Akina mama wakimasai wamwambia Samia asiwaondoe katika ardhi yao ya asili ya ngorongoro.

Waraka umewapa nguvu ya kukataa kuonewa...go go waraka goooooooo.
 
Tumia akili yako kwanza kufikiri. Ulipewa akili uweze kuitumia vizuri.
Tusifanye kila jambo liwe la kubishana tu hapa, mradi tu tumeshikiria nadharia fulani zinazotuendesha.
Hili ndo jibu la swali langu kwako?
 
Haya mkuu, tunapata pesa kiasi gani? Zinatumikaje? Tunajuaje hawachimbi madini, kukata miti, kuchukua wanyama, mbao? Tunapewa taarifa yoyote kuhusu hili?

Wapi duniani unaweza kuingia dili kama hili? Ulaya, Amerikas, Uarabuni, China, kwa wahindi?
Umetaja mambo muhimu sana kwa kutumia maneno machache. Haya uliyoeleza hapa ndio udhaifu mkubwa sana unaotuandama kama nchi.
 
Hili ndo jibu la swali langu kwako?
Ndiyo.
Kwani huoni maana yangu ninayolenga uijue?

Wewe ni mtu uliyekwisha jitambulisha hapa unacho kisomo cha kutosha na kuwa na uwezo wa kutumia elimu hiyo kufikiri vyema na kutatua matatizo.

Tumia hiyo elimu sasa, upate jibu.
 
Magufuli hakujua chochote kuhusu uchumi na biashara,siyo rejea sahihi,alikwambia gharama za utafiti mpaka uchimbaji!?..kwa nini hakutoa pesa hazina na kuwekeza kwenye nchi kuchimba rasilimali zake ili tunufaike!?
Wewe ni utoko halisi
 
Ndiyo.
Kwani huoni maana yangu ninayolenga uijue?

Wewe ni mtu uliyekwisha jitambulisha hapa unacho kisomo cha kutosha na kuwa na uwezo wa kutumia elimu hiyo kufikiri vyema na kutatua matatizo.

Tumia hiyo elimu sasa, upate jibu.
Niambie wewe tofauti ni ipi?
 
Bulyanhulu nilikuwepo,mkapa alikuja na kusema,nataka wabakie ndege tu hapa,hakika watu walikufa sana,baadhi ya watu walifukiwa kwenye mashimo kwa wale walijifanya kichwa ngumu
Naye amewafuata ! Sijui timbwili lilikuaje 🙏
 
Nimekumbuka sekeseke la kupanga watu kwenye vijiji vya ujamaa enzi za Nyerere!
Ile sekeseke iliumiza lakini pia ilileta neema baadaye kwenye huduma muhimu za kijamii !
 
Wewe ndo mjinga. Suala la watu kuhama Tanzania limeanza leo? Unajua watu walihamishiwaga kwenda vijiji vya ujamaa miaka ya 1967 - 1974?

Wao kina nani wasihame?
- baada ya Hao watu kuhama miaka hiyo ya 60s na 70s tija yake ilikuwa nini
 
Nyerere alihamisha wazee wetu Kwenye vijiji vyao vya asili kwa mtutu wa bunduki mwaka 1974.
Watu walihamishwa nchi nzima kwa madai ya kulundikwa pamoja ili tuletewe maendeleo.

Zoezi hilo la vijiji vya ujamaa lilikiuka haki za binadamu kwa kiwango kikubwa.
Wananchi walitupwa nyikani, hakukuwa na maji, umeme wala barabara.
Watu wamelala nje kwa siku kadhaa, wameliwa na Simba, chui, chatu nk. Hawa ndugu zetu wa Ngorongoro wanahamishwa kistarabu, wanapata nyumba, zenye miundombinu wezeshi, mashamba na maeneo kuchungia., tofati kabisa na vile alivyofanya baba wa taifa mwaka 1974.
Serikali inafanya hili kupisha uhifadhi, shida iko wapi? Serikali iendelee na mchakato huo, maana suala la uhifadhi limegusa jamii mbalimbali zilizo karibu na hifadhi zetu nchi nzima.
 
Nyerere alikosea japo alikuwa na nia nzuri, SSH anakosea,sina uhakika nia yake, anajali zaidi maslahi ya waarabu, dini, kuliko maskini Wamasai .

Wewe ukihamishwa ulipoishi kwa miaka elfu tano utajisikiaje?
 
Mungu sikia hiki kilio cha wajoli wako wasio na nguvu mbele ya wenye mamlaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…