Alexander Mnyeti Maji ya Shingo, miradi yake yaanza kufa mmoja baada ya mwingine

Alexander Mnyeti Maji ya Shingo, miradi yake yaanza kufa mmoja baada ya mwingine

Baada ya Magufuli kufa Lisu ana hali gani?

Bado ni mke halali wa Amsterdam
Ungeuliza baada ya Magufuli kutaka kumuua Lissu, sasa yuko kwenye hali gani? Mungu hadhihakiwi. Mshenzi alikuwa anajifanya mtu wa Mungu, kila siku analazimisha kupewa nafasi ya kuhubiria madhabahuni, kumbe ni muuaji!
 
Huyu ni miongoni mwa wale waliokuwa wanafaidi matunda ya nchi kwenye utawala wa Awamu ya 5, ni mmoja wa wale viongozi wa ngazi ya chini waliokuwa na Kiburi kilichopitiliza , inadaiwa alikuwa na uhusiano wa Kindugu na John Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania .

Mnyeti aliokotwa kutoka kwenye ualimu na kupewa Ukuu wa Wilaya , ghafla akaanza kuwa Tajiri wa kutupwa na dharau na kejeli vikamwingia ( ulevi wa madaraka ) , akapandishwa cheo na kuwa RC , akaanza kumiliki miradi kadhaa ikiwemo timu ya soka inayoitwa Gwambina , akapewa na TCC CLUB na kuiita Gwambina , ili ajenge hostel kwa ajili ya timu yake , akajenga na uwanja wa soka , yaani RC anajenga uwanja wa soka ambao Taasisi nyingi za nchi hii hazina , alikopata hela anajua mwenyewe , japo inadaiwa alikuwa na kolabo na mkubwa kwenye mashimo ya madini (tetesi) , kukawa na mpango wa kupewa Uwaziri , ikabidi kwanza aanzie kwenye ubunge wa Misungwi , wapinzani wakahujumiwa , akapita bila kupingwa .

Waswahili wanasema ukiona ngedere mjini basi ufahamu kwamba kafugwa , mfugaji akifa huyo ngedere atarudi mwituni au atakufa njaa , Sasa kwa kufupisha ni kwamba , Timu ya soka ya Gwambina inayomiliki uwanja wake , ambayo ni Mali ya Mnyeti ,
sasa IMEJIONDOA KWENYE CHAMPIONSHIP kwa kile kinachodaiwa ni kuelemewa na gharama za uendeshaji , Yaani baada ya Magufuli kufa Mnyeti anashindwa kuendesha Timu ! Hivi mnanielewa lakini jamani ?

Neno la leo linatoka kwenye kitabu cha YEREMIA 17 : 5-8

View attachment 2457682

Itaendelea ........
Watanzania seems tunaombeana laana kila kona
 
Unafuraia kufilisika kwa mwenzako hujui kwamba Kuna familia zitateseka hapo
 
Kwani mtoa mada hujui kwanini watu wanapigania uongozi japokuwa ni matajiri? Wanaogopa kufilisika viongozi wengi wabongo huwa hawawezi kutenganisha nyadhifa zao na utajiri wao wakipoteza nyadhifa na utajiri unapotea
 
Kuwachukia waliofanikiwa kwa njia za wizi ni kiungo muhimu kwa maskni kufanikiwa. Trust me. Kila maskini anatakiwa kuwa na chuki ya hali ya juu kwa mafisadi ili nchi iendelee.

Ulimuona anaiba? Una ushahidi? Maisha yake unayajua?
 
Masikini hufurahia kufilisika kwa matajiri!
Hili neno lipo mahali pengi nadhani nasema (nadhani) hata kwenye maandiko.

Mimi nafahamu masikini kuingia peponi inabidi itumike nguvu kubwa sana!.

UMASIKINI NI DHAMBI KUBWA SANA!.
 
