Ali Kiba hapa kwa Dulla umefeli kabla ujaanza

Unaongea ujinga tu, Salam sk ana ujanja gani? Ana fan base gani?

Watu wasifanye biashara waogope ngombe wanaopiga kelele eti kuigana, hizo biashara za peke yake zifanyeni nyie mtuboe, acheni chuki na wivu
 
kwenye media atafeli vibaya sana,maana kaingia katika kipindi ambacho ushindani ni mkubwa sana,na inataka mtaji mkubwa na ubunifu wa hali ya juu
Hizi ni kelele za mkund haziboi choo, watanzania tupunguze chuki na kuombeana mabaya, mtu hajaanza hata kazi umeshamtabilia atafeli,

Unadhani kakurupuka kuwekeza? Hakuna mtu anakurupuka kufanya kitu bila kufanya tathimini, mnadhani atafanya kila kitu yeye ile ni kampuni lazima watajiliwa watu wenye weredi.!
 
Uko sahihi 100%. Wasanii kwenye biashara hakuna kitu. Miaka ya zamani niliona AY ana duka la nguo Sinza ila ghafla likafa kifo cha kawaida.. list ni ndefu ya wasanii walioanzisha biashara zikafa kizembe. Kinachouma ni kwamba ule muda wao wa kuwika ukipita huwa ni ngumu sana kurudi juu tena. Mwaka 2000 mojawapo ya wasanii wakubwa duniani alikuwa Sisqo wa Dru Hill lakini kufikia 2002 alipotezwa vibaya na kina 50cent na chupukizi wengine. Mara ya mwisho niliona Sisqo anatangaza show yake ya Kinshasa Drc. Wasanii wawe na nidhamu ya ndani na nje ya muziki. Wengi wao hawana nidhamu kotekote.
 
Uko sahihi 100%. Biashara ya redio ni pasua kichwa sana. Watu wengi walioanzisha redio wanajuta kwa sasa. Zamani ilikuwa redio hazigombei matangazo na watu wa mitandaoni ila kwa sasa watu wa mitandaoni wanawapelekea moto vibaya radio na TV stations. Watangazaji na waandishi wana hali ngumu sana kiuchumi kutokana na wamiliki kukosa pesa.
 
Hayo yote yamekuja baada ya Alikiba kuanzisha media yake, u team unawafanya mnakua wanafiki.,

Mpaka kufikia hatua ya kuanzisha media unadhani yeye hajafanya tathimini? Weww una uzoefu kwenye media kumzidi salim kikeke?

Punguzeni ujuaji acheni watu wawekeze wanakoona kunawafa na kuwalipa hakuna mjinga wa kutupa pesa yake akijua kua inaenda kuteketea,

Kisa fulani alifeli kwenye biashara fulani ndo wengine wasiifanye? Kila mtu anaplan na target zake kwenye biashara.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nimefanya kazi kwenye media company kwa miaka kadhaa tena upande wa management. Najua nilichosema. Inawezekana Kikeke ni mzoefu tu wa studio ila kwenye biashara akawa mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…