Ali Kamwe: Shabiki wa Yanga paka Bleach kichwani na kwenye Ndevu "PACOME DAY"

Ali Kamwe: Shabiki wa Yanga paka Bleach kichwani na kwenye Ndevu "PACOME DAY"

Yani nimeacha bleach last week tu hapo ndio wanakuja na Pacome Day, Sijapenda.
 
pacome ni mbonge la player! siku itafana kwa kweli! kila lenye kheri YOUNG AFRICANS sc.
 
Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga Ali Kamwe, amewataka mashabiki wa Klabu ya Yanga kujipaka Bleach kwenye mechi ya Jumamosi.

Ali Kamwe amesema,

"Mtoko wa Jumamosi ni PACOME DAY 𝐊𝐢𝐭𝐚𝐚𝐥𝐚𝐦𝐮 𝐙𝐚𝐢𝐝𝐢 .. Mwanayanga piga Breach kichwani. Piga Breach kwenye ndevu.. chora rangi shavuni, usoni .. Wadada wa Yanga Rangi za kucha Jumamosi ni Njano na Kijani"

"Bilionea GSM ameandaa zawadi Maalum kwa Mwananchi atakayetokeleza 𝐊𝐢𝐭𝐚𝐚𝐥𝐚𝐦𝐮 𝐙𝐚𝐢𝐝𝐢 kwenye PACOME DAY.. Utapigwa picha na Wananchi watapiga Kura kuchagua mshindi"-Ali Kamwe

Nini maoni yako?

✍️ Mjanja M1
Huyu Ali Kamwe naye aache tabia yake ya kufikiri na sisi mashabiki wa Yanga ni Mbumbumbu. Watu wanataka matokeo bhana.

Haya masuala ya Pacome day, Nzengeli day, Aziz Kii day, Tate Mkuu day, nk. Yana utoto ndani yake.
 
Back
Top Bottom