Al-Barzakh: Haya ndio Maisha ya Kaburini baada ya kufa

Al-Barzakh: Haya ndio Maisha ya Kaburini baada ya kufa

Mwamba aliingizwa mkenge na mwanamke wa kiyahudi

Issue ya adhabu ya kaburi muhmmad alikuwa hajui kabisa, mwanamke wa kiyahudi alikuwa anamuhadithia aisha kwamba kuna adhabu na kuna test kwenye kaburi, muhhamad akakasirika sana kusikia hizo habari akasema waislamu hawatakuwa tested ni wayahudi ndio watakuwa tested.

Baada ya siku chache muhhammad akaja na stori kwamba ameletewa habari na jibril kwamba kutakuwa na test kwa waislamu pia , kuanzia hapo akawa kila akiomba anamuomba Allah amuepushe na adhabu ya kaburi

"Muhhammad came to me and there was a Jewish woman with me who was saying: 'You will be tested in your graves.' Muhhammad got upset and said: 'Rather the Jews will be tested."' 'Aishah said: "A few nights later, Muhhammad said: 'It has been revealed to me that you will be tested in your graves."' 'Aishah said; "Afterward I heard the Messenger of Allah seeking refuge with Allah from the torment of the grave. Sunan an-Nasa'i 2064
 
Faidika na Darsa la FaizaFoxy...

Unachanganya mambo sana usiyoyaelewa.

1) Kufa sio kuwa "Barzakh" kama unavyotaka kutuaminisha. Neno Kifo kwa lugha ya Kiarabu ni full stop. Kama unajua kidogo kusoma Kiarabu, hata vibao au saini zao za barabarani kwa Kiarabu zinaandikwa "Kif", kwa maana "stop". Kiswahili ndio tunakazia na kusema "Kifo".

2) Barzakh ni kizuizi "barrier", kwa maana wa uhai hayupo kwenye umauti na wa umauti hayupo kwenye uhai. Kati yetu ni hicho kizuizi (barzakh".

3) Umauti ni hali "state" nyingine ya kutokua hapa kwenye uhai, kuwepo kwenye umauti. Mfano tu, ni kama hali ya kuwa macho (conscious inatawala) na kuwa usingizini (subconscious inatawala). Tofauti ni kuwa upo hai hata ukilala.


Binafsi siamini katika adhabu za kaburi. Kwanza kwa kuwa hazijatajwa kwenye Qur'an, sijaziona. Pili Hadith iliyozitaja siikubali.

Ikiwa kuna adhabu ya kaburini basi Allah itakuwa "katudanganya" (AstaghafiruAllah) anaposema kwenye Qur'an kuwa kuna siku ya kiama (Kusimamishwa) kuhukumiwa? Sasa iweje tena tuhukumiwe kabla ya Kiama?

Naamini kuwa tunapotoka kwenye uhai kuingia kwenye umauti na hadi siku ya Kiama hakutakuwa na feeling za muda kama vile tupo hai. Itakua ni mano wa watu wa Pangoni, kisa cha kwenye Qur'an) au alielala miaka 100 kisa cha Qur'an).

Kifo, kinachokufa ni hiki kiwiliwili (body) chetu, nafsi haifi bali inaingia kweye umauti. Qur'an inahakikisha hili kwa kutukumbusha kuwa "kila nafsi itauonja umauti".

Hata sehemu tu ya kiwiliwili inaweza kufa na nafsi bado haijaingia kwenye umauti. Mfano ukikatika mkono au mguu, unakuwa umekufa huo mkono au mguu lakini nafsi bado haijaonja umauti.
Nikitoka hapa mojakwamoja mpaka kwenye darasa la bi Faiza foxy (our Jf Shekhat)
 
Nilisikiliza darsa la Barzakh na lilikiwa jambo geni sana kwangu. Never in my life niliwahi kujua kwamba kuna somewhere in between this world ambako ni Barzakh.

