Alichofanyiwa Zitto ndani ya CHADEMA: Akili ndogo inatawala akili kubwa

Alichofanyiwa Zitto ndani ya CHADEMA: Akili ndogo inatawala akili kubwa

images

Kuvuliwa vyeo kwa Zitto Zuberi Kabwe na Dr Kitila Mkumbo kutakuwa na visingio vingi, ukweli ni kwamba
​
"NDANI YA CHADEMA AKILI NDOGO INATAWALA AKILI KUBWA" It is natural kwamba akili ndogo ikitawala akili kubwa,
1) Yatatumika mabavu na nguvu nyingi kuizuia akili kubwa kupanda juu,
2) Zitatafutwa sababu nyingi na visingizio uchwara kuhalalisha kuizima akili kubwa tofauti na vigezo vya hoja kwakuwa akili ndogo haiwezi kuizidi akili kubwa kwa hoja,
3) Hutumika vitisho vingi kuzuia akili kubwa kuchukua hadhi yake
4) Akili ndogo ni rafiki wa akili ndogo mwenzake, hivyo akili ndogo huzungukwa na akili ndogo kwakuwa ushauri wa akili kubwa akili ndogo hushindwa kutumia ama kushindwa kuonesha umiliki mbele za watu. Kwenye chadema wenye akili wote wako nje ya uzio wa chemichemi ya mawazo.

Pale bungeni watu wanaoweza kufundisha na waliokuwa wakifundisha hata unaibu waziri kivuli hawapati kwakuwa wanatumia akili zaidi badala ya nguvu.

Lakini walioishia kidato cha kwanza, pili, tatu na zero ndio think tanks na ndio majembe ya chadema kwakuwa wanatumia mabavu na manguvu zaidi kuliko akili sawasawa na matakwa mahitaji ya akili ndogo inayoongoza akili kubwa.

Vijana wahitimu wa vyuo wanaopenda siasa waliandikiwa barua kuwazuia kuhutubia mkutano wowote wa hadhara sawasawa na matakwa ya akili ndogo inapotawala akili kubwa. Zito, Kitila, Christowaja, Matiko, Opulukwa, Baregu, Leticia, Selasini, Arfi, Akunay, Naste wengi wao MA holders kwa chadema ni rejects. Ukiwa mwanafamilia au ukoo au kazi au wito maalum wa viongozi ndio utakwepo kwenye list.

I know Zitto tangu tukiwa chuoni, he is a brilliant and consistent politician, namjua Dr Kitila tangu chuoni, he is resourceful. Hivi kosa walilofanya ni kubwa kuliko mchango wao waliofanya kwenye kuwajenga watanzania kuwaamini vijana kwenye siasa? Je kosa lao ni kubwa kuliko mchango wao unavyohitajika? Vijana tuko kazini na wakati huohuo tuko mafunzoni.

Sio adhabu nzuri ya kuwafukuza ama kuwaondoa kwenye fursa ya kujifunza zaidi.
Haya ndio madhara ya AKILI NDOGO KUTAWALA AKILI KUBWA, HOFU NDIO HUTAWALA

MN hakika ufalme wa mbinguni ni wako,maana umetengua kauli ya wahenga isemayo adui muombee njaa,leo adui umemuombea shibe.
Hopeless moving figure
 
Nchemba nyie magamba hamthubutu kufanya maamuzi hayo maana wengi ndani ya sisimu si wasafi na kibaya zaidi wachumia tumbo ni wengi. Akina mwampamba na masalia wenzie walipotimuliwa mlitoa povu hivihivi na utetezi wa kipuuzi.
kazi ni moja tu katiba ya chama chao ichukue mkondo bila kuangalia sura wala kujali ukwasi
Mwisho mfikishie wassira pole kwa mkakati wake wa kukiua cdm kushindwa
 
Mbona mwenyekiti wako ni akili ndogo na anaongoza mpaka maprofesa. Kwa hiyo unamdhalilisha mwenyekiti wako! Na ule udocta wake feki!!!!!!!!!!!

