Al Shabaab katika mafunzo na mahafali yao huko Somalia

Usinifanye nipigwe ban bure acha kudaganya watu. Nchi ambayo ina waislamu lkn imegoma kufuata itikadi za kishetani kama hao Alshaabu mojawapo ni Saudi Arabia japo bado inajitahidi kutoka katika sheria za zama za giza. Hakuna Muislamu anayeheshimu na kukubali dini ya mtu mwingine isipokuwa ya kwao. Takutajia hata viongozi wa Tanzania waislamu walioheshimu dini zingine ambao ni Karume (mtoto wa raisi wa kwanza Zanzibar). Nakumbuka siku moja Machui kanisani alialikwa. Alitoa wosia wa namna ya kuishi kwa upendo na amani huku tukiheshimu dini zote.
 
Naona baada ya kupewa kisango huko kwenye mashimo ya Amboni Tanga mmekuja kwa style nyingine. Jipambanue tu na uwashauri wawekeze kwenye elimu sio mafundisho ya ovyo. Mtu unaenda kusali msikitini na bastola ikiwa full magazine huo ndo uislamu unaoupigania!! Ujinga
 
Kuwakamata wasichana wa shule na kuwaingiza kambini na kuanza kuwalawiti, kuwabaka na kuwajaza mimba, huku ukiwalazimisha wapokee mapepo kwa lazima,... Hii ndio maadili na Imani iliyotukuka?... Pambaaafffff,... Hii sio dini kabisa, ni uhuni na ushetani..
 
Uislam haujawahi kukubali uonevu.
Shida inayoletwa na wanadamu.Kila Imani inatafuta usimamizi,tulitakiwa sote tuwe huru kueneza na kufuata pale inapokubalika.Vita huja pale inapoonekana jamii moja inaizuia nyingi kuishi kwa utashi wa imani yao.
 
Hili ndilo nililomaliza kusema
Huwezi sema uhuni wa kaka au dada yako ndio kosa la familia yenu
 
Acha kujificha kwenye ukiristu mjing.a wewe. Sri lanka wamevamia wapi kundi la ISIL hadi wawauwe vile? Kwa nini wasivamie kambi za jeshi kulipiza kisasi? Wadaganye hao wasioenda shule
@Ng'wanapagi, Sijakuelewa nini shida yako hadi umepaniki namna hii wakati unajinasibu kuwa ni mwenye akili nyingi.
Mimi sijawazungumzia watu wa Sri lanka au unaowaita ISIL.
Wala sijasema habari ya kuvamia mahali flani.
Hebu tulia na ueleze jambo linaloeleweka.

Ulitaka kusema nini kuhusu hapo uliponinukuu ?
 
Mbona Nchi ya Irani imepiga marufuku Dini nyingine zote isipokuwa Dini ya Kiislamu pekee ndiyo inaruhusiwa.
Nilichokusudia kusema ni kuwa hao Al-Shabaab wanafaa wakae nchi kama ya Iran.
Ambayo ni nchi ya Kiislamu. Na nikasema hawawezi kukaa nchi yenye dini nyingine.
Sasa wewe hujaelewa nini
hapo.
 
Ha...ha...ha.
Nimekueleza kwa mujibu wa mtazamo wa Al-Shaabab, na sio wewe au Waislamu wa Tanzania.

Majibu yako yamenifulahisha haswa.
Umeingiza kamuhemuko Kidogo sana.
Kuwa huru kama mimi.
 
Basi mkuu fanya kauchunguzi kwanini waislamu hujiona wako sahihi au huona dini yao ni sahihi kuliko zengine? mfano muislamu anaweza akawa kazidiwa kiwango cha imani na mkristo ila bado muislamu huyo jinsi anavyoiona dini yake ni sahihi ikawa zaidi ya huyu mkristo anavyoiona dini yake.

Hata ukiangalia mabishano yale ya kidini mfano kati ya ukristo na uislamu utaona sehemu kubwa ya mashambulizi ya wakristo kwenye uislamu ni katika yale mambo ya nje yenye kuuchafua uislamu kama vile ugaidi,uchawi na kufuga majini na mfano wa hayo. Ila mashambulizi makubwa ya waislamu kwenye ukristo ni katika mambo ya ndani ya ukristo kama usahihi wa biblia na msingi wa imani ya ukristo. Ukiona muislamu anataja mambo ya ushoga sijui kulawiti watoto na mfano wa hayo basi ni makusudi tu kumkela mkristo.
 
