sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Wengi tunakumbuka miaka ya nyuma Diamond ndie alikuwa msanii pekee aliekuwa ana promote video zake kwenye mitandao ya kijamii kwa kulipia, hiii ikapelekea kuongezeka kwa umaarufu mpaka sasa imefikia hatua kaacha ku promote kwa malipo maana kwa sasa anafaidi mavuno ya mashabiki wapya aliowapata.
siku wakati ngoma ya Jealous ya Alikiba inatoka niliona tangazo la sponsored (matangazo ya kulipia) na page iliyotangaza n ya ali kiba.
Nilishangaa sana maana kundi la wasanii wengi walikuwa wanalalamika zamani ukifanya hivi ndio kununua views, ila leo wenyewe wameanza kufuata mkondo aliopitia Diamond, hakika Teknolojia huwezi kubishana nayo.
Unapofanya matangazo ya sponsored unaweza kufikisha tangazo kwa watumiaji wa instagram au facebook, ukachagua tangazo liwafikie watu wa nchi gani, rika gani, wanaoishi katika jiji au kijiji gani, jinsia ,n.k zile taarifa tunazojazaga facebook au instagram ndio zinatumika.
Wengi pia wanashangaa ni kwanini alikiba ana views wengi ila ni trending namba 2, Jibu rahisi ni kwamba watazamaji wengi wame view hio video kupitia tangazo na huenda tangazo linafikia watu ambao wapo sehemu mbali mbali na sio sehemu moja, mfano waliocheki video kupitia tangazo wapo katika nchi 20 tofauti, sasa kwa namna hii hao watu hawawezi kujumuishwa kwenye esabu za trending za Tz na ndio maana bado Ali Kiba yupo namba 2, views nyingi anazopata ni za matangazo.
Yote kwa yote, Hongera kwa wasanii kuanza kufata njia za kupush mziki wao ufike mbali na sio kuridhika tu na kutambulisa ngoma kwenye vituo vya radio.