Huwa anajiona keki sana yani
Angefikia robo ya mafanikio ya diamond inaonekana hata mate angekuwa anawatemea
Si lazima wote wafikie hata robo ya mafanikio ya Naseeb wengine walipofika panawatosha na wanaona wamefika na kuanza kujisifu.
Huoni wa la kwanza hujivuna , wa la saba hujivuna, kidato cha nne cha sita ,cheti, stashahada, shahada ya kwanza, uzamili na udhamivu pia hujisifu na kujiona wanastahili walichopata hawaangalii kama kuna wa zaidi yao wanachojali walichonacho.
Mwenye baiskeli hujivuna nayo, mwenye pikipiki mwenye gari na mwenye ndege pia.
Aliyepanga na mwenye nyumba wote wana muda hufurahia walivyonavyo.
Hata bwana Naseeb alikisifia alipokuwa hatua ya chini na kukejeli wengine kama Ally afanyavyo.
Ni hulka tuu, mwache afanye akionacho chamfaa atimize furaha yake.
Maisha mafupi sana haya, alichokipata hadi sasa ni zao la kazi yake hata kama angeongeza juhudi angekuwa juu zaidi.