Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Alexander Mnyeti ni mtoto wa dada wa Magufuli. Huyu ndiyo mtu pekee ambaye wakati wa Magufuli alikuwa na uwezo wa kutaka chochote kwa mjomba wake na mjomba asipindue. Mnyeti akiwa RC Manyara alikuwa ana njia yake ya chini kwa chini ya kutorosha Tanzanite Kyle Mererani, huku Magufuli akituzuga kwa kujenga ukuta.Huyu ni miongoni mwa wale waliokuwa wanafaidi matunda ya nchi kwenye utawala wa Awamu ya 5, ni mmoja wa wale viongozi wa ngazi ya chini waliokuwa na Kiburi kilichopitiliza , inadaiwa alikuwa na uhusiano wa Kindugu na John Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania .
Mnyeti aliokotwa kutoka kwenye ualimu na kupewa Ukuu wa Wilaya , ghafla akaanza kuwa Tajiri wa kutupwa na dharau na kejeli vikamwingia ( ulevi wa madaraka ) , akapandishwa cheo na kuwa RC , akaanza kumiliki miradi kadhaa ikiwemo timu ya soka inayoitwa Gwambina , akapewa na TCC CLUB na kuiita Gwambina , ili ajenge hostel kwa ajili ya timu yake , akajenga na uwanja wa soka , yaani RC anajenga uwanja wa soka ambao Taasisi nyingi za nchi hii hazina , alikopata hela anajua mwenyewe , japo inadaiwa alikuwa na kolabo na mkubwa kwenye mashimo ya madini (tetesi) , kukawa na mpango wa kupewa Uwaziri , ikabidi kwanza aanzie kwenye ubunge wa Misungwi , wapinzani wakahujumiwa , akapita bila kupingwa .
Waswahili wanasema ukiona ngedere mjini basi ufahamu kwamba kafugwa , mfugaji akifa huyo ngedere atarudi mwituni au atakufa njaa , Sasa kwa kufupisha ni kwamba , Timu ya soka ya Gwambina inayomiliki uwanja wake , ambayo ni Mali ya Mnyeti ,
sasa IMEJIONDOA KWENYE CHAMPIONSHIP kwa kile kinachodaiwa ni kuelemewa na gharama za uendeshaji , Yaani baada ya Magufuli kufa Mnyeti anashindwa kuendesha Timu ! Hivi mnanielewa lakini jamani ?
Neno la leo linatoka kwenye kitabu cha YEREMIA 17 : 5-8
View attachment 2457682
Itaendelea ........
tuzuga