Al Ahly 1-0 Simba | CAFCL | Al Salam Stadium

Al Ahly 1-0 Simba | CAFCL | Al Salam Stadium

Nimeridhishwa na kiwango cha simba ugenini, siwezi kulaumu, na moyoni mwangu najisikia amani kabisa.

Mpira wameupiga mwingi mno, na kwa jinsi Simba walivyocheza bila lwanga na kufungwa goli moja tu, kama hii ndo ingekuwa Robo fainali basi Al ahly wangekuwa hawana matumaini ya kuendelea tena.


SIMBA CHAMA KUBWA. Nguvu moja[emoji123]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wamepigwa kimoja cha asubuhi walah
Sio khamsa tena?[emoji23] Kwa huu mpira uliopigwa, sidhani kama kuna shabiki yoyote wa Simba alieumia.Jaribu kuwaza kama hii ndo ingekuwa Nusu fainali, afu ndo tumeanza kwao kama hivyo yaani hapo fainali ilikuwa ni uhakika kabisa[emoji23].


Kama kuna shabiki yoyote wa Simba, alie athirika na haya matokeo basi atakuwa ni wakuja tu. Hii simba msimu huu ipo CCL kupambana kwelikweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mamelodi kapigwa mbili kavu nyumbani sisi ni nani mpaka tupigwe kamoja tu na wale mafarao na tupo ugenini ...
hebu tujipige pige kifua na kusema sisi ni washindi.
Kwanza mazingira ya kigoli chenyewe ni zali tu, upepo tu uliwapitia hakuna skills pale
 
Kama mamelodi kapigwa mbili kavu nyumbani sisi ni nani mpaka tupigwe kamoja tu na wale mafarao na tupo ugenini ...
hebu tujipige pige kifua na kusema sisi ni washindi.
Hao waliompiga mamelod home ndio tunakutana nao? Au kuna draw itachezeshwa?
 
Back
Top Bottom