Hilo linawezekana. Basi tupe biashara au investment zake kubwa hapa bongo
Ally Mufuruki ..huyu huyu aliechangia kufilisi Air Tanzania akiwa na yule jamaa wa Africa kisuni au mdogo wake??Inabidi amuombe radhi tena kwa maandishi
Mfuruki ni mjanja mjanja tu wa hapa mjini. Fobes wanasema Jamaa yupo top 10 kwa matajiri Tanzania, wakati jamaa hatujui kabisa bussness zake zaidi ya maduka ya Wolwoth sidhani kama ana kiwanda or tangible investmen
Na kipindi hicho ndo akaimarisha hiyo W-stores..si mbaya kama amekuwa mzalendo siku hizi..ahhhaaahh.Nakubaliana na wewe kuwa huyu ALi MFURUKI NI MJANJA MJANJA MMOJA HAPA MJINI. Kwa wale wenye kumbukumbu nzuri mtakumbuka kuwa huyu bwana aliwahi kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa board ya ATC [shirika letu la ndege ] na akita na wadhifa huo ndio akatuingiza ubia na shirika la ndege ya Afrika ya Kusini [SAA]. Ubia kati ya mashirika haya mawili ulikuwa kwa faida zaidi ya wenzetu kuliko shirika letu kiasi kwamba ATC ilibambikizwa madeni hewa under Mfuruki's watch kumbe huku yeye alikuwa anavuta mkwanja kwa njia za kiwizi!!
Hata hiva sasa bado shirika na ndege la Africa Kusini linadai ATC Fedha nyingi ambazo huko mbele zinaweza kusababisha ndege zetu mara zikitua huko zikakamatwa kwasababu ya ufisadi wa huyu bwana na genge lake!! Ni mnafiki anyejifanya kuwa ni mzalendo kumbe ni mou anayeishi kwa Ujanja Ujanja tu wa TAX AVOIDANCE/ EVASION!!!
Na sasa eti hapa kazi tuuuu!! Hakuna kitu!!Kwa hivyo anashauri nini kuhusu uwekezaji wa viwanda?
Tuache sababu ya muda au tuendelee?
Watanzania kwa kutaka njia ya mkato na matokeo makubwa sasa ndio maana tulichotwa akili
"Kasi mpya hari mpya"
Mara tunasikia
"Big result now (BRN)"
Mkuu aina gani ya tv?TV yangu Ni digital TV ukifunga nje antenna ya samaki namaanisha iliyochanua coz inareceiver ndani ukisearch unapata channel kibao FREE to air so Nabaki na Dstv yangu ila taarifa ya habari taangalia itv
Sent using Jamii Forums mobile app
Sera ya viwanda inabidi ifanyiwe marekebisho.
1. Kuchagua specifically aina gani ya viwanda tunavitaka
Hii inawezekana pale ambapo idara za usalama zinafanya kazi kwa maslahi ya taifa na siyo ya serikali.Nimemsikiliza, ana mambo mazuri sana na uelewa mkubwa wa masuala ya uwekezaji na mitaji.
Alitolea mfano Singapore, wanapotafuta mwekezaji, wanakuwa wamefanya utafiti wa kutosha juu ya uwezo was Hugo mwekezaji wanayemtaka, na wao kama nchi wanakuwa pia wamekwisha Fanya utafiti wao na kuweka mazingira rafiki, pamoja na kumhakikishia faida atakayopata.
Pia wanamhakikishia Sera zisizobadilika badilika kwenye uwekezaji. Nimemfurahia sana, na watendaji wetu has a TIC na Waziri wa viwanda na biashara, wana kitu cha kujifunza.
Amedai, huwezi kusema tunataka kuwa nchi ya viwanda bila kuainisha aina ya viwanda, mkakati wa kupata wataalamu, mkakati wa kupata malighafi na masoko pia. Akatoa mfano, Tz kwa mwaka wahitimu mainjinia ni 1,200 nchi yenye watu milioni 50 wakati Singapore watu mil 30 inawahitimu zaidi ya laki moja kwa mwaka.
Hebu tupeni Cv ya Ally Mufuruki wakuu.
Huyu jamaa atakuwa hajasoma UDSM aisee hii ni Havard Bussiness School (HBS) or Massachusetts Insititute Of Technology (MIT) maana kwenye masuala ya viwanda jamaa yuko well informed.
Over