Alama/ logo ya Nyoka katika fimbo kwenye mambo ya afya ina maana gani?

Alama/ logo ya Nyoka katika fimbo kwenye mambo ya afya ina maana gani?

Hii alama inamaana gani?
1449298444809.jpg
 
Waisraeli walipokuwa wanakufa jangwani Mungu alimwamuru Musa aweke sanamu ya nyoka na yeyote aliyeiangalia alipona. Japo sijafanikiwa kuiweka vizuri, maana halisi ya hiyo nyoka ni hiyo. Ipo kwa bibilia. Ngoja wenyewe waje waniwekee fresh
 
ngoja nikae karibu maana mi mwenyewe sielewi
 
Habari za jumapili wadau,

Napenda kuuliza kujua uhusiano uliopo kati ya Nyoka na taasisi ya Afya kwani naona LOGO za baadhi ya taasisi zikiwa imechorwa Nyoka.

Mfano mzuri ni Muhimbili Hospital... Karibuni sana wadau kwa Masada.
 
Kuna hospital pale magomeni morroco nilipita nikaona hiyo alama nikashangaa sana
 
Habari za jumapili wadau,

Napenda kuuliza kujua uhusiano uliopo kati ya Nyoka na taasisi ya Afya kwani naona LOGO za baadhi ya taasisi zikiwa imechorwa Nyoka.

Mfano mzuri ni Muhimbili Hospital... Karibuni sana wadau kwa Masada.
Mkuu jibu lake utalipata kutoka katika kitabu cha Hesabu 21:4-9
BWANA akatuma nyoka za moto kati ya watu wakawauma watu wengi wakafa watu wakamwendea musa wakasema tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung'unikia Mungu na wewe utuombee kwa BWANA atuondolee nyoka hawa basi Musa akawaombea watu BWANA akamwambia musa jifanyie nyoka ya shaba ukaiweke juu ya mti na itakua kila mtu aliye umwa aitazamapo ataishi.

Musa akafanya nyoka ya shaba akaiweka juu ya mti hata ikiwa nyoka amemwuma mtu alipoitazama ile nyoka ya shaba akaishi...


Kwa hio kuwepo kwa logo ya nyoka kwenye tasisi za afya ni kuhusianisha mambo ya utabibu yaliotukuka na matibabu yaliyopo katika tasisi hizo..
 
Yule wa Muhimbili sio nyoka, ni aina fulani ya mnyoo, ambae akikomaa mwilini hutembea ndani ya ngozi hadi miguuni, huondolewa kwa kumzingusha kwenye kijiti chenye panda, kama kinavyoonekana kwenye ile nembo ya Muhimbilli.

Yule anaonekana kama nyoka kwenye nembo ya hospiittal ya Muhimbili ni mnyoo, na kile kijiti, ndicho aina ya kijiti kinachotumika kumtolea mwilini, hii ni kwa Mujibu wa mtaalamu wa muhimbili, aliefanya kipindindi na radio hata hivyo shirika la afya la Duniani WHO, nao hutumia alama hiyo ya kijiti na mnyoo, na ndiyo waasisi.
 
Yule wa Muhimbili sio nyoka, ni aiina fulani ya mnyoo, ambae akikomaa hukutembea ndani ya ngozi hadi miguuni, huondolewa kwa kumzingusha kwenye kijiti chenye panda. Yule anaonekana kama nyoka kwenye nembo ya hospiittal ya Muhimbili ni mnyoo, na kile kijiti, ndicho aina ya kijiti kinachotumika kumtolea mwilini, hii ni kwa Mujibu wa mtaalamu wa muhimbili, aliefanya kipindindi na radio hata hivyo shirika la afya la umoja mataifa na hutumia alama hiyo ya kijiti na mnyoo.
Hiyo ni scenario moja...
 
Back
Top Bottom