Football ya Tanzania imekuwa sana ghafla, uwekezaji kwenye mpira ni mkubwa sana kiasi Cha timu zetu kugombania wachezaji na mabenchi ya ufundi na timu kubwa Africa. Hii ni ishara na indicator kuwa Sasa lazima mpira wetu professionalism kwenye nyanja zote. Itakuwa aibu na kusababisha hasira kubwa kuona mambo kama:
1. Mchambuzi anakuwa wakala
2. Mchezaji anamrukia na kumuumiza kipumbavu mchezaji ghali wa timu ya taifa ya nchi fulani.
3. Refa anachezesha mechi kwa kupendelea timu fulani kwa sababu yoyote Ile. Tuwe na waamuzi hodari kabisa wanaochezesha kwa kufuata kanuni za mpira.
4. Kiongozi wa mpira/TFF anakuwa na mahaba na upendeleo na timu fulani kwa sababu zake.
5. Mdhamini wa hovyo asiyetimiza mkataba.
6. Wachambuzi wa mpira wasiokuwa na weledi, wanaokatisha tamaa wachezaji na wadhamini kipumbavu utadhani wanachangia uendeshaji wa timu.
7. Viwanja vya hovyo vinavyohatarisha afya za wachezaji ghali wanaotegemewa na timu za mataifa Yao.
8. Kuwa na kanuni za ligi na ratiba ya ligi ya hovyo inayopendelea timu fulani TU au unsporting.
9. Zawadi ndogo za mashindano na wadhamini zisizofanana na gharama halisi za uendeshaji wa timu.