Ali Kiba nae kaanza ku promote video zake kwa kulipia mtandaoni

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
1627979801041.png

Wengi tunakumbuka miaka ya nyuma Diamond ndie alikuwa msanii pekee aliekuwa ana promote video zake kwenye mitandao ya kijamii kwa kulipia, hiii ikapelekea kuongezeka kwa umaarufu mpaka sasa imefikia hatua kaacha ku promote kwa malipo maana kwa sasa anafaidi mavuno ya mashabiki wapya aliowapata.

siku wakati ngoma ya Jealous ya Alikiba inatoka niliona tangazo la sponsored (matangazo ya kulipia) na page iliyotangaza n ya ali kiba.

Nilishangaa sana maana kundi la wasanii wengi walikuwa wanalalamika zamani ukifanya hivi ndio kununua views, ila leo wenyewe wameanza kufuata mkondo aliopitia Diamond, hakika Teknolojia huwezi kubishana nayo.

Unapofanya matangazo ya sponsored unaweza kufikisha tangazo kwa watumiaji wa instagram au facebook, ukachagua tangazo liwafikie watu wa nchi gani, rika gani, wanaoishi katika jiji au kijiji gani, jinsia ,n.k zile taarifa tunazojazaga facebook au instagram ndio zinatumika.

Wengi pia wanashangaa ni kwanini alikiba ana views wengi ila ni trending namba 2, Jibu rahisi ni kwamba watazamaji wengi wame view hio video kupitia tangazo na huenda tangazo linafikia watu ambao wapo sehemu mbali mbali na sio sehemu moja, mfano waliocheki video kupitia tangazo wapo katika nchi 20 tofauti, sasa kwa namna hii hao watu hawawezi kujumuishwa kwenye esabu za trending za Tz na ndio maana bado Ali Kiba yupo namba 2, views nyingi anazopata ni za matangazo.

Yote kwa yote, Hongera kwa wasanii kuanza kufata njia za kupush mziki wao ufike mbali na sio kuridhika tu na kutambulisa ngoma kwenye vituo vya radio.
 
Ali kiba kaupiga mwingi Sana ana ka-mziki Fulani hivi kametulia Sana! Jealous [emoji91][emoji91]

Nampongeza pia diamond platnumz wanapambana kusaka maisha Huku wajinga wachache wanabaki kukosoa!
 
Yes, Ali Kiba kaamua kuwaza mbali, Mambo ya kuona aibu kwamba atachekwa kisa ka promote video yake kama alivyokuwa akifanya mwenzake miaka ya nyuma kaamua kuyaweka kando, Kupambana na teknolojia ni kazi mno,

wasanii wengine nao waanze ku promote video zao tu, kuna wasanii wanapenda ku mix kiingereza na kiswahili kama kina niki mbishi, hawa inabidi wapromote sana kazi zao kwa majirani zetu Kenya
 
Wenzako wanapata pesa unajifanya mchambuzi wa muziki uchwara
Views wa alikiba wametoka hapa bongo na mpaka Nigeria kutokana na uwepo wa mayorkun...
Finish
 
oohh kiba kaisha

sadala aka magodoro anahaha sasa

independent hapa kimyaaaaaaa, na wale mashoga mavi wa diamond kimya kabisa JF hii
 
Unafikiri yuko neutral huyo?!! Soma post yake iliyo #3
He is neutral yeah, unless kama kitu haujakipenda lakini amejitahidi kueleza uhalisia ulivyo.
Hii ni kama tu utaisoma na neutral mind.
 
Hivi Wakenya hawaangalii nyimbo zao, nashangaa Wabongo kutawala popular trending za Kenya.
IMG_20210804_000702.jpg
 
Kuna ujinga fulani unaendelea huko u tube...

Yani ni kama Mondi ndio mwenye haki ya kutrend number one....