Mimi kama mimi najiona niko sahihi Katika imani yangu ya Kikristo na kamwe haitotokea nikaikubali imani nyingine yoyote ile bila kuziona faida zake kwangu.
Na msingi wa imani yangu ni Upendo, uliofundishwa na Kiongozi wangu Yesu Kristo wa Nazareti.
Kwamba nihakikishe kwa dhati kabisa.
1. Nampenda Mungu.
2. Nampenda jirani yangu, yaani binadamu yoyote ninayekutana naye.
3. Pia amenihakikishia kwenda kuishi Naye Mbinguni baada ya kifo changu.
Yeye ndiye atakaye nifufufua siku ya Kiyama na kunipeleka huko Mbinguni.

Haya maelezo nimeridhika nayo Kabisa na yamenifanya nikubali kuwa Mkristo.

Sasa kama kuna imani nyingine inataka niiamini, lazima nijue inasemaje kuhusu maisha yangu ya sasa na ya baadae.

Kama ina ahadi nzuri zaidi kuzipita hizi alizoniahidi Bwana Yesu Kristo, basi naweza nikabadili dini nitakapo zisikia.

Ila mpaka sasa hivi Sijaambiwa hizo ahadi nyingine za kuniridhisha ndio maana bado ni Mkristo.

Watu wanao lawiti, wanao fanya uovu mwingine mimi hawanihusu ni mambo yao.
Mimi nimeambiwa niyatende matendo yanayo mpendeza Mungu na pia Jirani yangu.

Sifahamu chochote kuhusu imani nyingine.
Hata Uislamu sielewi unaeleza nini kuhusu mimi.
 
Umeeleza ukweli kabisa na ulichoeleza si wewe tu bali wakriso wote ndio wako hivyo kwamba wanaangalia yale yanayo wapendeza na ndiyo kipimo cha usahihi wa dini yao(ndiyo sababu kubwa wao kushikamana na ukristo) na si kuangalia ukweli ni upi ukweli hata kama haukupendezi,hivyo kwao si muhimu hizo ahadi nzuri zimetoka kwenye msingi wa ukweli au si kweli bali muhimu ni ahadi nzuri na mambo yenye kuwapendeza na kuwaridhisha.
 
Kama hataielewa hii hoja yako basi, he will never understand!
 
UKWELI unao uongelea ni dhana mtambuka.
Ukweli wa mtu mmoja unaweza kuwa Uwongo kwa mtu mwingine pia.
Kwa mfano.
Dawa ya Mseto inaweza kumtibu mtu fulani ugonjwa wa Malaria na ikashindwa kumtibu mtu mwingine mwenye ugonjwa huohuo wa Malaria.
Au dawa hiyo hiyo ikamtibu mgonjwa fulani kwa kipindi fulani lakini baada ya muda fulani ikashindwa kumtibu tena ugonjwa uleule.
Huu ni utafiti wa Kisayansi.

Hivyo ndugu, ukweli wako sio lazima uwe ukweli wa mtu mwingine.
Na hata hao Al-Shabaab wanajiona wanafuata Ukweli wa maisha unavyotakiwa uwe.
Na ndio maana wanalazimisha na wengine wawe kama wao, na wafanye kama wao.

Yesu Kristo ni Binadamu pekee aliye weza kusimama hadharani na kusema kuwa yeye hana Dhambi na hakuna anayembishia kwa kipindi chote.

Na akasema pia Yeye ndiye NURU ya Ulimwengu, na ni NJIA, KWELI na UZIMA na hadi leo hakuna anayepinga.

Fulamu zinazotungwa kuonesha Matendo ya Yesu zote zinathibitisha maneno haya hadi hii leo.

KWELI nyingi zilizoonekana hapo awali zimefikia mahali zimeshindwa kujithitisha kuendelea ubora wake na zimekufa.

