Akumbukwe John Okello, Baba wa Taifa la Zanzibar. Bila huyu leo Zanzibar wangekuwa bado Utumwani

Mzee siku hizi umekuaje, wakati huo si kwamba lazma uwe na jeshi bali uwe na uwezo wa kuwaongoza wenzio katika harakati kama hizo .John Okello akataliwi kwa misingi ya ukweli wa mambo au Historia bali kwasababu ya udini (dini) yake ,jina na nchi alikotoka. Na ajabu ni kua Okello anakataliwa na mabaki ya wana wa Sultan ingawa wajuvi na wajuzi wa ukwweli wa mambo ya Historia za mapinduzi kamwe hatuwezi kumuacha John Okello.
 
Bishweko,
Nimemweleza John Okello kama nilivyomtafiti.

Si lazima uniamini.
 
Bishweko,
Nimemweleza John Okello kama nilivyomtafiti.

Si lazima uniamini.
Wala swala sio kukuamini ,kumbuka katika utafiti wako tayari ulikua na upande na fikra hasi dhidi yake. Kwahiyo atuwezi kutarajia mazuri au ukweli kutoka kwako. Lakini pia kumbuka kuna wengi tunaofanya kazi za kitafiti kuhusu mapinduzi ya Znzibara na Harakati za kutafuta Uhuru wa mwana wa Afrika . John Okello aliongoza wenzie kufanya mapinduzi dhidi ya Sultan Jamshid na kuiweka Zanzibar huru.
 
Najua humpendi shujaa okelo kwa sababu sio muislamu na hakutokea kariakoo!!!Sources zako za habari watu wa ASP na TANU hatuzikubali labda wanachama wa hizbu
 
Facts
 
Bishweko,
Unao ushahidi kuwa nimeingia katika utafiti tayari nikiwa na matokeo ya utafiti?

Ikiwa unao tafadhali weka hapa jamvini sote tunufaike.

Hiyo mosi.

Pili unasema umefanya utafiti kuhusu mapinduzi ya Zanzibar.

Tafadhali tuwekee hapa hicho ulichotafiti juu ya Okello tunufaike sote.

Kuwa Okello "aliongoza," mapinduzi unahitaji kuwafuta waliopanga mapinduzi kutoka Tanganyika na Zanzibar tena ndani ya serikali na vyombo vya usalama.

Unahitaji pia kuwafuta walioweka kambi ya Kipumbwi ambao sasa si siri wote wametajwa katika kitabu cha Dr. Harith Ghassany "KwaheriUkoloniKwaheriUhuru": Ali Mwinyi Tambwe, Jumanne Abdallah, Mohamed Omari Mkwawa na, Victor Mkello.

Upande wa Zanzibar nakuachia wewe ututajie kwani umetafiti historia ya mapinduzi.

Hii itatusaidia kulinganisha uyajuayo wewe na ninayoyajua mimi na yangu tayari yapo kitabuni watu wanayajua sasa zaidi ya miaka 10.
 
Najua humpendi shujaa okelo kwa sababu sio muislamu na hakutokea kariakoo!!!Sources zako za habari watu wa ASP na TANU hatuzikubali labda wanachama wa hizbu
Nelson...
Ikiwa hukubali sawa hakuna neno.

Hapa tunabadilishana fikra na kuna wenzetu wanatusoma.

Hili ndilo muhimu.
 
Naweka siti ya kupata madini ya wataalamu.
Che...
Nakuwekea hapo chini historia ya Okello:

''Okello was not a participant in the Mau Mau uprising but he used the reputation of this resistance movement to strengthen his own position.

On 14 January 1964, Okello proclaimed, “I was a very high ranking person in Kenya in the Mau Mau Army which knows how to make weapons . . . . I

n fact, I can easily make no less than 500 guns per day. I can beyond doubt make a bomb that can destroy an area of three square miles.

I can make about 100 grenades in an hour.” 51 In his book, Okello reports that in a discussion with some African fishermen on his way to Unguja Island in February 1963, he explained that they would soon see “Arab colonialists eliminated.”

They did not believe that was possible, remarking that “perhaps the ‘Mau Mau’ from Kenya” could do such a thing, but “no one can dare attack the imperialists here.”52

Both these stories 50 Smith 1973: 107–8 51 BBC Written Archives, Summary of World Broadcasts Part IV The Middle East and Africa. 52 Okello 1967: 90 155 help explain that Okello used the Mau Mau movement metaphorically, for its psychological value of striking fear into the hearts of both British and Zanzibaris, given the British view of the Mau Mau as uncontrollable atavistic savages.

