Ali Kiba kama anataka afanye muziki wa kipekee basi atafute muziki wa pekee yake sio huu wa ushindani, atajikuta anakimbia mbio ambazo hawezi.
Sijawahi kupenda wimbo wa Ali Kiba mbali na Karim, kama unajua vyema na una sikio la kusikiliza utagundua Ali Kiba ni mzuri sana kwenye Rumba/Zuku tena akiimba kwa sauti original sio hii ya Yooooooo!
Sikiliza kwenye wimbo wa Karim kuna baadhi ya maneno Ali alikuwa anapachika kwa sauti yake halisi na kufanya ule wimbo kuwa mzuri kwangu sijajua kwa wengine.
Ali hawezi kuimba bongofleva siku zote atapuyanga anabana sauti akijua ndio ataimba vizuri kumbe utumbo tu.
Producer wake amshauri jamaa ajikite kwenye rumba au Zuku na aimbe kwa uhalisia wa sauti yake sio kulialia yoooo kama Mbuzi jike anataka kupandwa.