Iran ilitumia pesa nyingi sana kwenye masuala ya vita, kwa gharam kubwa ya kuwafanya wananchi wake kuishi kwenye umaskini mkubwa. Iran iliamini kuwa imejilinda sana kivita. Kitendo cha Israel kuipiga kama vile haina chochote, kuwaua makamanda wakuu wote, wanasayansi, kiasi cha kumfanya Ayatollah kukimbilia mashimoni kuokoa maisha yake, kumeifanya Iran ione imepoteza muda na pesa nyingi kwa kitu ambacho hakijawasaidia chochote.
Iran ilipeleka pesa nyingi sana kwa makundi ya kigaidi, na kuyapatia mafumzo mengi, ikiamini makundi hayo yataifanya Iran kuwa super power mashariki ya kati nzima. Halafu Israel ikayapiga kama vikundi vya sungusungu, imeivunja nguvu sana Iran. Kwa sasa inabidi ijitafakari sana kama, kama iendelee kupoteza pesa kwenye miradi yake kichaa au itumie pesa yake kuwaletea maendeleo Wairan