At least yeye ana BA Economics kutoka UDSM pia ni Luteni Kanali wa Jeshi. Weka CV za Mbowe hapa tuzione. Mbowe ni akili ndogo kweli
 
images

Kuvuliwa vyeo kwa Zitto Zuberi Kabwe na Dr Kitila Mkumbo kutakuwa na visingio vingi, ukweli ni kwamba
​
"NDANI YA CHADEMA AKILI NDOGO INATAWALA AKILI KUBWA" It is natural kwamba akili ndogo ikitawala akili kubwa,
1) Yatatumika mabavu na nguvu nyingi kuizuia akili kubwa kupanda juu,
2) Zitatafutwa sababu nyingi na visingizio uchwara kuhalalisha kuizima akili kubwa tofauti na vigezo vya hoja kwakuwa akili ndogo haiwezi kuizidi akili kubwa kwa hoja,
3) Hutumika vitisho vingi kuzuia akili kubwa kuchukua hadhi yake
4) Akili ndogo ni rafiki wa akili ndogo mwenzake, hivyo akili ndogo huzungukwa na akili ndogo kwakuwa ushauri wa akili kubwa akili ndogo hushindwa kutumia ama kushindwa kuonesha umiliki mbele za watu. Kwenye chadema wenye akili wote wako nje ya uzio wa chemichemi ya mawazo.

Pale bungeni watu wanaoweza kufundisha na waliokuwa wakifundisha hata unaibu waziri kivuli hawapati kwakuwa wanatumia akili zaidi badala ya nguvu.

Lakini walioishia kidato cha kwanza, pili, tatu na zero ndio think tanks na ndio majembe ya chadema kwakuwa wanatumia mabavu na manguvu zaidi kuliko akili sawasawa na matakwa mahitaji ya akili ndogo inayoongoza akili kubwa.

Vijana wahitimu wa vyuo wanaopenda siasa waliandikiwa barua kuwazuia kuhutubia mkutano wowote wa hadhara sawasawa na matakwa ya akili ndogo inapotawala akili kubwa. Zito, Kitila, Christowaja, Matiko, Opulukwa, Baregu, Leticia, Selasini, Arfi, Akunay, Naste wengi wao MA holders kwa chadema ni rejects. Ukiwa mwanafamilia au ukoo au kazi au wito maalum wa viongozi ndio utakwepo kwenye list.

I know Zitto tangu tukiwa chuoni, he is a brilliant and consistent politician, namjua Dr Kitila tangu chuoni, he is resourceful. Hivi kosa walilofanya ni kubwa kuliko mchango wao waliofanya kwenye kuwajenga watanzania kuwaamini vijana kwenye siasa? Je kosa lao ni kubwa kuliko mchango wao unavyohitajika? Vijana tuko kazini na wakati huohuo tuko mafunzoni.

Sio adhabu nzuri ya kuwafukuza ama kuwaondoa kwenye fursa ya kujifunza zaidi.
Haya ndio madhara ya AKILI NDOGO KUTAWALA AKILI KUBWA, HOFU NDIO HUTAWALA

Mwigulu una tatizo la akili nakushauri uwahi Mirembe Hospital haraka! na kama akili zako ziko sawa ebu jibu hii kwanza;

Subject: Fw: kazi nzuri
Date: Sunday, November 17, 2013 20:28
From: " Mwigulu Nchemba " <[email protected]> >
To: “Emmanuel Nchimbi” < [email protected] >

On Sunday, November 17, 2013 6:15:44 PM, Mwigulu Nchemba <[email protected]> wrote:

sawa boss,,jumatano saa moja imekaa safi kabisa. tuchape kazi. ntakupa update nikitoka kuonana na zzk. mh. Lukuvi namtafuta punde

MN

2013/11/17 Emmanuel Nchimbi < [email protected] >

bila shaka vijana wamefanya kazi nzuri sana. mapambano yanaendelea, hakuna kulala, hapa sasa tume lote livunjwe na huyo waryoba apumzishwe. mtafute mh. Lukuvi ana mazuri ya kuongea na wewe. kuna mapya pale ufipa, nimeshaongea na mh. zitto na amenipa brifieing .. tukutane jumatano basi jioni ya saa1 pale pale cheer,, Emma

Sent from my ipad

On Sunday, November 17, 2013 5:55:02 PM, Mwigulu Nchemba <[email protected]> wrote:

Naona vijana wametekeleza shuguli vizuri, na cham imewakilishwa vizuri sana. Msangi jembe, sasa tutaipata katiba tunayoitaka hicho kikwazo kikishaondolewa bila shuruti. Alafu upande wa pili (cdm) inabidi tuongeze dau ili shujaa zzk abakie ndani, nasikia kuna mkakati wa kumtoa kwenye kinyang'anyiro. tujitahidi sana sana kumsaidia kujenga mtandao wa ndani apate u wenyekiti. taarifa zaidi za ndani zinasema wkamba wanajaribu kumfukuza kabla ya mwisho wa mwaka, tuendeleze vita hilo lisitokee, naona kundi ndani ya bavicha hasa hiyo mitoto inafanya sana mashambulizi lakini hawataweza. inabidi wadhibitiwe. rockup wiki mbili itawasambaratisha. Tuongeze kasi kwa wajumbe wa kamati kuu. wengi wao ni njaa sana nazani 5mil kila moja inatosha kabisa.wananifata sana kuomba hela ili wasaidie nakutana na ZZK baadae plae pa siku ile, unaweza kufika saa 1 jioni

