City Of Lies
JF-Expert Member
- Sep 8, 2011
- 4,925
- 6,137
Sure.Chanzo hasa ni baba na mama kuishiwa upendo. Mana akijua upendo hakuna anageukia watoto na kumshutumu baba. Ndoa yenye upendo hayo hayatokei
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sure.Chanzo hasa ni baba na mama kuishiwa upendo. Mana akijua upendo hakuna anageukia watoto na kumshutumu baba. Ndoa yenye upendo hayo hayatokei
Mzee uko sahihi kwa asilimia 300....Laana inaweza kuonekana dhahiri au ikaonekana kwa kuyatafsiri maisha halisi ya mtu ! Kila nilipokuwa narejea nyumbani nilimpa kipaumbele mama kuliko baba! ,Na mama aliutumia udhaifu wangu kunisimulia Kila jambo baya la baba ili niendelee kumchukia baba! Mama alikuwa ana wezq kunisimulia matusi ambayo baba Huwa anamtukana na kamwe hakuwahi kunisimulia yeye ni matusi Gani amewahi kumtukana baba! Mama alikuwa na tabia ya kunionyesha makovu na ubaya wa baba ,ikiwemo baba Yako ni malaya sana ! Baba Yako hanipi Hela au haninunulii nguo nk ,lakini sikuwahi kumsikia baba akinisimulia kuhusu ubaya wa mama ,hata ningeshinda nae kutwa kucha hakuwahi thubutu kuniambia ubaya wa mama! Wanaume hufa kiume!! Niliyachukua maneno ya mama kama yangu nikamtenga baba .nikawa namtumia pesa mama TU !inaweza kupita hata mwaka mzima bila kuongea na baba lakini kila baada ya masaa matatu manne lazima nitaongea na mama ! Kuna wakati baba anaweza kuniomba Hela lakini mama akaniambia usimpe! Na mimi natii sauti ya mama! Nimejifunza jambo hasa baba alipofariki nimegundua niliegemea upande Mmoja . Lakini baba ndie alieumia zaidi kunisomesha na hata kujinyima Kila kitu, .wakati wa kunilipia ada nilimtafuta baba lakini nilipofanikiwa sikumtambuq Tena ! Nawewe unazaa ! Hicho unachomfanyia baba Yako na wewe utafanyiwa ! Na Kuna mikosi itakuandama hata kama unapata mshahara mkubwa namna Gani laana haiogopi kipato ! Mkumbuke babaako ,mkumbe babaako ,usisikilize malalamiko ya mama pekee ! Hiyo ni ndoa Yao .wewe angalia wajibu wako
AminInavyoonekana Hata kama Mwanaume atakuwa amekosea kwa sehemu lakini wewe mwanamke unatakiwa ujue jinsi ya kushughukia jaribu hilo kwa hekima na subira nyingi bila kuathiri heshima yake huyo Mwanaume wako.
Respect is fundamental in every strong relationship.
Kumheshimu mtu ni kumfanyia lile lenye kufaa na lenye kumpendeza.
FactMwanamke ambae anashindwa kushughulikia tofauti zao kati ya yeye na mumewe au Mwanaume wake na kuanza kuingiza watoto kati na kuwafanya wamuone Baba yao ni mkosefu ili wamchukie ni mwanamke mjinga na mpumbavu.
Wanawake wanatakiwa wapate mafundisho ya imani Kwa usahihi, Psychology and the related.
Waache mapokeo.