Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,677
Sijui shida ni elimu au vip. Mfano mdogo sana nilijaribu kwenda kununua kiwanja maeneo mawili tofauti katika mikoa miwili tofauti.
Kilichonishangaza ni kwamba, unakuta muuzaji wa kiwanja, au mmiliki amegawa hivo viwanja kwa style ambayo mpaka unaweza kujiuliza 'hivi huyu mtu ni kichaa?'
Unakuta viwanja vimegawanywa mara kingine unakuta kina shape ya pembetatu, kingine cha pembeni kina shape ya trapeza, kingine ni mraba ambao haujakaa sawa pande zote.
Matokeo yake watu wanakuja kujenga, unashangaa nyumba zimepangana kama kikao cha nzi. Yaani mpaka ukipaangalua hivi unapata kichefuchefu.
Nikakaa chini nikajiuliza 'Hivi hata hili nalo linahitaji uwepo wa serikali? Kwanini hawa wauzaji wa viwanja wasigawanye maeneo kwa kufuata mpangilio unaovutia?