Kwanza kabisa inakubidi utambuwa Mwenyezi Mungu ndio muumba wa viumbe vyote, pia ameumba ardhi na mbingu pamoja na vilivyomo,
Quote from the Holy Qur'an: Taa-Haa (20:6)
Ni vyake vyote viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, na viliomo baina yao, na viliomo chini ya ardhi.
Pili tuje kwenye majini sasa,
Hawa ni viumbe miongoni mwa viumbe alivyoumba mwenyezi Mungu( Hawajajiumba wenyewe wala hawajatokea tu by chance au kuumbwa na shetani hapa sifa na uwezo wa uumbaji ni wa mwenyezi mungu pekee, hapa ndo maana Yesu anakosa sifa za kuwa mungu kwakuwa ameumbwa na hajawai na hawezi kuumba hata inzi au jani la mti)
Baada ya kujua kuwa ni viumbe, pia katika majini wapo wanaofata amri za mungu na kuwa watiifu na pia wapo walio hasi kwenda kinyume na maamrisho ya muumba wao kundi hili sasa ndilo wanaitwa mashetani ambao wamelaaniwa yaani wapo mbali na rehema za Allah na kiongozi wao ni Ibilisi.
Miongoni mwa sifa za majini ni kuwa hawana umbo rasmi au kwa lugha nyingine wanawza kujibadilisha kuwa na umbo lolote, pia hawaonekani kwa haya macho yetu(sisi hatuwaoni ila wao wanatuona)
Pia idadi yao ni kubwa sana wametapakaa sehemu kubwa ni vile hatuwaoni tu
Mashetani wanatumika na waganga na waiga ramli ktk mambo yao ya uchawi na uasi.
Sasa sijajua shida inatoka wapi ktk hiyo hadith au haujaielewa unahitaj ufafanuzi??
Na Allah anajua zaidi