Kipindi kile Kiba anarudi kwenye game,mtu ambaye alikuwa mdomoni kwake ni Diamond,katafuta kiki kwa Mondi ,kila akihojiwa mara hoo dogo aniheshimu,mara dogo amefuta verse yangu mara sijui nini,kila interview yake alikuwa akimponda Mondi alikaa kimya.Nakumbuka alijibu issue ya hiyo kufuta verse ya kiba ktk nyimbo ya lala salama,baada ya kiba kufuta verse yake ktk single boy(kwa sababu hii kwangu mimi beef lao naona ni la kitoto).Kaendelea kumwongelea mwenzake -ve kweli akafanikiwa kusimama tena kwenye game.
Zikaja kampeni za KILI MUSIC AWARDS baadhi ya media plus team, team Wema,Team Jokate na Team Kiba (Team ndipo zilipozaliwa kwenye mziki) zikaaungana ktk tuzo za KILI,kweli Diamond kuna baadhi ya tuzo wakambania,Mungu si Athuman mwaka huo huo MTV MAMA wakampa tuzo ya Best entertainer.
Jamaa baada zile team,chuki zilizosambazwa na Kiba na team za ma-ex wake ,Diamond akazomewa Fiesta.Mungu si Athumani akapambana we ,mwaka 2015 kwa mujibu wa EMC Kenya ,Mondi akaendeleza record ya kuwa msanii anayesikilizwa sana kwenye Radio na TV,hii ilimfanya apate zaidi ya mil 600.Mpaka sasa jama ana utitiri wa show,ubalozi kwenye kampuni mbalimbali na kila anachogusa kinakuwa almasi kama jina lake.
Ukiyaangalia haya matukio utakuja kugundua,alieanza maswala ya kumungelea mwenzie kwa kumpaka matope ni Kiba na hali kama hii iliyomkuta Mondi kama ingemkuta kiba nahisi angedata.
Zamani Mondi alikuwa akipayuka akiulizwa maswala ya kiba,ila siku hizi anavyo react kama hakuna kitu.Ila WCB wana kauli yao mbiu,kama ukijaribu kutengeza beef ,wao lile BEEF wanaligeuza linakuwa BIASHARA kwao.WCB hapa wanacheza mind game.