Ali Kamwe achaguliwa kuwa Afisa Habari wa Yanga

Ali Kamwe achaguliwa kuwa Afisa Habari wa Yanga

Itabidi clubs nyingine waige,haijawahi kutokea team kuwa na afisa habari toka media
Pia kuwa na digital manager na app ya club
Yanga ni mfano wa kuigwa
Ilianza azam fc kumchukua zaka zakazi kutoka azam media ikafata simba kwa ahmed ally sasa unavyosema haijawah kutokea ina naana hua hufatilii habar za timu nyingne au n kujifyatua tu
 
Ila ushabiki huu unatutoa akili sana, hivi kati ya simba na yanga nani aliyeanza kuajiri msemaji kutoka katika media

Yaani ulivyoiweka ni as if simba haina msemaji na yanga ndio wa kwanza kuajiri msemaji kutoka katika media
Mkuu hao wanaendeshwa na ushabiki wa oya oya na ugeni kwenye michezo unawasumbua, hivyo ni shida kuwa katikati ya Wapunguani.
 
Kwa kuiga tu panya road wa Zambia hamjambo 😂😂😂
NB ceo wenu ana cv za jela jela tu😂😂😂😂
 
Sheria ya yanga uwezi kugombea nafasi yyte ile kama sio mwana chama hai kwa kua na kadi active.
Ndio maana wakiwa wanaambiwa kuwa n wachambuzi wa mchongo wawe wanaelewa kua watu hawakulupuki tu kusema ivyo.
Kazi njema
Mkuu kuwa mchambuzi wakati ni mfuasi ni kitu cha kawaida, sioni shida.
Mbona Wallace Karia ni Simba damu na ana kadi kabisa lakini ni boss wa vilabu vyote nchini??

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Klabu ya Yanga imemteua Mchambuzi Ally Kamwe kuwa Afisa Habari mpya wa klabu hiyo huku Privaldinho Abiud akiteuliwa kuwa msimamizi Mkuu wa Digital (Digital Manager) kwa lengo la kusimamia platforms zote za habari za klabu hiyo.
View attachment 2369989
View attachment 2369986
Ahueni timu yetu imeondokana na kile kirusi kinachoitwa Hajji Sunday Manara. Kiukweli sikufurahiwa kabisa na uwepo wake pale Jangwani.

Maana alitukejeli na kututukana kila aina ya matusi, wakati akiwa ni msemaji wa timu yake ya mbumbumbu fc.
 
Hakuna ubaya wowote hoa kina Garry Navel, Rio Ferdinand, Thierry Henry , Alli Mayai mbona wana julikana ni mashabiki na ni wachambuzi inawezekanaje mtu apende football asiwe Shabiki wa timu flani tuache unafiki
 
Sheria ya yanga uwezi kugombea nafasi yyte ile kama sio mwana chama hai kwa kua na kadi active.
Ndio maana wakiwa wanaambiwa kuwa n wachambuzi wa mchongo wawe wanaelewa kua watu hawakulupuki tu kusema ivyo.
Kazi njema
Mkurugenzi, tofautisha kati ya cheo cha kugombea, na kile cha kuteuliwa! Cheo cha Afisa Habari ni cha kuteuliwa, na siyo cha kugombea. Hivyo katika vyeo vya aina hii, ubora wa mtu hupewa kipaumbele! Na siyo kadi au uanachama wake ndani ya Klabu.
Kupitia haya mawazo yako unataka utuaminishe hata yule Mtendaji mpya wa Klabu kutoka Zambia naye alikuwa ni mwanachama wa Yanga, au Viongozi walimteua kwa uwezo wake?

Halafu utakuwa unfair kwa kumuweka Ali Kamwe kwenye hiyo orodha yako ya wachambuzi wa mchongo! To be honest; huyo Ali Kamwe na mwenzake Ahmed Ally, ni moja ya wale watangazaji ambao hawajawahi kuonesha mapenzi yao ya waziwazi kwa baadhi ya Vilabu nchini wakati wanatumikia media zao za awali, kama ilivyo kwa watangazaji wengine mfano Maulid Kitenge (Yanga), Shafii Dauda (Simba), nk. Kiufupi walijitahidi kuwa neutral.

Hivyo jukumu ketu kama wadau wa michezo ni kuwaombea tu, ili wafanye kazi inayotakiwa kwenye vilabu vyao.
Waache kutumia nguvu kubwa kwenye mipasho, matusi, kejeli, dharau, na kila aina ya ujinga. Wakumbuke kuna maisha nje ya hiyo kazi yao ya Uafisa Habari wa Klabu.
 
Mkuu kuwa mchambuzi wakati ni mfuasi ni kitu cha kawaida, sioni shida.
Mbona Wallace Karia ni Simba damu na ana kadi kabisa lakini ni boss wa vilabu vyote nchini??

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
Haji kisha waharibu mpaka kwenye nanihii!
Hilo la Karia kuwa na kadi ya Simba, unaweza kuthibitisha?
 
Ahueni timu yetu imeondokana na kile kirusi kinachoitwa Hajji Sunday Manara. Kiukweli sikufurahiwa kabisa na uwepo wake pale Jangwani.

Maana alitukejeli na kututukana kila aina ya matusi, wakati akiwa ni msemaji wa timu yake ya mbumbumbu fc.
Katika mashabiki wa Yanga ambao mlisimamia hoja zenu za kutomkubali Manara ni kweli wewe ni mmojawapo.Hata pale wengine walielekea kujaribu kuyafukia yale aliyowafanyieni akiwa Simba wewe hukuyumbishwa.
 
Back
Top Bottom