Kwanza umeshasema alikuwa ana share kwenye madini kwa hiyo ndipo alipokuwa anapata pesa ukichukulia huyu alikuwa mkuu wa mkoa wa manyara ambapo kuna machimbo ya tanzanite.
Lakini kuhusu uwanja labda utuambie ni uwanja upi alioujenga na uko wapi maana kama tcc club pale alipopanga kuendesha club uwanja upo tokea ye akiwa chuo cha ualimu kabla hajafika kote huko ulikosema.

Kuhusu uchaguzi hakuna jimbo ambalo nyie hamjasema mmehujumiwa, yaani kuanzia urais hadi ubunge hakuna pointi ambayo hamjahujumiwa.
 
Kwanza umeshasema alikuwa ana share kwenye madini kwa hiyo ndipo alipokuwa anapata pesa ukichukulia huyu alikuwa mkuu wa mkoa wa manyara ambapo kuna machimbo ya tanzanite.
Lakini kuhusu uwanja labda utuambie ni uwanja upi alioujenga maana kama tcc club pale alipopanga kuendesha club uwanja upo tokea ye akiwa chuo cha ualimu kabla hajafika kote huko ulikosema.
Nyie misukule kwelikweli..chawa yoyote wa jiwe hata awe mchafu kiasi gani kwenu ni malaika
 
Kwanza umeshasema alikuwa ana share kwenye madini kwa hiyo ndipo alipokuwa anapata pesa ukichukulia huyu alikuwa mkuu wa mkoa wa manyara ambapo kuna machimbo ya tanzanite.
Lakini kuhusu uwanja labda utuambie ni uwanja upi alioujenga na uko wapi maana kama tcc club pale alipopanga kuendesha club uwanja upo tokea ye akiwa chuo cha ualimu kabla hajafika kote huko ulikosema.

Kuhusu uchaguzi hakuna jimbo ambalo nyie hamjasema mmehujumiwa, yaani kuanzia urais hadi ubunge hakuna pointi ambayo hamjahujumiwa.
Uwanja wa soka ameujenga Misungwi na umetumika sana tu , kuwa na share za mchongo kwenye machimbo ni ufisadi , maana kwa kiongozi wa umma huo ni utovu wa maadili .

Kingine ni kwamba wao hawakuwa wanafuata sheria za kuuza madini kama walivyowafanyia wachimbaji wengine , walitorosha madini watakavyo huku wengine wakiwajengea ukuta ( Hii mada italetwa kwa uzi tofauti )
 
Masikini hufurahia kufilisika kwa matajiri!
Ni kama nyinyi mlivyokuwa mnafurahia kina lema walivosota jela kwa kesi za kisoro na kipuuz za kusingiziwa. Ni kama nyinyi mlivyofurahia mbowe kuporwa bilicanas na shamba lake kuharibiwa. Ni kama nyinyi mlivyofurahia braza lissu kumimiminiwa risasi. Sukuma gang go to hell
 
Uwanja wa soka ameujenga Misungwi na umetumika sana tu , kuwa na share za mchongo kwenye machimbo ni ufisadi , maana kwa kiongozi wa umma huo ni utovu wa maadili .

Kingine ni kwamba wao hawakuwa wanafuata sheeia za kuuza madini kama walivyowafanyia wachimbaji wengine , walitorosha madini watakavyo huku wengine wakiwajengea ukuta ( Hii mada italetwa kwa uzi tofauti )
Unathibitisha vipi kama ni mchongo? Vipi kama ana nyaraka kamili za kumiliki?

Kama ni biashara kuna kiongozi gani chadema asiye na biashara pamoja na dili za michongo? na juzi Sugu akiwa iringa akamshabikia Samia kuzuia TRA kukusanya kodi na bado akakiri ni sheria hivyo Samia aifute hiyo sheria ya TRA kukusanya kodi walizozikwepa nyuma.
 
Back
Top Bottom