Nilifurahi sana. Why?

1. Tuna uwezo wa kuwaombea waliotangulia na Mwenyezi Mungu akawajaalia wepesi na Nur yake katika mapumziko yao. Your fate can be changed by dua.... so can that of our dear departed family, friends and loved ones.

2. Nilifurahi kujua kwamba wanaishi kwa kutembeleana hivyo wakati tunawaaga huku tunatakiwa tuwaage wavae nguo zao (sanda) na manukato mazuri kwa vile huwa wanapokeana na kutembeleana. Wanaulizwa vipi fulani na fulani umewaachaje? Na wao wanajibu kulingana na hali ilivyo.

3. Kila Ijumaa wanarudi kwenye makazi waliyokuwa wanaishi na kama ulitoa sadaqa kwa ajili ya kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu basi wanakuwaga na furaha sana. But kama tumejisahau wanakuwaga na masikitiko sana. Ilinifanya nikawa na bidii ya kutoa chocjote so that my relatives smile. I really miss my Babu, I really miss all of them. Mwenyezi Mungu atukutanishe na ndugu zetu na wapendwa wetu waliotangulia.

Kuna mengi ya kujifundisha and the story of Barzakh is a beautiful one.

Asante mtoa mada.
 
Ni kwamba hujanielewa ndugu yangu hiyo taurati injili zaburi vyote vilituma na waislam wa kabla ya mtume Muhammad baada ya hapo washirikina wakavibadilisha maana katika baadhi ya aya, Allah akamteremshia quran mtume Muhammad iwe ndo muongozo wa umma huu,, na nimekuambia pia tumefahamishwa hayo ndani ya quran na si zaidi ya hapo..ukitaka aya moja moja torati ipo na aya nyingi. Zaburi ipo na aya nyingi na injili ipo na aya nyingi na bibilia pia. Cwezi kuandika zote hapa nipe namba yako ya whatsapp nikufafanunulie moja baada ya jngne huenda Allah akakuongoza
Achana na hili Jahili utajisumbua buureee
 
Ikiwa kuna adhabu ya kaburini basi Allah itakuwa katudanya (AstaghafiruAllah) anaposema kwenye Qur'an kuwa kuna siku ya kiama (Kusimamishwa) kuhukumiwa? Sasa iweje tena tuhukumiwe kabla ya Kiama?


Mbona kuna watu Mungu amewaadhibu hapa hapa duniani na bado anaendelea kuwaadhibu na huko akhera watu hao watakutana na adhabu ya moto (hii ni kwa mujibu wa Qur'an), sasa huoni hapa Mungu anatoa hukumu hata kabla ya Qiyama??!-- sasa Mungu anashindwaje "kuzionjesha" adhabu katika Barzakh roho zilizokuwa ovu na "kuzionjesha" raha roho zilizokuwa njema??
 
Achana na hili Jahili utajisumbua buureee
Shidanashindwa kujibu , kasema vitabu vipo namuuliza surah moja moja at least 5 kakimbia , muwe mnajipanga sio kupiga story tu tukuache uende
 
Nilisikiliza darsa la Barzakh na lilikiwa jambo geni sana kwangu. Never in my life niliwahi kujua kwamba kuna somewhere in between this world ambako ni Barzakh.

Nilifurahi sana. Why?

1. Tuna uwezo wa kuwaombea waliotangulia na Mwenyezi Mungu akawajaalia wepesi na Nur yake katika mapumziko yao. Your fate can be changed by dua.... so can that of our dear departed family, friends and loved ones.

2. Nilifurahi kujua kwamba wanaishi kwa kutembeleana hivyo wakati tunawaaga huku tunatakiwa tuwaage wavae nguo zao (sanda) na manukato mazuri kwa vile huwa wanapokeana na kutembeleana. Wanaulizwa vipi fulani na fulani umewaachaje? Na wao wanajibu kulingana na hali ilivyo.

