Ali Kiba atambulisha rasmi label yake(Kingmusic) aachia nyimbo mpya "SINA".

Ali Kiba atambulisha rasmi label yake(Kingmusic) aachia nyimbo mpya "SINA".

Mimi ni shabiki wa kiba ila jamaa anazingua sikuhizi, Kiba ajipange aisee, Juzi yeye mwenyewe aliifuta "Hela" baada ya kuona dislikes kibao na comments zenye hasira kutoka kwa mashabiki kwasababu ya kazi mbovu, Tulitegemea ataleta jiwe ila sijaona cha ajabu mana kwenye hii kazi hata nuh mziwanda angefaa
usiumie mkuu ndio uwezo umeishia hapo
 
WATU WANAZIDI KUUMBUKA ASEEEE!!!HUYU JAMAA ANA KIWANGO CHA KAWAIDA SANA KATIKA KUTENGENEZA NYIMBO ZITAKAZOENDANA NA WAKATI.
Tatizo anajisahau kuendana na wakati na hitaji la soko husika
Afu rafiki zake Clouds walimtumia naona siku hizi kama wamemmwaga,sijui tatizo nini
 
Ali Kiba kama anataka afanye muziki wa kipekee basi atafute muziki wa pekee yake sio huu wa ushindani, atajikuta anakimbia mbio ambazo hawezi.

Sijawahi kupenda wimbo wa Ali Kiba mbali na Karim, kama unajua vyema na una sikio la kusikiliza utagundua Ali Kiba ni mzuri sana kwenye Rumba/Zuku tena akiimba kwa sauti original sio hii ya Yooooooo!


Sikiliza kwenye wimbo wa Karim kuna baadhi ya maneno Ali alikuwa anapachika kwa sauti yake halisi na kufanya ule wimbo kuwa mzuri kwangu sijajua kwa wengine.

Ali hawezi kuimba bongofleva siku zote atapuyanga anabana sauti akijua ndio ataimba vizuri kumbe utumbo tu.

Producer wake amshauri jamaa ajikite kwenye rumba au Zuku na aimbe kwa uhalisia wa sauti yake sio kulialia yoooo kama Mbuzi jike anataka kupandwa.
 
Aandae crew aipe promo vijana wafanye kazi ye aachane na mziki
 
Msanii nguli nchini Tanzania Alike a maarufu KingKiba ametambulisha rasmi lebal yake ya King Music kwa kuachia nyimbo mpya ya pamoja akiwa na wasanii wake. Enjoy

hawa jamaa ukiwasimamisha na Ze Mafik watalamba udongo,pamoja na bosi wao,sa ndo wimbo gani huu? anyaway ni vijana wetu tuwapokee na tuwape sapoti ya kutosha hakuna namna sasa
 
Ajikite zaidi Coastal Union kwa sasa huku kwenye muziki amwache Tandale boy.
 
Wimbo wa mwisho Alikiba kuimba ni "Aje remix", the rest ni takataka tuu
 
Mkuu alikiba namuonea huruma sana naomba niwanufaishe na wengine kwa USHAURI HUU,kwenye level ya familia yangu ninachakumjuza huyu bwana ,tukiwa kwetu marangu tulizaliwa watoto 4 wa familia moja tukiwa wadogo tulianza biashara ndogo ndogo wenzangu walikuwa na hulka ya kushindana sana ,mimi nilijitenga na ushindani huo kabisa leo hii mimi namaisha ya kawaida mazuri nyumba mbili tatu vigari vya kutembelea na tulodge ,sasa wenzangu wako so active ,so competitive wote ni matajiri sana wana misemi kibao maghorofa uchafu ,lakini nimewazidi kitu kimoja na wanakili AMANI YA MOYO,wote kwanza hawaongei kabisa wao kwa wao na hata wake zao wamerithi wanaendeana hadi kwa waganga ,wote walevi wa kutupwa na wawili wanavisukari ,wote wananipenda sana na huwa hawamalizi mwezi huja kulala na wake zao kwangu ,ila wao kwa wao hawakaribishani na husemana vibaya sana ,imerithi hata watoto wao ni wa hivyo hivyo walevi na wakorofi ,mimi namaisha ya kushinda kanisani na kushukuru kwa kidogo kinachonitosha nina amani sana...SOMO maishani usikubali kuwekwa kwenye trap ya kushindana mbio ni kweli utaweza fika mbali ila utakuwa restless maisha yote maana daima wakukuzidi atakuwepo pangilia unataka ufike wapi kadiria spidi iendee ndoto yako .UTAKUWA NA AMANI ...Haka kawimbo hakafai hata kuimbwa na beka flavor ni kakawaida sana imagine presha anayoipata kiba akipita mitaa ya Dar kila mahali jibebebebe
 
Nice move...wafanye kazi sasa.....
naona wameanza na test za WCB,,........
 
Back
Top Bottom