MN
 
Hata kama mods hamuweki post zangu lakini mnapata jumbe hizi.MH ZITO kemea wanaccm waache ushabiki juu yako kwani wanatengeneza ushahidi wa kwamba wewe ni mamluki ndani ya Chadema.MPINZANI WA KWELI ATAONEKANA KWA WATU AU WAFUASI WAKE SI WAPINZANI WAKE.
 
Angekubali kuitwa john badala ya zuberi mambo huenda yangemuendea vizuri.
 
Mara kadhaa nimekuwa nikimwandikia Zitto kumuuliza hivi ni kwanini kila siku yeye tu? Kwanini asisemwe mtu mwingine?

Siku zote Zitto amekuwa akijitetea kwamba hahusiki na wala hajui chochote kuhusu hayo yanayosemwa juu yake. Lakini katika hali ya kushangaza, tangu CHADEMA ifanye maamuzi magumu ya kuwavua vyeo Zitto na Kitila, wanaCCM ndiyo wameonekana kuwa na uchungu zaidi na maamuzi haya. Hata Mwigulu Nchemba ambaye tumekuwa tukimjua kama mpinga CHADEMA kwa kila hali, ameanza kuropoka kama mwehu akipinga kitendo kilichofanywa na CHADEMA.

Hivi kama CHADEMA wamefanya maamuzi mabaya, yenye madhara kwa chama, ni kwanini wanaCCM wasishangilie kwa kuamini kwamba CHADEMA itadhoofika, na hatimaye wao waendelee kushika dola? Ni kwa vipi, tuanze kuona akina Ridhiwani wakiibuka na kuponda maamuzi haya, kana kwamba wanaitakia mema CHADEMA? Na kwanini Pro CCM wote wa hapa Jamiiforums nao wameungana na wanaLumumba kushambulia maamuzi ya CHADEMA? Kwa hiki tu, yafaa tujifunze jambo hapa.

CCM wamepata mshituko baada ya kuona kwamba wale waliokuwa wanawatumia katika kukiumiza chama hawatatumika tena. Kama wanaCHADEMA hatutamtetea yeyote kati ya hawa waliofukuzwa kwa kuwa ushahidi upo dhahiri kwamba walikuwa ni wahaini. Mtu kama Zitto alitajwa waziwazi na Ben Saanane kuwa ni engineer wa uasi ndani ya chama. Kama Zitto alijua amesingiziwa kwanini hakumshitaki Ben mahakamani au hata chamani? Zitto anajua alichokuwa anakifanya!

Zitto alitishia kupeleka mahakamani vifaranga na mama zao wanoeneza uongo juu yake na hasa baada ya kuvuja kwa ile report ya siri. Lakini mwisho wa siku Zitto kaenda polisi kuomba ulinzi badala ya kupeleka kesi mahakamani. Si awe mkweli tu?

Naipongeza kamati kuu ya CHADEMA kwa maamuzi haya makubwa na magumu.
 
Last edited by a moderator:
Huo ni ushauri mzuri. Image yake imechafuka kabisa baada ya CCM kulivalia njuga suala lake na ukichanganya na waraka wa siri kuhusu uhusiano wa Zito na CCM na email za mawasiliano kati ya nchimbi na mwigulu anaeamini kuwa Zito ameonewa atakuwa kichaa tu.
 
Watu mna maswali ya kipuuzi, mbona ya CCM huwa yanawagusa Chadema hadi mnaitisha press conference na mikutano ya hadhara. Kwa mawazo yako unataka kujustify usaliti wa Zitto kwa kutumia comments za CCM? Huo ni upuuzi na pengine ndio maana mmemuhukumu Zitto na Kitila kwa nyaraka za kusadikika.
 
Naunga hoja mkuu. Mbona wanaccm wameumia sana hata magazeti mengi vbaraka wanaponda maamzi ya CDM.
 
