hamis77
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 18,678
- 27,653
Alexander III wa Makedonia maarufu kama Alexander Mkuu alizaliwa mwaka 356 K.K. mjini Pella. Alipokea mafunzo ya kijeshi na kielimu chini ya uangalizi wa baba yake, Mfalme Philip II, na pia mwanafalsafa maarufu Aristotle.
Baada ya kifo cha baba yake, Alexander alirithi kiti cha enzi akiwa na umri wa miaka 20 tu kijana mdogo na mbichi kabisa .
Katika kipindi kifupi, aliteka na kushinda maeneo makubwa kutoka Ugiriki, Uajemi, Misri, Asia ya Kati hadi mpaka wa India.
Uhodari wake wa kijeshi, maono ya kiutawala, na mbinu bunifu za kivita na mashambulizi ya haraka vilimfanya awe miongoni mwa majina makubwa zaidi katika historia ya wanajeshi., fikiria kijana wa miaka 20 tu anafanya haya.
Biblia inamrejelea Alexander katika ishara za kinabii ndani ya kitabu cha Danieli sura ya 8. Maono haya yanafafanua wazi falme zinazohusika
Daniel 8👇👇👇👇
20: Yule kondoo mume uliyemwona, mwenye pembe mbili, hizo ndizo wafalme wa Umedi na Uajemi.
21 :Na yule beberu, mwenye manyoya mengi, ni mfalme wa Uyunani; na ile pembe kubwa iliyo kati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.
22 :Tena katika habari ya pembe ile iliyovunjika, ambayo badala yake zilisimama pembe nne, falme nne zitasimama kutoka katika taifa lile, lakini si kwa nguvu kama zake.
Ngoja tufafanue
Kondoo mume anawakilisha Dola ya Umedi na Uajemi;
beberu anawakilisha Uyunani;
Pembe kubwa ni mfalme wa kwanza wa Uyunani Alexander.
Baada ya pembe kuvunjika (kifo cha Alexander), pembe nne zilichukua nafasi yake ikimaanisha falme nne zilizogawanyika baada ya kifo chake.
Alexander aliongoza jeshi dogo lakini lililopangiliwa kwa ustadi, likiwa na nidhamu ya hali ya juu na kasi ya kushangaza. Alimshinda Mfalme Dario III wa Uajemi katika vita vya Issus na Gaugamela, akavunja nguvu za Dola ya Uajemi na kuanzisha himaya kubwa.
Sera zake zilijumuisha kuheshimu tamaduni za wenyeji, kuanzisha miji mipya, na kueneza lugha ya Kigiriki cha Koine kama lugha kuu ya biashara, elimu, na utawala. Hapo ndipo ulipoanza mchakato unaoitwa Hellenismo.
Hellenismo ni kipindi cha historia na mchakato wa kitamaduni ulioanza baada ya ushindi wa Alexander, ambapo lugha, falsafa, elimu, sanaa, na desturi za Kigiriki ziliunganishwa na tamaduni za Mashariki ya Kati, Afrika Kaskazini, na Asia.
Ni kupitia Hellenismo ndipo Kigiriki cha Koine kikawa lugha ya kimataifa, kikatumika katika maandiko ya kifalsafa, kisayansi, na hata katika Agano Jipya la Biblia.
Kama ilivyotabiriwa na Nabii Daniel ,Alexander alipofariki mwaka 323 K.K. akiwa na umri wa miaka 32 tu, hakuwa na mrithi mwenye nguvu sawa na yeye.
Ufalme wake uligawanywa kati ya majenerali wake wanne:
Seleuko — alitawala sehemu kubwa ya Asia (Dola ya Seleukia).
Ptolemai — alitawala Misri na kuanzisha nasaba ya Ptolemaioi.
Lisimaki — alitawala Asia Ndogo na Thrace.
Kasanda — alitawala Masedonia na Ugiriki.
Hali hii inalingana moja kwa moja na maneno ya Danieli:
“falme nne zitasimama… lakini si kwa nguvu kama zake.”
Hakuna hata moja ya falme hizo iliyoifikia nguvu ya utawala wa Alexander.
Mwanahistoria Myahudi, Flavius Josephus, anasimulia kuwa Alexander alipotembelea Yerusalemu, Kuhani Mkuu alimwonyesha maandiko ya Danieli yanayomtabiri.
Alexander alipoyasoma, alikiri kuwa unabii huo unamhusu yeye, na kwa heshima hiyo akawapa Wayahudi uhuru wa kuendelea na sheria zao na akapunguza masharti fulani kwa wayahudi.
Ushuhuda huu unaonyesha jinsi jamii ya Kiyahudi ya wakati huo ilivyohusisha moja kwa moja Danieli 8 na Alexander.
Kuna athari Zilizodumu Hadi Leo Sababu ya Alexander Great, mfano
Alexandria ya Misri: Mji aliouanzisha mwaka 331 K.K. uliendelea kuwa kitovu cha elimu na biashara, ukihusishwa na Maktaba ya Alexandria na kituo cha kitaaluma na Museum.,waliofika Misri wanajua haya makumbusho na Kuna mji wa Alexandria
Kuenea kwa Hellenismo: Lugha ya Kigiriki cha Koine ilitumiwa kote katika Bahari ya Mediterania na Mashariki ya Kati, na ikawa msingi wa maandiko mengi ya kale.
Athari kubwa zaidi ya Hellenismo ni kwamba Kigiriki kiliendelea kuwa lugha ya elimu na sayansi kwa karne nyingi.
Wanasayansi wa kale kama Archimedes, Euclid, na Ptolemy waliandika tafiti zao kwa Kigiriki, jambo lililofanya maneno ya Kisayansi ya Kigiriki yaendelee kutumika hadi leo.
Mfano wa maneno ya asili ya Kigiriki yanayotumika katika sayansi ni: biology (bios = maisha), physics (physis = asili), astronomy (astron = nyota).
Pia, alama nyingi za hisabati na fizikia hutumia alfabeti ya Kigiriki (mfano: π, Ω, α).
Kuhusu Wapinzani wa Biblia na
Wakosoaji ,wengi wamekosa hoja , maana imetabiri kwa usahihi kabisa .
Hata hivyo, ushahidi wa kihistoria na wa maandiko unaonyesha kwamba Danieli aliandika unabii huu katika karne ya 6 K.K., muda mrefu kabla ya kuzaliwa kwa Alexander.,Zaidi ya miaka 200 .
Hata wakosoaji hulazimika kukiri kwamba Danieli 8 inamtaja wazi “mfalme wa Uyunani” na vita dhidi ya Uajemi, jambo linalolingana kwa ajabu na historia ya Alexander.
Hoja yao pekee inabaki ni tarehe ya uandishi lakini maudhui yenyewe yanaonyesha utimilifu wa unabii kwa usahihi wa kipekee.
Ushindi wa Uyunani dhidi ya Uajemi, kifo cha ghafla cha mfalme wa kwanza, na mgawanyo wa himaya yake katika falme nne zisizo na nguvu kama zake.
Historia, ushuhuda wa Josephus, na athari za Hellenismo zinathibitisha kwamba matukio haya yalitimia kama ilivyotabiriwa. Ueneaji wa lugha ya Kigiriki na urithi wa kielimu wa enzi ya Alexander umeendelea kugusa dunia hadi leo kutoka kwenye majina ya kisayansi, falsafa, na tiba, hadi alama tunazotumia katika sayansi na teknolojia.
MWISHO