Nimemsoma Magufuli akizungumzia ujio wa Corona mpya nchini kwanz amekiri ipo akidai imeletwa na watu walioenda kutafuta chanjo nje, hapa naamini lile tamko lake la kusema Corona hakuna Tanzania ndio kalifuta rasmi.
Lakini pia amekazania watanzania wasitumie kinga kwasababu wazungu hawatupendi, hiyo kinga anadai inaweza kusababisha tusizaliane kwa mtazamo wake anadai wazungu hawapendi tuzae.
No research, no right to speak; huyu mtu aliemtumbua yule mtoto wa Malecela NIMR kwasababu alitimiza majukumu ya kazi yake kwa kutoa taarifa ya kitaalamu nitamwamini vipi kwenye hii sababu yake ya wazungu hawatupendi? sio yeye ndio hapendi matokeo ya kazi za kitaalamu?
He is not a doctor or a pharmacist, but kwanini hupenda kuingilia taaluma za watu kwa kutoa majibu mepesi kwenye maswali ya msingi? hapa nikisema yeye ndio hawapendi wazungu ndio maana huwasingizia vitu asivyo na uthibitisho navyo nitakuwa nakosea?
Nikiri hapa, mtazamo wa Rais wetu kwenye hili jambo ni wa kushangaza na kusikitisha, sasa kama Rais hataki watu wake wajikinge kwa chanjo ambayo naamini ametumia hisia kusema hiyo chanjo sio salama kwa raia, na kusisitiza watu wajifukize.
Sasa huku kujifukiza kulithibitishwa na maabara ipi hapa kwetu wakati maabara ile ya mwanzo iliyopima mapapai walidai ilikuwa mbovu? na mtaalamu wake akatumbuliwa?