezeta club ya mpira ikisajili mchezaji wa mabilioni anasema tuna pesa tumesajili ila yeye hana hata Mia hivyo hivyo inaendela.
 
Unatumia akili kuamua au kukataa kutumia akili kwenye mambo muhimu. Hivyo una akili kidogo.
 
Kila mmoja ana akili nyingi kwenye eneo lake alilopewa kulitumikia, ukifanya vizuri kwenye field Fulani basi wewe moja Kwa moja Una akili nyingi haijalishi darasani ulikuwa Unapata grade gani...Nikola Tesla ana mbingu Yake, Isaac Newton ana mbingu Yake, Al-Khwarizmi ana mbingu Yake, Ramanujan ana mbingu, hawa wote ni super genius kwenye field zao...Kila mmoja wetu ambaye ni mzima wa afya ana kieneo chake ambacho akikijua au kukiotea basi anakuwa exception kabisa....
 
I stand to be corrected.

Hakuna akili ndogo wala kubwa, kwani akili ni uwezo wa asili ambao kila mtu anao kwenye eneo husika.

Kwa mujibu wa Neurological Institute of Los Angeles, 2015 "Akili ni uwezo wa asili uliomo kwenye ubongo unaomwezesha binadamu au kiumbe kufikiri, kuelewa, kujifunza, kupanga na kutatua matatizo"

Perception ya ukubwa ama udogo wa akili hupimwa kwa njia moja pekee ambayo ni "Kiwango cha maarifa alichonacho mtu" katika eneo husika, na kiwango cha maarifa hayo ni jumla ya taarifa alizonazo mtu kutoka vyanzo mbalimbali kuhusu jambo fulani.

Mfano: Ukikosa taarifa sahihi kwenye eneo la fedha automatically unakuwa na uelewa mdogo kwenye eneo hilo na kinyume chake ni sahihi pia.

Taarifa Nyingi = Maarifa Mengi
Taarifa Kidogo = Maarifa Kidogo
 
Back
Top Bottom