Ni kweli, nilimuuliza Sheikh Said ikiwa Mapinduzi ni halali au ni haramu. Sijawahi kupata jibu zaidi ya ku'dance'
Kuna ''Mwarabu wa London'' Bw Rajab, yeye alijaribu lakini pia hakuwa na jibu la moja kwa moja.
Katika gazeti la Raia mwema, alisema ' kwamba ni halali au haramu inatagemea mtu yupo upande gani''
Ni nadra kumsikia Jussa akitamka neno Mapinduzi lakini ni kawaida sana kumsikia Mansour Himid akitamka.
Mifano hiyo inaonyesha sensitivity ya jambo zima na linavyowagawa Wazanzibar hasa kwa rangi na nywele
Niliwahi kumuuliza Mo ikiwa Mapinduzi ni haramu na yalifanywa na Watu kutoka Tanganyika kambi ya Kipumbwi, je, Wazanzibar wanaosherehekea wanafanya makosa kutukuza haramu?
Hakuna jibu hadi kesho, ana 'dance' tu
Kwa bahati mbaya katika wale 12 wa Baraza la Mapinduzi wengi wametangulia mbele ya haki, waliobaki wachache ni A.H.Mwinyi sina habari za Kanali S.Bakar. @JokaKuu kama una taarifa zaidi tafadhali
Wanamapinduzi 12 hawakuacha nyaraka kwa kimaandishi kama vitabu vya kueleza nini kilijiri, sijui kama walikatazwa au la. Tunabaki na simulizi za upande mmoja kutoka Oman au mrengo wa Kiimani.
Kinachosikitisha ni chombo kama TBC kinachoendeshwa kwa kodi zetu kinatumiwa 'kiharamia'
Tido alilipa gharama pia kwa kutaka kuiweka TBC huru. Aliahidi kuonyesha chaguzi mubashara. CCM hawakubaliani na mambo ya kwenye mwanga, wanapenda mambo kizani, Tido akalipia gharama.
Lakini pia kuna kauli nimeisikia na hapa Mohamed atanisahihisha kwamba ' kuna nyakati heri inafichwa ndani ya shari'' kule Buckingham palace wanasema '' a blessing in disguise' , Tido is better off today.