For his African audience, Okello also claimed a connection with the Mau Mau on the radio to give himself credibility as a guerilla leader, since the Mau Mau were a symbol of African guerilla fighters who could bring down imperialists.53

Given that he had no military or police training or experience, he needed to make himself look more prepared than he was.54

This type of misinformation was passed along not only by newspapers but by British and American intelligence reports.

Don Petterson, the vice consul at the U.S. embassy in Zanzibar at the time of the revolution, comments on the process of information gathering, indicating that the British MI5 accepted information with little discernment and the Americans banked on the good name of MI5 and parroted it.55

Despite all the evidence that he was none of these, the myths of Okello as Mau Mau fighter, Zanzibari policeman, World War II veteran, King’s African Rifles soldier, and Cuban-trained revolutionary are still quite active.

That these myths persist elucidates how this untrained, uneducated man played such a fundamental role in overthrowing the government of Zanzibar.

His supporters proudly claim he was a soldier because it adds to his prestige.56

His detractors are convinced he had military training because the 53 It did not matter that the Mau Mau technically “lost” their campaign; they fought the British, and Kenya got its independence as a result.

And East Africans knew that the British were afraid of the Mau Mau. 54 All the Ugandan elders who knew Okello, as well as a Ugandan military historian, confirmed that he was never in the King’s African Rifles or the Ugandan military.

Additionally, Okello was not a policeman in Zanzibar (BNA DO 185/59 and RHL MSS. Afr. s. 1446). 55 Petterson 2002: 74–5 56

His wife’s son proudly told me that Okello was in KAR, and fought in World War II.

Interview with Moses Onyok, 20 January 2014;

Another informant said Okello was chosen to lead the revolution because he 156 idea of a barely literate mainlander, such as Okello, having the ability to topple a government of more sophisticated and better-educated men was difficult to believe; this feat was incongruous with Zanzibari exceptionalism.''

Source: Anne Lee Grimstad Dissertation 2018 Univerity of Florida - ''Zanzibar The Nine-Hour Revolution.''


Anne Lee Grimstad akizungumza na mke wa Victor Mkello nyumbani kwake Nguvumali, Tanga wakati wa utafiti
(Mohamed Said alikuwa mwenyeji wa Grimstad picha kwa hisani yake)​
 
Hata hivyo Mzee saidi, Okello alikuwa sehemu ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 64.
Hapa namaanisha alishiriki kikamilifu kabisa katika harakati na vita iliyo angusha utawala wa Sultani.

Ukisoma kitabu chake cha
"Revolution in Zanzibar"
Unaona kabisa ushiriki wake mkubwa katika harakati hizo.

Mi naona kwasababu ya kuwa Okello sio Raia wa Zanzibar, ndio maana mchango wake haukuthaminiwa wala kutambuliwa na viongozi wa Zanzibar.

Okello ni raia wa Uganda, nadhani wanamapinduzi wa Zanzibar hawakutaka kumpa sifa au hadhi aliyostahili kwakuwa tu sio Mzanzibari.

Nipo
 
Hata hivyo Mzee saidi, Okello alikuwa sehemu ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 64. Hapa namaanisha alishiriki kikamilifu kabisa katika harakati na vita iliyo angusha utawala wa Sultani...
Che...
Hakuna uhakika kama kitabu hicho chake ni mkono wake ulioandika.

Mohamed Omari Mkwawa alishiriki katika mapinduzi lakini hatambuliki hali kadhalika Victor Mkello, Ali Mwinyi Tambwe, Aboud Mmasai wengi tu.

Nimekuwekea hiyo ili uone vipi Mkello alivyokuwa anasema maneno ya uongo katika radio alipopewa nafasi.
 
Che...
Hakuna uhakika kama kitabu hicho chake ni mkono wake ulioandika.
Kwanini kusiwe na uhakika kuwa aliandika kitabu hicho? Kuna mtu amewahi kujitokeza na kusema kuwa ni yeye aliandika kitabu hicho na si Okello?
 
Father...
Okello alikuwa fedheha kwa ASP.

Maneno aliyokuwa anatoa yalimfanya Karume na mapinduzi yawe kichekesho...
Mzee asalam aleikum,hii ni February 2023 huu mjadala umeletwa January kwa bahati mbaya nilichelewa kuuona..kila mtu kaweka hoja yake humu kwa jinsi anavyoelewa yeye mchango wa John okelo

Lakini sasa kupitia hoja yako hii ya kusema Okello hakuwa kiongozi wa mapinduzi mbona inapingana na ushahidi wa video iliyoletwa hapo juu?