Leo dawa ya Chloroquine, haitibu tena Maralia.
Watu wengine maarufu wa zamani wanazuiwa kuoneshwa matendo yao hadharani kwa kuogopa fedheha.

Yesu Kristo ndio kabaki binadamu pekee ambaye ni Mfano wa binadamu wa kuigwa na wengine.
Na nakuambia ndiye, binadamu pekee wa kumsikiliza na kumwamini.
Kwakuwa ukimtazama usoni unasema hakika wewe ndiwe NURU, NJIA KWELI na UZIMA na chochote unachokisema ni sahihi.

Hapo Ndipo Lilipo Chimbuko na Nguzo ya Ukristo na Wakristo.

"Wameshika Chenye Nguvu"

Panahitajika Hekima Kubwa Kuelewa Hayo Maelezo na Mifano Niliyotoa Hapa.
 
Watu wa Mnyaazi Mungu ktk ubora wenu
 
Nakumbuka Dr.Slaa aliwahi kusema kwamba ukweli hauna upande,na ni sahihi mkuu hauwezi kusema kwa fulani huu ni ukweli ila kwa mwengine sio ukweli,hiyo sio sifa ya ukweli hata dawa kufanya kazi mtu na kushindwa kufanya kazi kwa mwengine haifanyi kuwa sio dawa itabaki kuwa ni dawa tu huo ndio ukweli.
Mkuu imani inatakiwa iwe na mizizi au nguzo yenye kushikilia hiyo imani bila hivyo hiyo imani itakuwa yenye kuyumba yumba ama inaelea,na hapo hisia itachukua nafasi kubwa. Na hisia inapochukua nafasi ndipo yanapowezekana kutokea mambo ya kulishwa vitu vya ajabu ajabu(mf."jik" majani n.k) na kufanyiwa vitu vya ajabu huko makanisani,haya yote ni kwa sababu wametanguliza hisia mbele na ndiyo matokeo ya imani iliyokosa kitu cha kushikilia inaelea tu.

Najua unaweza kueleza mengi mazuri yenye kuvutia kuhusu Yesu au ukristo lakini tatizo hayo mambo (imani) yameshikiliwa na nini chenye kukufanya kuwa na hakika na hayo unayoamini?
 
Unajua Wenzetu Waislamu mna faida moja kubwa.
Nyumba yenu ya Ibada inajulikana kwa jina moja la
Msikiti.
Mtu akisikia Msikiti basi ni moja kwa moja anaelewa kuwa ni Nyumba ya kufanyia ibada kwa Waislamu.
Tofauti na nyumba inayoitwa Kanisa.
Kuna
Free Masonic Church
Lusiferian Church
Church of Satan
Church or Mormon
The Rastafarian Church
NK
Sasa mtu wa kawaida unaona Mashoga wanafunga ndoa kwenye jengo linaloitwa kanisa, mara moja unaanza kudhani Wakristo wanaozesha Mashoga bila kufahamu kuwa hilo ni kanisa la nani.
Hao wanao lishana nyoka kanisani au kulishana majani au dawa ya Jiki.
Watu wasio wakristo wanaamini tu kwakuwa tendo linafanyika Kanisani basi hao waliondani ni Wakristo.
Kumbe sio.
Kanisa la Rastafarian ibada yao ni pamoja na kuvuta bhange, lakini nje limeandikwa neno Kanisa.
Mtu akipita nje atasema Wakristo wanavuta bhange Kanisani.

Ninachotaka kusema ni kuwa Kanisa la Wakristo ibada yake imeelezwa katika Injiri ya Yesu Kristo.
Ukiona ibada inaendeshwa tofauti na Agano Jipya linavyosema basi ujue hilo sio kanisa la Kristo.
Hata ukiona kanisa Lina Sujudia Sanamu ujue hilo sio Kanisa la Kikristo.
Kuna Makanisa mengi sana lakini Makanisa ya Kikristo ni machache mno.
Makanisa ya Kikristo Yanafuata kile tu Yesu Kristo alifundisha.

Hivyo ukisiakia Kanisa la Kilindini usiweke imani yako hapo, angalia wanafanya nini humo Kilindini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…