3. Kila Ijumaa wanarudi kwenye makazi waliyokuwa wanaishi na kama ulitoa sadaqa kwa ajili ya kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu basi wanakuwaga na furaha sana. But kama tumejisahau wanakuwaga na masikitiko sana. Ilinifanya nikawa na bidii ya kutoa chocjote so that my relatives smile. I really miss my Babu, I really miss all of them. Mwenyezi Mungu atukutanishe na ndugu zetu na wapendwa wetu waliotangulia.

Kuna mengi ya kujifundisha and the story of Barzakh is a beautiful one.

Asante mtoa mada.


Sijui hicho cha kuvaa nguo na kutembeleana kwa roho zilizomo Barzakh ni sahihi.

Kumbuka Barzakh ni kaburi ambamo roho iliyotengana na mwili huishi humo ikisubiri kufufuliwa kuingia akhera ili baadaye ikasimame katika hukumu (Qiyama), hivyo maisha ya roho katika Barzakh waweza fananisha na maisha ya mimba katika tumbo la mama, mimba inayosubiri kuzaliwa kuja duniani, katika Barzakh roho inasubiri ifufuliwe kuingia ulimwengu wa Akhera.
 
Swali zito sana tulitoka wapi? Sababu theory of evolution ukiisoma inajichanganya and it doesn't make any sense, hata theory ya cosmic inflation pia doesn't make any sense!!


Tulichipuka kutoka ardhini kipindi dunia hii ilipokuwa katika hatua ya "Biotic Soup"--- walianza wanyama, ndege na viumbe wengine hatimaye ndio watu wakachipuka na Mungu akaweka mfumo wa kuongezeka jinsi kwa kuzaliana na baadaye sana Mungu alipoona mtu anahitaji Muongozo wa kiroho na ustaarabu ndipo akaanza kutuma manabii wake na Nabii wa kwanza kutumwa duniani kwa watu wake alikuwa Adam, hivyo Adam ni nabii wa kwanza kutumwa duniani na Mungu na sio mtu wa kwanza kuumbwa kama jinsi inavyoaminiwa kimakosa na watu wengi.
 
Kufa ni nini? Kufa ni hali ya roho kuepukana na kiwiliwili, au kufa ni kukatika matumizi ya roho kwa kiwiliwili na kukosa kiwiliwili ambayo ndio ala yake na kumuepusha mtu na mali yake na watoto wake na mke wake.

Kufa kunakata utamu wa maisha ya kiulimwengu na kwenda ulimwengu mwingine. Mtu ambaye alikuwa akifurahia maisha ya ulimwengu kwa kufanya ufedhuli amepata khasara baada ya kufa.

Na yule ambaye alikuwa akifurahi kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu basi atapata neema kubwa na inakamilika kufaulu kwake.

Watu wengi hudhania ya kwamba mtu anapokufa na akazikwa amemaliza kila kitu na amepumzika na ulimwengu, wala halimjii yeye jambo lolote.

Kudhani hivyo ni kosa kubwa bali hakika mwanadamu baada ya kufa kwake anaingia katika maisha mapya, maisha ya barzakh na kutoka maisha ya barzakh huenda kwenye maisha ya akhera ambayo ndiyo maisha ya mwisho na ya milele.

View attachment 2140429

Bar-zakh ni maisha ya baadaye; maisha baada ya haya tuliyonayo hivi sasa hapa duniani.

Maisha hayo kuanzia mtu anapokufa huitwa ni ‘Maisha Ya Barzakh’.
Barzakh ni kipindi baina ya wakati wa mauti na Qiyaamah. Na kila maiti atapitia katika maisha hayo, awe Muislam au Mkristo au asiye na dini, awe mwema au mwovu, na katika kipindi hicho kunakuwa na fitna na mitihani ya kaburi ambako mtu anajiwa na Malaika wawili na kuhojiwa na kisha hufuatia neema au adhabu za kaburini.