Kwenye video inaonekana wazi kwamba karume na Babu wanakubaliana kwamba John ndio aliyeongoza mapinduzi na hata mwandishi anauliza swali linalohusiana na hilo...ajenda yako ni ipi kwa kujaribu kuficha ukweli huu!?
 
Mzee asalam aleikum,hii ni February 2023 huu mjadala umeletwa January kwa bahati mbaya nilichelewa kuuona..kila mtu kaweka hoja yake humu kwa jinsi anavyoelewa yeye mchango wa John okelo....
Tad...
Hiyo video ndiyo inasema kuwa Okello ndiyo kiongozi wa mapinduzi?

Ushahidi wako ni mazungumzo hayo?

Inabidi usome historia ya mapinduzi kuweza kujua ukweli.
 
Tad...
Hiyo video ndiyo inasema kuwa Okello ndiyo kiongozi wa mapinduzi?

Ushahidi wako ni mazungumzo hayo?
Inabidi usome historia ya mapinduzi kuweza kujua ukweli.
Come on mzee wangu! Kwenye hiyo video swali la pili la mwandishi linamdondokea John Okello baada ya swali la kwanza kujibiwa na karume muendelezo wa swali anaulizwa John Okello mwandishi anauliza "by what means mr Field marshall as the LEADER of the revolution army......" hadi hapo hujaamini kwamba John alikuwa ni kiongozi wa jeshi la mapinduzi!? You have to fheck the video mzee,

Halafu kingine kuna hoja nimeiona hapo juu unasema jina la field marshall Okello alijipachika mbona hapo mwandishi anamuita kabisa field marshall kuonyesha ni kwamba ni jina lililozoeleka hapo kisiwani kabla hata ya zoezi la mapinduzi kufanyika!?

Mzee historia ya maandishi siku zote ina mapungufu maana kila mtu atakuja na andiko lako huku akijificha kwenye kichaka cha utafiti alioufanya,hiyo video ilikuwa ni ushahid tosha kuonyesha ushiriki wa Okello katika mapinduzi..

Narudia tena historia ya kwenye maandishi yenu yana upotoshaji mkubwa sana na mara nyingi hubeba interest za mtu au kundi fulani..Nadhani hata wewe unajua kwa kiasi gani maandishi yamekuwa yanatudanganya juu ya historia ya uhuru au hata historia ya Mkwawa...

Hitimisho Okello kashiriki kwa kiasi kikubwa sana hayo mapinduz na ndiye aliyeongoza jeshi la mapinduz utake usitake huo ndio ukweli jaribu kuwa hata na aibu
 
Tadpole,
Haya mimi nina uzoefu mkubwa.
Historia ya Tanganyika ina matatizo makubwa sana.

Iliaminika kuwa historia ya TANU ni Julius Nyerere hadi nilipoandika kitabu cha Abdul Sykes.

Soma kitabu cha Dr. Harith Ghassany "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru," (2010) kuhusu mapinduzi.

Pdf ipo hapa mtandaoni.
 
Tadpole,
Haya mimi nina uzoefu mkubwa.
Historia ya Tanganyika ina matatizo makubwa sana...
Nimekwambia tangu mwanzo siwez kusoma kitabu ambacho mara nyingi kinakuwa na interest na kundi/mtu fulani....

Suala lilikuwa ni video umeangalia hiyo video kuona kile ambacho nimekwambia ya kwamba kwenye mahojiano Okello anatambulika kuwa ni kiongozi wa jeshi la mapinduzi!?
 
Tad...
Ikiwa huwezi kusoma basi si tatizo.

Mimi katika maisha yangu nimekuwa sichagui katika kutafuta elimu nasoma kila kitu isipokuwa matusi.

Ndiyo sababu nimekuwa hivi.

Ikiwa utakuwa unasoma vile unavyopenda ndiyo hivyo leo unaamini hadithi ya Okello.

Ungemsoma na Ghassany ungemsoma Abeid Mmasai na wengine hawajatajwa katika historia ya mapinduzi.

Mwisho ungejiuliza mbona Kassim Hanga hatajwi katika historia ya mapinduzi ilhali yeye ndiye alikuwa kiongozi mkuu wa mapinduzi?

Kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika ungejiuliza mbona Ally Sykes TANU Card No. 2 na kaka yake Abdul Sykes TANU Card No. 3 hawatajwi kwenye historia ya TANU?

Ikutoshe baba yao Kleist Sykes ndiyo aliyeasisi African Association 1929 na ndiye aliyejenga ofisi ya TAA ilipozaliwa TANU 1954.

Vipi historia nzima inamtaja Nyerere peke yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…