Al-Barzakh: Haya ndio Maisha ya Kaburini baada ya kufa

Unataarifa story za adhabu ya kaburi muhammad alitoa kwenye story ya mwanamke wa kiyahudi alikuwa anamuadithia Aisha ,tena fairy tale stories za kiyahudi?
 
Embu nioneshe surah moja moja ya vitabu kama vitano vya mitume wa waislamu, vipi kama laki na 20 ila mi nataka tuanze na vitano tu kwanza
1. Torati( nabii musa)
2. Zaburi( nabii daudi)
3. Injili( nabii issa)
hivo ni vitabu ambavyo vinatumiwa na baadhi ya imani zisizokuwa ya kiislam mpaka sasa
4. Qur'an( ilipoteremshwa quran hivo vitabu vya nyuma vilifutwa ikawa havitumiki katika umma huu wa mtume Muhammad na sio kama havipo lakini havitumiki kwasababu yale mafunzo na sheria na miongozo inayopatikana katika vitabu hivyo yote ipo katika quran na kuna watu walibadilisha baadhi ya maana katika hivyo vya nyuma ndio maana Allah akataka quran iwe ndo kitabu chenye kufuatwa kwa umma huu wa mtume Muhammad rehema na amani iwe juu yake.
pia kuna kurasa alizofunuliwa nabii ibrahim na musa
sisi waislam tunaamini mitume ni wengi l kama anavyosema Allah "Na Rusuli Tuliokwishakusimulia kabla; na Rusuli (wengine) Hatukukusimulia.[An-Nisaa: 164] "

tuliofahamishwa ndani ya quran ni 25 tu na inatupasa kuamini hivo. ambao ni


1. Aadam

2. Idriys

3. Nuwh

4. Huwd

5. Swaalih

6. Ibraahiym

7. Luwtw

8. Ismaa'iyl bin Ibraahiym

9. Is-haaq bin Ibraahiym

10. Ya'quwb bin Is-haaq bin Ibraahiym

11. Yuwsuf bin Ya'quwb bin Is-haaq bin Ibraahiym

12. Shu'ayb

13. Ayyuwb

14. Dhul Kifl

15. Muwsaa

16. Haaruwn nduguye Muwsaa

17. Daawuwd

18. Sulaymaan bin Daawuwd

19. Ilyaas

20. Alyasaa'

21. Yuwnus

22. Zakariyyaa

23. Yahyaa bin Zakariyyaa

24. 'Iysaa bin Maryam

25. Muhammad

(Swalla Allaahu 'alayhim wa sallam)

na katika hao tuliofahamishwa waliopewa vitabu ni hawa na vitabu vyao

1. Torati ilifunuliwa kwa Nabii Musa (a.s.)
2. Zaburi ilifunuliwa kwa Nabii Daudi (a.s.)
3. 3. Injili ilifunuliwa kwa Nabii Isa (a.s.)
4. Qur'an ilifunuliwa kwa Mtukufu Mtume
Muhammad Rehma na amani iwe juu yake
6. Kitabu hiki yaani Qur'an haina kosa hata
moja, maneno na ahadi zake zote ni kweli
tupu.
Sisi tunaenda kwa vile tulivyofahamishwa na quran na sunna za nabii wetu na si zaidi ya hivyo wala hatudadisi yale ambayo si katika uwezo wetu wa kuyajua.
Na Allah anajua zaidi..
Allah akuongoze
 
Unataarifa story za adhabu ya kaburi muhammad alitoa kwenye story ya mwanamke wa kiyahudi alikuwa anamuadithia Aisha ,tena fairy tale stories za kiyahudi?
Na waliopita kabla yako pia walisema hayo unayoyasema kabla ya hata Huyo mtume wa Allah Muhammad rehema na amani ziwe juu yake.
"Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wale waliokufuru husema juu ya haki inapowajia: Huu ni uchawi ulio wazi"
"Au wanasema: Ameizua! Sema: Ikiwa nimeizua mimi, basi nyinyinyi hamwezi kunifaa chochote mbele ya Mwenyezi Mungu."
So walishasema hayo kabla lakini baadae yakawafika yale Allah ambayo waliyaahidi na laiti wangelirudi wangekupeni izo khabari lakini Allah hajaruhusu hivo. Muhimu ni kuamini na kujua kuwa adhabu ya kaburi ipo na sio kaburi tu bali kuna siku mtu atalipwa kutokana na alichokichuma katika dunia hii ..ikiwa ulifanya kheri zinazomridhisha Allah utafanikiwa na kinyume chake ni khasara.
Allah akuongoze
 
