Alaghahiwa na Wi-Fi ya uongo ya uwanja wa ndege, apoteza fedha na kukosa ndege

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Mtu mmoja alikwama kwenye uwanja wa ndegekatika jiji fulani, akisubiri ndege ya kuunganisha safari.

Kama ilivyo kwa wengi wetu, alitafuta WiFi ya bure ili kupotezamuda. Akaona WiFi inayoitwa “Free Airport WiFi” na akajiungabila kufikiria mara mbili.

Ndani ya dakika chache baada ya kujiunga, simu yakeilianza kuonesha hali isiyo ya kawaida;

1. Kadi yake ya benki ilitoa taarifa kuwa kuna mtu alikuwaakinunua bidhaa Singapore.

2. Kuna Mtu alikuwa akinunua mikoba ya bei ghali katikaduka la kifahari.

3. PayPal yake ilimtumia misimbo (codes) za uthibitisho bilakukoma.

Cha ajabu ni kwamba simu yake ilikuwa mkononi mwake mudawote, na Wallet yake ilikuwa mfukoni.

Hakuwa amenunua chochote wala kumpa mtu yeyote taarifa za kadi yake ya benki.

Utapeli huo ulikuwa mkubwa kuliko yeye pekee.

Alidhani ni hitilafu ya mfumo tu.

Mfanyakazi mmoja wa uwanja wa ndege akaangalia simu yakena kumwambia: ‘Hiyo si Wi-Fi halisi ya uwanja wa ndege. Ni feki, imeundwa mahsusi kuwadanganya Watalii.”

Ilibainika kuwa, hakuwa mhanga pekee siku hiyo.

Wasafiri wengine pia walitapeliwa katika Uwanjahuo, ambapo;

1. Watu walitumia kadi zao za benki kununua vitu ambavyohawakuwahi kuviagiza.

2. Picha za Hati ya Kusafiria za mtu mmoja ziliibwa kutokakwenye simu yake.

3. Nyaraka za VISA za mtu mmoja zilitumwa kwenye anwaniya barua pepe ya mtu asiyemjua.

Yote haya yalitokea kwa sababu tu walijiunga kwenye WiFi yaUongo.

Namna Utapeli huu Unavyofanya Kazi

Maelezo kwa ufupi:

Matapeli huanzisha WiFi ya Uongo inayofanana na halisi.

Huiita majina kama “Free Airport WiFi” au “Airport Guest” majina yanayoakisi uhalisia.

Unapojiunga na WiFi hiyo, matapeli wanaweza kuona kila kituunachofanya kwenye kifaa chako:

1. Nywila zako unapojaribu kuingia kwenye program

2. Taarifa zako za kibenki

3. Picha na nyaraka ulizonazo kwenye kifaa chako

4. Kila unachokiandika

Kuwa Salama: Kanuni Rahisi.

1. Kabla ya kujiunga na WiFi yoyote, uliza Wafanyakazihusika jina halisi la WiFi

2. Ikiwa inaonekana nzuri kupita kiasi (kama bure kabisa bilanywila), kuwa na shaka.

3. Ukiwa na mashaka, tumia tu Intaneti ya simu yako.

Ikiwa ni lazima utumie WiFi ya umma

1. Usijaribu kuingia kwenye akaunti yako ya benki au kununua kitu chochote mtandaoni.

2. Usifungue barua pepe au nyaraka muhimu.

3. Kimsingi, itumie tu kwa kutafuta taarifa za kawaidamtandaoni.

WiFi ya bure siyo kila mara ni bure. Wakati mwingine inaweza kukugharimu zaidi kuliko hata kulipia.

Usikubali intaneti ya bure ukakupelekea kupoteza maradufu.
 
Wadukuzi wa hivyo wakija Bongo watawapiga sana watu. Maana Mbongo utamwambia nini kwa 'waifii' ya bure.
Watawapiga nini na hawana hiyo mifumo ya kipesa kielectkroniki?

Labda wachukue namba za ndgu, jamaa na marafiki na kuwatumia "ile pesa tuma kwa namba hii"

Kuna wale hudukua accounts kwenye mitandao ya kijamii, zaidi ya kutapeli ndgu na jamaa wa muhanga huwa haimuathiri muhanga kwasababu wengi hawana hizo simbanking.
 
sawa
 
Mtu mmoja alikwama kwenye uwanja wa ndegekatika jiji fulani, akisubiri ndege ya kuunganisha safari.