Sijui michezo hii inachezwaje... Licha ya Kiba kumzidi views kwa mbaaliii
 
Nilitaka kuuliza humu sasa hivi ili nipate elimu. Mwanzo nilijua mwenye views nyingi ndiye anayetrend. Leo siku ya tatu kiba anaongoza dhidi ya diamond lkn no.1 anabaki kuwa diamond........sielewi tu.

Pia naomba kujua hapo anaepiga mpunga mwingi ni nani; anaetrend au anaeongoza views?!!
 
Kazi kweli.. Kuna namna.. Mambo ya fake views...
 
View attachment 1878292

Wengi tunakumbuka miaka ya nyuma Diamond ndie alikuwa msanii pekee aliekuwa ana promote video zake kwenye mitandao ya kijamii kwa kulipia, hiii ikapelekea kuongezeka kwa umaarufu mpaka sasa imefikia hatua kaacha ku promote kwa malipo maana kwa sasa anafaidi mavuno ya mashabiki wapya aliowapata.

siku wakati ngoma ya Jealous ya Alikiba inatoka niliona tangazo la sponsored (matangazo ya kulipia) na page iliyotangaza n ya ali kiba.

Nilishangaa sana maana kundi la wasanii wengi walikuwa wanalalamika zamani ukifanya hivi ndio kununua views, ila leo wenyewe wameanza kufuata mkondo aliopitia Diamond, hakika Teknolojia huwezi kubishana nayo.

Unapofanya matangazo ya sponsored unaweza kufikisha tangazo kwa watumiaji wa instagram au facebook, ukachagua tangazo liwafikie watu wa nchi gani, rika gani, wanaoishi katika jiji au kijiji gani, jinsia ,n.k zile taarifa tunazojazaga facebook au instagram ndio zinatumika.

Wengi pia wanashangaa ni kwanini alikiba ana views wengi ila ni trending namba 2, Jibu rahisi ni kwamba watazamaji wengi wame view hio video kupitia tangazo na huenda tangazo linafikia watu ambao wapo sehemu mbali mbali na sio sehemu moja, mfano waliocheki video kupitia tangazo wapo katika nchi 20 tofauti, sasa kwa namna hii hao watu hawawezi kujumuishwa kwenye esabu za trending za Tz na ndio maana bado Ali Kiba yupo namba 2, views nyingi anazopata ni za matangazo.

Yote kwa yote, Hongera kwa wasanii kuanza kufata njia za kupush mziki wao ufike mbali na sio kuridhika tu na kutambulisa ngoma kwenye vituo vya radio.
Nilishangaa sana maana kundi la wasanii wengi walikuwa wanalalamika zamani ukifanya hivi ndio kununua views, ila leo wenyewe wameanza kufuata mkondo aliopitia Diamond, hakika Teknolojia huwezi kubishana nayo.[emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Nilitaka kuuliza humu sasa hivi ili nipate elimu. Mwanzo nilijua mwenye views nyingi ndiye anayetrend. Leo siku ya tatu kiba anaongoza dhidi ya diamond lkn no.1 anabaki kuwa diamond........sielewi tu.

Pia naomba kujua hapo anaepiga mpunga mwingi ni nani; anaetrend au anaeongoza views?!!
Kupiga pesa YouTube inatokana na Matangazo mkuu na inategemea na Aina ya Matangazo yenyewe, obviously Kwa Tanzania msanii ambae analipwa hela nyingi itakuwa Diamond kwakuwa yeye ni maarufu kuliko wengine lakini pia watakaolipa hela yao waamini Matangazo Yao yatatazamwa mbali zaidi

So kupiga hela hakuna uhusiano na kuwa trending, kuwa trending maana yake ni kwamba Kwa muda huo wewe unaangaliwa zaidi Kwa nchi husika, unaweza kuwa unaangaliwa Zaid Tanzania Ila alie trending namba 2 akawa anaangaliwa zaidi nchi zingine
 
Shukrani sana kiongozi
 
Back
Top Bottom