Swali langu ni kuwa umejuaje kama kimetungwa ? Usikwepe swali, unaposema kitu fulani kipo hivi maana yake una kijua kiundani. Sasa umeshindwa unatakiwa ukiri au ukiri ya kuwa umesikia kwa watu na wewe huwezi kuthibitisha hilo.
Sasa kwanini umesema kimetungwa huku unajua fika huwezi kuthibitisha ?
Usiwe mjinga kiasi hiki kijana, mfano Big Bang ina mantiki gani na ina uthibitisho gani au The Black Hole au Quantum Physics ina mantiki gani na ina uthibitisho gani au Infinity Series ina mantiki gani na ina uthibitisho gani au The Universal Gravitational Force ina mantiki gani na ina uthibitisho gani ?
Inaonekana huijui Sayansi bali unaishabikia Sayansi.
Ndiyo utuonyeshe hilo hitimisho limefikiwa vipi ? Na utaje hatua za kimantiki ulizo fata. Sababu mimi elimu ya Mantiki nimesoma na ninajua udhaifu wa elimu hii, hasa udhaifu wake upo katika hitimisho na si mantiki tu bali mpaka hiyo Sayansi nayo ina tatizo hilo hilo.
Huu ujinga mwingine halafu unataka ujadili hii mada. Kwani wewe unazijuaje na unazihakiki vipi habari za miaka 200 au 300 iliyo pita ?
Au mfano mwepesi ni wewe umejuaje kama Newton aliwahi kuishi au Plato au Aristosto au Socrates au George Washington ? Ulipotaka kuwajua ulirudi nyuma au unaropoka ropoka tu ? Hili ndiyo tatizo la kujadiliana na wajinga na hawajui kama hawajui.