Apa tunaongea kwa ushahidi na nukuu , umesema vitabu vipo , na kuwa makini tunazungumza vitabu vya waislamu kabla ya Muhammad

Nimekuomba surah moja moja kwa vitabu vi Tano tu sijataka utaje taje majina ya mitume wa waislamu

Kama hakuna nenda karekebishe ulipo sema vipo
 
Muhammad alikuwa hajui adhabu ya kaburi mpaka alipopewa stroy na Aisha ambazo Aisha alisimuliwa na mwanamke wa kiyahudi tena fairy tale stories Yani ni fiction sio za kweli
 
Acha usanii wako wewe, kaburini hakuna maisha, mwili unaoza fahamu zinaondoka unakuwa sawa na mtu aliyelala usingizi "fo fo fo"
Kama kaburini hakuna maisha ilikuwaje Lazaro na tajiri walipokufa Lazaro akamuona tajiri anavyoteseka na moto wa Jehannam?
 
Ni kwamba hujanielewa ndugu yangu hiyo taurati injili zaburi vyote vilituma na waislam wa kabla ya mtume Muhammad baada ya hapo washirikina wakavibadilisha maana katika baadhi ya aya, Allah akamteremshia quran mtume Muhammad iwe ndo muongozo wa umma huu,, na nimekuambia pia tumefahamishwa hayo ndani ya quran na si zaidi ya hapo..ukitaka aya moja moja torati ipo na aya nyingi. Zaburi ipo na aya nyingi na injili ipo na aya nyingi na bibilia pia. Cwezi kuandika zote hapa nipe namba yako ya whatsapp nikufafanunulie moja baada ya jngne huenda Allah akakuongoza
 
Hakuna kitabu kilichopotea..vitabu vyote vipo
Nimekutaka uweke surah moja moja ya vitabu ata vi 5 tu sio utaje majina ya mitume wa kiislamu

Kumbuka Allah alituma mitume laki na 20 Mimi sijataka majina yao
 
Wewe ndio unashindwa kunielewa ukishadai vitabu vya waislamu wa zamani kabla ya muhammad vipo, sasa unapotaja biblia tena unakuwa anachanganya , jikite kwenye mitume waislamu
 
Nimekutaka uweke surah moja moja ya vitabu ata vi 5 tu sio utaje majina ya mitume wa kiislamu

Kumbuka Allah alituma mitume laki na 20 Mimi sijataka majina yao
Mimi nimeongelea vitabu vingaoi vilivyokuwepo au wapi nimesema mitume wote wameshushiwa vitabu. Nimekufahamisha na kukuambia kuwa mitume ni wengi waliokuja kutokana na mafundisho ya sunna za mtume..Tuliofahamishwa katika quran ni 25 na si zaidi. Na hakuna muislam atakutajia zaidi ya hapo. Na waliopewa vitabu tukafahamushwa ninwatano ambao nimekutajia na majina ya vitabu vyao nimekutajia na aya zake zipo ndani ya hivyo vitabu na vinatumika pia na baadhi ya imani. Nikakuambia alipotumwa mtume Muhammad rehema na amani Allah alivifuta vitabu hivyo na akleta quran ambayo ndo uwe muogozo wetu
 
Ni kwamba hujanielewa ndugu yangu hiyo taurati injili zaburi vyote vilituma na waislam wa kabla ya mtume Muhammad baada ya hapo washirikina wakavibadilisha
Washirikina waliwezaje kuwakwapua vitabu waislamu alafu wakavibadili? Je waislamu hao hawakuwa ata na nakala moja original?
 
Ikiwa mwili utaoza ni kipi Kinachomfanya Firauni aliyejiita MUNGU asioze hadi leo karne na karne?
Mie ni muislam, ila hiyo dhana ya kusema Firaun akizikwa mwili wake unatemwa na ardhi na wadudu wamegoma kuula mwili wake ni uongo mtupu.

Yule amekaushwa na binadam wenzake kama wengine walivyokaushwa.
 
Sawa vitabu vilibaki vitano , tuwekee surah moja moja kaitka kila kitabu
 
quran ina miaka 1500,biblia ina miaka 2000 shinto ina miaka 5000 punguza mihemko ongea reality,acha kukremisha uliyomezeshwa madrasa na ustazi
 
Swala Alie liwa na chui na kuacha mtoto wake ndogo nae analipwaje?maana nae Ni kiumbe
 

Kwahiyo ambao walikufa/watakufa kwa Yesu ndio watakao fufuka.Vipi wale wengine itakuwaje ?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…