Huko ulipoitoa hii habari,walikua wameandika hivyo Jiji fulani au ni wewe ndio umeandika hivyo?
Kwanini hili jiji lifichwe? Au hii ni Chai ya tangawizi?

Japo najua kua ni kweli WI-FI inaweza kumpa hacker access ya kuingilia mifumo yako
 
Mtu mmoja alikwama kwenye uwanja wa ndegekatika jiji fulani, akisubiri ndege ya kuunganisha safari.

Kama ilivyo kwa wengi wetu, alitafuta WiFi ya bure ili kupotezamuda. Akaona WiFi inayoitwa “Free Airport WiFi” na akajiungabila kufikiria mara mbili.

Ndani ya dakika chache baada ya kujiunga, simu yakeilianza kuonesha hali isiyo ya kawaida;

1. Kadi yake ya benki ilitoa taarifa kuwa kuna mtu alikuwaakinunua bidhaa Singapore.

2. Kuna Mtu alikuwa akinunua mikoba ya bei ghali katikaduka la kifahari.

3. PayPal yake ilimtumia misimbo (codes) za uthibitisho bilakukoma.

Cha ajabu ni kwamba simu yake ilikuwa mkononi mwake mudawote, na Wallet yake ilikuwa mfukoni.

Hakuwa amenunua chochote wala kumpa mtu yeyote taarifa za kadi yake ya benki.

Utapeli huo ulikuwa mkubwa kuliko yeye pekee.

Alidhani ni hitilafu ya mfumo tu.

Mfanyakazi mmoja wa uwanja wa ndege akaangalia simu yakena kumwambia: ‘Hiyo si Wi-Fi halisi ya uwanja wa ndege. Ni feki, imeundwa mahsusi kuwadanganya Watalii.”

Ilibainika kuwa, hakuwa mhanga pekee siku hiyo.

Wasafiri wengine pia walitapeliwa katika Uwanjahuo, ambapo;

1. Watu walitumia kadi zao za benki kununua vitu ambavyohawakuwahi kuviagiza.

2. Picha za Hati ya Kusafiria za mtu mmoja ziliibwa kutokakwenye simu yake.

3. Nyaraka za VISA za mtu mmoja zilitumwa kwenye anwaniya barua pepe ya mtu asiyemjua.

Yote haya yalitokea kwa sababu tu walijiunga kwenye WiFi yaUongo.

Namna Utapeli huu Unavyofanya Kazi

Maelezo kwa ufupi:

Matapeli huanzisha WiFi ya Uongo inayofanana na halisi.

Huiita majina kama “Free Airport WiFi” au “Airport Guest” majina yanayoakisi uhalisia.

Unapojiunga na WiFi hiyo, matapeli wanaweza kuona kila kituunachofanya kwenye kifaa chako:

1. Nywila zako unapojaribu kuingia kwenye program

2. Taarifa zako za kibenki

3. Picha na nyaraka ulizonazo kwenye kifaa chako

4. Kila unachokiandika

Kuwa Salama: Kanuni Rahisi.

1. Kabla ya kujiunga na WiFi yoyote, uliza Wafanyakazihusika jina halisi la WiFi

2. Ikiwa inaonekana nzuri kupita kiasi (kama bure kabisa bilanywila), kuwa na shaka.

3. Ukiwa na mashaka, tumia tu Intaneti ya simu yako.

Ikiwa ni lazima utumie WiFi ya umma

1. Usijaribu kuingia kwenye akaunti yako ya benki au kununua kitu chochote mtandaoni.

2. Usifungue barua pepe au nyaraka muhimu.

3. Kimsingi, itumie tu kwa kutafuta taarifa za kawaidamtandaoni.

WiFi ya bure siyo kila mara ni bure. Wakati mwingine inaweza kukugharimu zaidi kuliko hata kulipia.

Usikubali intaneti ya bure ukakupelekea kupoteza maradufu.
UMetoa elimu nzuri. Ubarikiwe sana
 
Back
Top Bottom