Zzk ni sikio la kufa,halina dawa,ukizoea kula nyama ya binadamu, utaendelea tu, ndivyo alivyo yeye na kizazi chake cha akina kafulila
 
Mkuu hili liko wazi kama umeona mawasiliano kati ya Mwigulu na Nchimbi. Zito amevuna alichopanda.
 
Watu mna maswali ya kipuuzi, mbona ya CCM huwa yanawagusa Chadema hadi mnaitisha press conference na mikutano ya hadhara. Kwa mawazo yako unataka kujustify usaliti wa Zitto kwa kutumia comments za CCM? Huo ni upuuzi na pengine ndio maana mmemuhukumu Zitto na Kitila kwa nyaraka za kusadikika.

Hebu tujuze mfano wa yalitokea CCM na CHADEMA wakawa wanahangaika Kama CCM tunavyofanya now.
 
Zzk ni sikio la kufa,halina dawa,ukizoea kula nyama ya binadamu, utaendelea tu, ndivyo alivyo yeye na kizazi chake cha akina kafulila

Kwa sababu ndani ya suala hili itafika maamuzi ya wanachadema tu,hata pilato akisema haoni kosa kwake,wanachadema watasema kwetu sisi analo kosa hivyo asulubiwe tu,kisa anashangiliwa na mahasimu
 
Watu mna maswali ya kipuuzi, mbona ya CCM huwa yanawagusa Chadema hadi mnaitisha press conference na mikutano ya hadhara. Kwa mawazo yako unataka kujustify usaliti wa Zitto kwa kutumia comments za CCM? Huo ni upuuzi na pengine ndio maana mmemuhukumu Zitto na Kitila kwa nyaraka za kusadikika.
Ni maamuzi gani magumu yaliyowahi kufanywa na CCM yakawafanya CHADEMA waitishe press conference? Au ni kushindwa kwa mpango wa kujivua gamba? CCM haijawahi kufanya maamuzi magumu ya kuikuna CHADEMA. Mlimfukuza uanachama yule mbunge wenu wa Zanzibar na hakuna mwanaCHADEMA hata mmoja alianzisha hata thread kulijadili hilo. Hakuna jambo kubwa la CCM la kuifanya CHADEMA iitishe press conference.
Kwamba tunajenga justification ya usaliti wa Zitto kwa kutumia nyaraka za kusadikika hilo halina manitiki. Ikumbukwe kwamba hukumu ile ilitolewa huku Zitto na Kitila mwenyewe, wakiwa ndani ya Kikao. Na gazeti la mwananchi limeeleza kwamba Kitila alikiri kuhusika na waraka uliokutwa kwenye laptop ya Mwigamba. Sasa wewe una hoja gani nyingine ya kumtetea Zitto?

Kwa mujibu wa waraka wenyewe, "Mkakati huu umeandaliwa kwa pamoja na M2 na M3 na kupitiwa na kurekebishwa na M1 ili upelekwe kwa MM kwa maoni ya mwisho na kuanza utekelezaji." Mbele ya Kamati Kuu, Dk. Mkumbo alikiri kwamba MM au Mhusika Mkuu ni Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe; M1 ni yeye mwenyewe Dk. Mkumbo na M3 ni Bwana Mwigamba. Dk. Mkumbo alikataa kata kata kumfahamu M2. Aidha, Dk. Mkumbo alikiri mbele ya Kamati Kuu kwamba yote yaliyoandikwa katika &#8216;Mkakati wa Mabadiliko 2013' yametoka kwenye &#8216;Mtandao wa Ushindi' na hayajabadilishwa.
 
Issue ya ZZK itapita kama moto wa mabuwa,safari yako kisiasa imeishia hapo,utajadiliwa leo na kesho hapa jf baada ya hapo kwishiney watakuwa wameshamaliza mazishi yako.CCM waliokuwa wanakutumia wamekufikisha hapo walipokuwa wanataka na wewe bila akili ukakubaliana nao,sasa furaha ya CCM IMEKAMILIKA,walikuwa wanakuogopa ndiyo maana wakakutega kwa pesa na wewe ukaingia kwenye mtego bila ajizi wmekunasa vilivyo,polee.
 
mambo ya ajabu sana haya nilitegemea Wanachadema wangekuwa wanaandamana wakipinga kuwavua uongozi watu walio kuwa wachapa kazi njema

ajabu kijani ndiyo wanaandaa mabango tunajiuliza kulikuwa na nini nyuma ya pazia hadi mpinzani anakasirika safu ya mashambulizi inapopanguliwa !
 
Back
Top Bottom