Akina dada, kwanini mnakubali kutoa namba kisha mkipigiwa simu hampokei?

Wasipokuelewa hapa wakapimwe mkojo.
 
Haupati faida kwa kunisingizia majambo, tafadhali kuwa mkweli kuwa ulinipotezea, kiri haya kwa wana jukwaa ili tuanze upya! 😀

(kiswahili changu kama cha ChatGPT)
Labda hukusikia simu inavyoita kwasababu wewe ni Binti Kiziwi, lakini nilipiga sana simu.
 
Sasa kutoa namba na kuto respond unapopigiwa au tumiwa sms ndio surviving mechanism?.

Surviving mechanism ni kukataa kutoa namba from the first place kama utaona huyu mwanaume sio wa taste yako.

Mwanamke kutongozwa sio jinai wala udhalilishaji, na kama haujavutiwa na uyo mwanaume unamkatalia tu ombi lake.
 
Hauna hela wewe
 
Si mnasema si vizuri kutanguliza pesa mbele sasa hapa inakuaje tena? Na ukishampata akikuomba hela mbeleni utaendelea kumpa au ndio inakua bye bye??
Akiwa mtu wakuomba hela sana anamrahisishia mwanaume kujua huyu ni wa hit and run
 
Pole, mvumilie. Mimi huwa nashangaa wale wanaume wakiomba namba wasipopewa wanaporomosha mvua ya matusi, hawa nao unawaweka kundi gani?
Kwenye kundi la wapumbavu.
 
Huu ni uhuni😂
 
Huu ni uhuni😂

Wanawake wengi tunapenda wasio kama maboga, Moyo ukipewa chalenjiz na heshima iwepo zoo hapo utafurahia sanaaaa..
Na kupendwa ila mwanaume tumia akili.

Sio kila dk masimu kama huyo, ukipigiwa pokea zooo ukiringa makusudi or upo bizi basi meseji au masimu ka dk chache muhimu

Lege Lege wa kuambiwa na kufata kila jambo aisee utapoteza nyapu akikaa nawe basi kuna kitu anataka..

Chalenji 😘 huku mahaba moto motooooo
 
Sawa sasa ile ishu yetu vp? Mana namba yako niliyonayo haipatikani Madam lake 🤗

Ebu un lock kidogo bana
 
Huenda upo sahihi
 
Mentality ya kitoto na ya kishamba? Haya bwana hayo ni mawazo yako nayaheshimu. Uwe na siku njema!
Kwangu Mimi binafsi naiona hivyo aisee, lakini kama nilivyosema awali ni kutokana na aina ya jamii tuliyonayo.
 
Kwann ulazimishe kumuomba namba kama vip mpe yako akikupigia ni sawa akipotezea ni sawa wanaume lazima tuache ushamba wa namna hi ii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…