Alichoandika MwanaHistoria Mohamed Said, Baada Tamko La Askofu Rais Wa TEC

Hiki kizee sijui kimeahidiwa mabikira wangapi huko jehanamu
Mbalizi...
Mbona imekuwa matusi?
Tena matusi ya kumkashifu Allah aliyewataja mabikra katika Qur'an.

Haifai hata kidogo.

Jadili niliyoandika.
Usitukane Uislam wala usinitukane mie.

Hii kizee vipi tena?

Kitabu cha Abdul Sykes nimeandika nikiwa kijana na nilianza utafiti
nikiwa kijana zaidi.

Usidhani kwa kuwa unajificha katika jina bandia hilo linakupa ruhusa
ya kutukana watu mitandaoni.

Angalia picha hapo chini nimepiga leo asubuhi nikiwa studio nakitia
kitabu cha Shaaban Robert kwenye sauti (audio book).

Kizee ndicho hicho hapo chini:



Mie nina heshima yangu hapa JF.
Angalia picha nyingine hapo chini.



Umekiona kizee hiki?
 
Sina tatizo na fikra zako.

Mimi nimefafiti historia ya uhuru na akili yangu imeniambia kuwa
kukosekana kufamika kwa historia ya hao wote waliokuwa hawako
katika historia ya uhuru si sawa.

Ndiyo nimeandika kitabu cha Abdul Sykes.

Watu wengi wanashtuka wanaposikia historia kwanza ya babu yake,
Sykes Mbuwane aliyeingia German Ostafrika na Herman von Wissman,
baba yake Kleist Sykes na wazalendo wengine wa wakati ule kama Sheikh
Hassan bin Ameir, Hamza Mwapachu, Steven Mhando, Earle Seaton kwa
kuwataja wachache.

Kwa kazi hii nimealikwa vyuo vikuu vingi ndani na nje ya mipaka yetu kutoa
mihadhara.

Ikiwa wewe hupendezewi wala mimi sikubughudhi.
Naheshimu msimamo wako.

Angalia picha hapo chini Al Jazeera wamekuja kutoka Qatar kufanya mahojiano
na mimi mwaka wa 2007:

 
No Reform no Election!
 
Habari ya Kanisa la Lindi inahisiano vipi matamshi ya Askofu Jumapili?!
 
Wagalatia ni shida sana, yaani mtu akiandika uislam haraka sana mnambandika udini, ila ukiandikwa ukristo kila mmoja anafurahia,

Kwa ushahidi tu wa mazingira nani mdini?

Alishindwa firauni nfio mtaweza nyie?
Inside10
Jarib
Baba yangu mimi naomba unisaidie jambo moja dogo tu..

Lengo lako hasa la andiko hili nini?!
Maana tamko la askofu huyo wa Lindi lilikuwa ni kuzungumzia uchaguzi wa huru na haki, pia kuachiwa kwa wanasiasa (lissu) ambae anadai taratibu sahihi za uchaguzi na mwenendo wake?

Sasa wewe umekuja na historia uhuru lindi nà mambo ya lindi kuwa mji wa kiislamu, uhusiano wake na tamko la askofu ni nini?!

Ahsante ukinijibu hili moyo wangu utakuwa umesuhuzika.
 
Mkuu 'inside10', umegonga penyewe hasa. Sina la ziada la kuongezea hapa. Ni wazi hawa waTanzania wenzetu wana ajenda nyingine zaidi ya kujenga umoja na mshikamano kati yetu.
 
Mkuu 'inside10', umegonga penyewe hasa. Sina la ziada la kuongezea hapa. Ni wazi hawa waTanzania wenzetu wana ajenda nyingine zaidi ya kujenga umoja na mshikamano kati yetu.
Naona amekwepa sana kunijibu na nimemkumbishia tena kwenye post #188
 

Huyu askofu mbona sijawahi kumsikia kuzungumzia haki ya Zanzibar katika muungano wala sikumsikia kusema chochote wakati wale masheikh waliposota miaka zaidi ya 9 gerezani , na hawa ambao mpaka leo wako gerezani kwa zaidi ya miaka 10 kwa kesi za kubambikiza za ugaidi ??
 
Lengo lake ni kueleza historia ya TANU Lindi.