Inajulikana kuwa kuna makazi matatu; makazi ya Dunia (Daarud-duniya), makazi ya Barzakh (Daarul-Barzakh) na makazi ya kudumu (Daarul-Qaraar).

Maisha ya kaburini ni kile kipindi anachokaa mtu baada ya kufa kwake mpaka kufufuliwa kwake. Kipindi kati ya parapanda la kwanza ambalo ni amri ya kufa viumbe vyote na parapanda la pili ambalo ni amri ya kufufuliwa viumbe vyote vitakavyotakiwa vifufuke, Huitwa Barzakh.

Katika kipindi hichi cha maisha ya dunia ni mambo gani yanayoendelea katika nafsi ya mwenye kufa? Wengi kwa kujiliwaza katika wakati huo hufikiria kuwa watu wakifa wanakuwa mapumzikoni.

Na watu ambao hawaamini siku ya mwisho huamini kuwa kifo ndio mwisho wa maisha ya watu na iliyobaki ni kuoza na kuwa chumvi chumvi zitakazotumika ardhini.

Katika kipindi cha Barzakh roho za watu wema zitakaa pahali pazuri kungojea malipo yao ya Peponi, Ama zile za watu waovu zitakuwa mahabusu zikingojea siku ya hukumu yao. Ama kuhusu mtu muovu yeye atakaa katika kaburi lake kwa khofu na fadhaa.


Maisha ya Barzakh ni maisha yanayotofautiana kabisa na maisha ya dunia, na hakuna ajuaye hakika kamili ya maisha haya na namna yalivyo isipokuwa Mwenyezi MUNGU pekee.

Jiandae na maisha ya barzakh ambayo hayana salama ila kwa wacha-Mungu

View attachment 2140430
Nani alienda akarudi na hizo hadithi
 
Ikiwa mwili utaoza ni kipi Kinachomfanya Firauni aliyejiita MUNGU asioze hadi leo karne na karne?
Kwa iyo kwaakili yako unahisi firauni hafanyiwi chochote kuzuiwa kuoza


Aahaaah aah dah akili zetu sisi aiseee, ulaya pia kuna watu hawaozi wamewekwa kusubiria improvmnt ya kisayans ili wafufuliwe teena baadae... Je na wao ni mafirahun??
 
Sijui hicho cha kuvaa nguo na kutembeleana kwa roho zilizomo Barzakh ni sahihi.

Kumbuka Barzakh ni kaburi ambamo roho iliyotengana na mwili huishi humo ikisubiri kufufuliwa kuingia akhera ili baadaye ikasimame katika hukumu (Qiyama), hivyo maisha ya roho katika Barzakh waweza fananisha na maisha ya mimba katika tumbo la mama, mimba inayosubiri kuzaliwa kuja duniani, katika Barzakh roho inasubiri ifufuliwe kuingia ulimwengu wa Akhera.
Huenda sikujieleza ndivyo. Ila ni kwamba katika maandalizi ya safari ya mwisho, tunatakiwa tuwaaandae vizuri na manukato pia sababu huwa wanatembeleana.
 
quran ina miaka 1500,biblia ina miaka 2000 shinto ina miaka 5000 punguza mihemko ongea reality,acha kukremisha uliyomezeshwa madrasa na ustazi
Ndo unavyojidanganya hivo kama quran ina miaka 1500 na ukaidanganya nafsi yako pia..Hiyo quran inayoizungumzia ni maneno ya Allah na na nimuongozo ambao ameupangalia billions of years kabla ata wewe mwanadamu hujafikiriwa kuumbwa sio hio miaka 1500 unayosema ..hyo miaka elfu na miatano unayosema ndo ilipokamilika kuteremshwa tu..isome dini upate kuelewa,,
Allah akuongoze
 
Back
Top Bottom