Akina Jemedari wamenawishwa kazi ya uwakala wa wachezaji

Akina Jemedari wamenawishwa kazi ya uwakala wa wachezaji

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Watafute kazi walizokuwa na ujuzi nazo. Baada FIFA na TFF kutaka wachezaji wasimamiwe na mawakala (agent) badala ya meneja asiekuwa na weledi wa kusimamia wachezaji.

Hii imekata ngede kwa machawa wa wachezaji, watafute kazi nyingine.
 
Bongo kwenye soka letu tumeshindwa kutofautisha, Mchambuzi na Mwandishi wa habari za michezo na vilevile tumeshindwa kutofautisha role ya meneja,mwanasheria na wakala wa mchezaji. Siku hizi watangazaji/wachambuzi ndio mameneja na kuna baadhi ya wanasheria ndio mawakala, yaani kama kawaida yetu kivyetuvyetu na kwa style yetu.
 
Bongo kwenye soka letu tumeshindwa kutofautisha, Mchambuzi na Mwandishi wa habari za michezo na vilevile tumeshindwa kutofautisha role ya meneja,mwanasheria na wakala wa mchezaji. Siku hizi watangazaji ndio maeneja na kuna baadhi ya wanasheria ndio mawakala, yaani kama kawaida yetu kivyetuvyetu na kwa style yetu.
Wachambuzi ndio mameneja
 
Kawatolea povu FIFA? Duh kweli kavurugwa
Ana kwambia fifa wamekurupuka...Kwa nchi za Africa mfumo wa uwakala hautofanya kazi Bora waendelee na mameneja wakati wanatoa mafunzo na semina mbalimbali yaani mfumo wa uwakala uongie taratibu sio kufungua ghafla ...mamaaaaae
 
Ana kwambia fifa wamekurupuka...Kwa nchi za Africa mfumo wa uwakala hautofanya kazi Bora waendelee na mameneja wakati wanatoa mafunzo na semina mbalimbali yaani mfumo wa uwakala uongie taratibu sio kufungua ghafla ...mamaaaaae

Ukipinga mabadiliko basi mabadiliko yakubadilisha wewe, yaani wasomi wakurupuke ilihali yeye mpayukaji awe sawa kweli?
 
Bongo kwenye soka letu tumeshindwa kutofautisha, Mchambuzi na Mwandishi wa habari za michezo na vilevile tumeshindwa kutofautisha role ya meneja,mwanasheria na wakala wa mchezaji. Siku hizi watangazaji ndio mameneja na kuna baadhi ya wanasheria ndio mawakala, yaani kama kawaida yetu kivyetuvyetu na kwa style yetu.
Edo Kumwembe anabaki kuwa Mchambuzi ninayemheshimu sana nchini. Yeye hufanya chambuzinzake ambazo zinabebwa na facts, humkuti kwenye migogoro na vilabu au wachezaji.
Upande wowote ule utakapigwa na uchambuzi wake huwa unaona suluhu pia isiyo na any bias
 
Ana kwambia fifa wamekurupuka...Kwa nchi za Africa mfumo wa uwakala hautofanya kazi Bora waendelee na mameneja wakati wanatoa mafunzo na semina mbalimbali yaani mfumo wa uwakala uongie taratibu sio kufungua ghafla ...mamaaaaae
Football ya Tanzania imekuwa sana ghafla, uwekezaji kwenye mpira ni mkubwa sana kiasi Cha timu zetu kugombania wachezaji na mabenchi ya ufundi na timu kubwa Africa. Hii ni ishara na indicator kuwa Sasa lazima mpira wetu professionalism kwenye nyanja zote. Itakuwa aibu na kusababisha hasira kubwa kuona mambo kama:
1. Mchambuzi anakuwa wakala
2. Mchezaji anamrukia na kumuumiza kipumbavu mchezaji ghali wa timu ya taifa ya nchi fulani.
3. Refa anachezesha mechi kwa kupendelea timu fulani kwa sababu yoyote Ile. Tuwe na waamuzi hodari kabisa wanaochezesha kwa kufuata kanuni za mpira.
4. Kiongozi wa mpira/TFF anakuwa na mahaba na upendeleo na timu fulani kwa sababu zake.
5. Mdhamini wa hovyo asiyetimiza mkataba.
6. Wachambuzi wa mpira wasiokuwa na weledi, wanaokatisha tamaa wachezaji na wadhamini kipumbavu utadhani wanachangia uendeshaji wa timu.
7. Viwanja vya hovyo vinavyohatarisha afya za wachezaji ghali wanaotegemewa na timu za mataifa Yao.
8. Kuwa na kanuni za ligi na ratiba ya ligi ya hovyo inayopendelea timu fulani TU au unsporting.
9. Zawadi ndogo za mashindano na wadhamini zisizofanana na gharama halisi za uendeshaji wa timu.
 
Back
Top Bottom