Embu nioneshe surah moja moja ya vitabu kama vitano vya mitume wa waislamu, vipi kama laki na 20 ila mi nataka tuanze na vitano tu kwanza
1. Torati( nabii musa)
2. Zaburi( nabii daudi)
3. Injili( nabii issa)
hivo ni vitabu ambavyo vinatumiwa na baadhi ya imani zisizokuwa ya kiislam mpaka sasa
4. Qur'an( ilipoteremshwa quran hivo vitabu vya nyuma vilifutwa ikawa havitumiki katika umma huu wa mtume Muhammad na sio kama havipo lakini havitumiki kwasababu yale mafunzo na sheria na miongozo inayopatikana katika vitabu hivyo yote ipo katika quran na kuna watu walibadilisha baadhi ya maana katika hivyo vya nyuma ndio maana Allah akataka quran iwe ndo kitabu chenye kufuatwa kwa umma huu wa mtume Muhammad rehema na amani iwe juu yake.
pia kuna kurasa alizofunuliwa nabii ibrahim na musa
sisi waislam tunaamini mitume ni wengi l kama anavyosema Allah "Na Rusuli Tuliokwishakusimulia kabla; na Rusuli (wengine) Hatukukusimulia.[An-Nisaa: 164] "
tuliofahamishwa ndani ya quran ni 25 tu na inatupasa kuamini hivo. ambao ni
1. Aadam
2. Idriys
3. Nuwh
4. Huwd
5. Swaalih
6. Ibraahiym
7. Luwtw
8. Ismaa'iyl bin Ibraahiym
9. Is-haaq bin Ibraahiym
10. Ya'quwb bin Is-haaq bin Ibraahiym
11. Yuwsuf bin Ya'quwb bin Is-haaq bin Ibraahiym
12. Shu'ayb
13. Ayyuwb
14. Dhul Kifl
15. Muwsaa
16. Haaruwn nduguye Muwsaa
17. Daawuwd
18. Sulaymaan bin Daawuwd
19. Ilyaas
20. Alyasaa'
21. Yuwnus
22. Zakariyyaa
23. Yahyaa bin Zakariyyaa
24. 'Iysaa bin Maryam
25. Muhammad
(Swalla Allaahu 'alayhim wa sallam)
na katika hao tuliofahamishwa waliopewa vitabu ni hawa na vitabu vyao
1. Torati ilifunuliwa kwa Nabii Musa (a.s.)
2. Zaburi ilifunuliwa kwa Nabii Daudi (a.s.)
3. 3. Injili ilifunuliwa kwa Nabii Isa (a.s.)
4. Qur'an ilifunuliwa kwa Mtukufu Mtume
Muhammad Rehma na amani iwe juu yake
6. Kitabu hiki yaani Qur'an haina kosa hata
moja, maneno na ahadi zake zote ni kweli
tupu.
Sisi tunaenda kwa vile tulivyofahamishwa na quran na sunna za nabii wetu na si zaidi ya hivyo wala hatudadisi yale ambayo si katika uwezo wetu wa kuyajua.
Na Allah anajua zaidi..
Allah akuongoze