Akina mama wakimasai wamwambia Samia asiwaondoe katika ardhi yao ya asili ya ngorongoro.

Nimekumbuka sekeseke la kupanga watu kwenye vijiji vya ujamaa enzi za Nyerere!
 
Mambo mengine tuwe serious kweli na tuwe na maono ya kuona mbali.Wamasai wa ngorongoro ni haki yao kukaa pale sbb ilikuwa maeneo yao ya asili lakini kwa upande wapili serikali ipo halali kuwahamisha sababu ya mabadiliko ya tabia ya nchi na uharibifu wa mazingira.MASAI alikuwa na ngombe wachache na wao walikuwa wachache leo wanamifugo wengi wamejaza hifadhi wao wenyewe kuliko wanyama nao wao pia wamekuwa wengi.je tuhifadhi wanyama hao mifugo ya wamasai?masai walikuwa hali nyama ya porin leo masai anashndana na simba kula wanyama wa pori.wamasai wanapaswa kuhama ili amilike eneo kuliko kwnye hifadh ambapo haruhusiwi kumilik wa kujenga nyumba.kwa manufaa ya nch wamasai wanatakiwa kuhama.
 
Huku wakibeba mabango ya kutuma ujumbe kwa rais Samia, akina mama wa kimasai wameishutumu serikali ya Samia ya kuwalazimisha kuondoka ngorongoro na kwenda huko Tanga.

Wakitumia kauli za uchungu wa mwanamke kwa mtoto wake. Mama mmoja wa Kimasai akasema yeye ni mzazi na ni mama kama Samia, kwa nini Samia anakuwa anawaganyia mambo haya kutumia maguvu kuwaondoa katika ardhi yao.

Mama huyo wa kimasai akaendelea kusema, watoto wao wamelazimika kukimbia makazi yao kwa sababu kuna majeshi yanatumwa huko kuwaaondoa kinguvu. Akasema wakati watoto wao wanalala maporini katika hatari, yeye Samia watoto wake wako wanaishi raha mustarehe.

Wamasai wakamalizia kwa kusema kuwa, hawataki kuondoka kama ni kufa kheri wafe katika ardhi yao lakini hawataki kwenda huko Tanga.

Unaweza kuwasikiliza hapa.

View attachment 2729379
Maza kwa kweli ameshindwa mambo mengi sn
 
Kwani wamekwambia wanataka kumiliki ardhi? wao wanataka kuishi basi
 
Katika watu ambao sio wakutetewa kabisa ni hawa masai wao waliamua kujiweka mbali kabisa na siasa nakuona maisha huwa yanaenda tu kumbe maisha ni siasa
 
Waache kujaza wamasai wa Kenya na kuwaficha huko.
 
Maigizo tu hayo.
Mtu mwenye akili anang'anganiaje kukaa poring kusipo na huduma zozote anaacha kukaa kwenye nyumba na sehemu yenye huduma zote?

Hawa ni wajinga tu na watahama tu. Walihamishwa kimara sembuse hawa? Hawa kina nani tena kimara tulihama bila fidia yeyote?
Wewe ni mjinga ila hujui ni hasara kwako na familia yako
 
Huku wakibeba mabango ya kutuma ujumbe kwa rais Samia, akina mama wa kimasai wameishutumu serikali ya Samia ya kuwalazimisha kuondoka ngorongoro na kwenda huko Tanga.

Wakitumia kauli za uchungu wa mwanamke kwa mtoto wake. Mama mmoja wa Kimasai akasema yeye ni mzazi na ni mama kama Samia, kwa nini Samia anakuwa anawaganyia mambo haya kutumia maguvu kuwaondoa katika ardhi yao.

Mama huyo wa kimasai akaendelea kusema, watoto wao wamelazimika kukimbia makazi yao kwa sababu kuna majeshi yanatumwa huko kuwaaondoa kinguvu. Akasema wakati watoto wao wanalala maporini katika hatari, yeye Samia watoto wake wako wanaishi raha mustarehe.

Wamasai wakamalizia kwa kusema kuwa, hawataki kuondoka kama ni kufa kheri wafe katika ardhi yao lakini hawataki kwenda huko Tanga.

Unaweza kuwasikiliza hapa.

View attachment 2729379
Wanatumiwa kisiasa tu, tulisoma {rimary School kuwa hao hawana asili ya popote Tanzania, ni wahama hamaji.

Hawawezi kuwachwa kuishi ndani ya hifadhi ya dunia.
 
Wewe ndo mjinga. Suala la watu kuhama Tanzania limeanza leo? Unajua watu walihamishiwaga kwenda vijiji vya ujamaa miaka ya 1967 - 1974?

Wao kina nani wasihame?
Tena kwa nguvu, ukitaka usitake na hajashauriwa wala kuulizwa mtu. Wengi walikufa kwa maradhi, kwa kuliwa na Simba, kwa kugongwa na nyoka, na wengine waliliwa mpaka na chatu.

Hao wanahamishwa Kistaarabu na nyumba wanajengewa, leo wanasiasa wajinga wajinga wanawatumia kisiasa.
 
Wakazie hapohapo

Mtu unaondokaje sehemu yako ya asili?

Wamasai simameni waTanganyika tuko nyuma yenu
 
Tena kwa nguvu, ukitaka usitake na hajashauriwa wala kuulizwa mtu. Wengi walikufa kwa maradhi, kwa kuliwa na Simba, kwa kugongwa na nyoka, na wengine waliliwa mpaka na chatu.

Hao wanahamishwa Kistaarabu na nyumba wanajengewa, leo wanasiasa wajinga wajinga wanawatumia kisiasa.
Hawa wanaharakati uchwara na watoto wa juzi wana shida sana
 
Back
Top Bottom