Naeleza kile kilichotokea ndani ya Kanisa Katoliki, Lindi wakati
wanachama wa TANU walipomsindikiza Mwalimu Julius Nyerere
ndani ya kanisa hilo kwa ajili ya Misa ya Jumapili.

Hapakuwa na mwanachama hata mmoja Mkristo kumsindikiza
Mwalimu Kanisani.

Hii ikasababisha Mwalimu asindikizwe na Waislam.
Nakuongezea mengine hapo chini katika historia ya TANU Lindi:

''Salum Mpunga alimsisitizia Nyerere umuhimu wa yeye kwenda Lindi ambako kunaweza kuwa ndiyo chanzo cha TANU kupata ufanisi Newala, Songea, Tunduru na Masasi ambako kulikuwa na upinzani mkubwa dhidi ya TANU.

Kanisa lilikuwa likiwazuia Wakristo kujiunga na TANU.

Sheikh Suleiman Takadir, Said Chamwenye, John Rupia, Ali Mwinyi Tambwe wote waliunga mkono ule ujumbe wa Lindi juu ya suala hili.

Baada ya kufikia makubaliano, Mpunga na Ali Mnjawale walipewa barua ya kuthibitisha safari ya Nyerere.
Ziara ya Nyerere ilikuwa ianze muda mfupi kutokea hapo kwa kuwa ilikuwa ndiyo siku za mwisho za kiangazi.

Barabara sehemu ya kusini ya Tanganyika zilikuwa hazipitiki wakati wa masika, zikiitenga kabisa kusini toka sehemu zilizobaki za nchi.

Ali Mwinyi Tambwe na Rajab Diwani walifuatana na Nyerere kwenda Jimbo la Kusini kuondoa wasiwasi na woga uliozushwa na Gavana Twining na kibaraka Yustino Mponda.''

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)
 
Naona amekwepa sana kunijibu na nimemkumbishia tena kwenye post #188
Inside10,
Sina sababu ya kukwepa chochote.
Mimi nikukwepe wewe?

Kwa kipi kikubwa?

Mimi nimefanya mijadala ya uso kwa uso kwingi duniani
na hawa hawajaacha kunialika.

Halikadhalika nimepokea tuzo kadhaa.
Nikukwepe wewe hapa JF mtu ambae umeficha sura yako?


Mzumbe University 2004
 
Kalamu
Jibu la ile hoja yako ambayo niliikazia kwenye #131 ndio hili..

Swali la ziada mzee wangu..
Kulikuwa kuna haja gani nakuambatanisha na kauli ya askofu wakati ni vitu viwili tofauti?!
Cc Mwalihehe
 
Kwanza historia hiyo anayodai ndiyo sahihi, inaorodhesha majina tu. Hata siku moja hutasikia akitoa maelezo ya hao watu walifanya nini. Hata mikutano kama ilikuwepo haielezwi ilifanyika wapi na kilizungumzwa kitu gani kinachoonyesha kupigania uhuru!
Vikao vingi inaonyesha vilikuwa kama vya 'club' eneo la Kariakoo pekee, hakuna mahali pengine popote hao wanaotajwa katika historia hiyo walipafikia kwa lengo la kueneza habari za kutafuta uhuru.
Kiufupi, maelezo ya huyo mzee ni utapeli mtupu.
Anachoweza kujivunia ni ujuzi wake wa kupangilia mambo katika hali inayoweza kuvuta hisia za mwasomaji, hasa wale ambao akili zao tayari zimejiegemeza katika uamini wa anayoyasimulia.
 
Kalamu
Jibu la ile hoja yako ambayo niliikazia kwenye #131 ndio hili..

Swali la ziada mzee wangu..
Kulikuwa kuna haja gani nakuambatanisha na kauli ya askofu wakati ni vitu viwili tofauti?!
Hawezi kuwa na jibu la hoja hiyo, kwa sababu nia ya maelezo yake haikulenga kabisa kilichosemwa na yule askofu. Yeye alikuwa na lengo tofauti kabisa; lengo la kusambaza yale anayo yapigania maisha yake yote.
 
Ukiacha suala la historia yake na wazee wake..
Ameshindwa kujibu hiyo historia kwanini ameihusisha na tamko la askofu.
Pamoja na ukongwe wake wa papers hana hoja ktk hilo.
Ukimbana anakuchanganya kwakukujazia majina mengi yakipwani mara said mpunga etc🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…