Mimi ni Mkatoliki, tena ex seminarian na niliachia ngazi hatua moja kabla sijawa shemasi. Kanisa Katoliki japo bado lina waumini wengi, kiuhalisia limepoteza kabisa mwelekeo. Limetoka kuwa chombo cha ukombozi wa mwanadamu kiroho (human spiritual redemption) na kumgeuza muumini wake kuwa mtaji wa maendeleo ya kanisa. Ukienda kanisani, wimbo, mahubiri, semina na Kila kitu ni MICHANGO tu. Hakuna sehemu au mahali popote ambapo kanisa linashughulika na maendeleo ya kiroho ya muumini wake na ukitaka uimbwe sana kanisani, toa sadaka na michango sana. Lakini ukiomba uchangiwe na kanisa hata ada ya mwanao, kanisa halina kabisa habari nawe. Wakatoki ni mbumbumbu kabisa wa Neno la Mungu Kwa sababu licha ya mapadri wetu kusoma sana, lakini hawatufundishi chochote kanisani zaidi ya kuhimiza tu michango isiyokwisha na isiyo na maelezo timilifu. Hivyo kwenda kwa Mwamposa is inevitable na kwa kuwa viongozi wa kanisa Katoliki, ni waoga sana kupoteza supremacy (Kwa vile wao hawana karama ya kutenda miujiza), basi ni lazima wampinge Mwamposa