Alichokifanya P Diddy iwe Funzo Kwa Vijana Wengine Wapenda Kitonga

Alichokifanya P Diddy iwe Funzo Kwa Vijana Wengine Wapenda Kitonga

Mtu unaweza ukajiona unaandika kitu cha maana kumbe unaandika ufala tu. P didy alichofanya ni makosa, na hata wanaomfikia ni wapambanaji. Hivi kumgikia didy ni kitonga??? Unafikiri ni rahisi hivyo???

Watu wowote waliofanikiwa kimaisha kuna moments lazima mtu atafute networking na connection ni jambo la kawaida. Si kosa wala sio kuoends kitonga kuonana na huyo didy.

Pointi ni kwamba mpaka kumfikia huyo didy tayari mtu kapambana
Nonsense
 
Nafikiri umeamua kupotosha umma, ungeuliza ni sababu ipi inayowafanya wakae na kusimama mbele beach.

Unafikiri beach za hapa Zanzibar unajiendea halafu unakaa mbele na kutaka kuongea na mzungu?? Kuna utaratibu maalumu lazima uufuate.

Kama umeamua kutafuta kipato chako na kunufaika kwa kupitia ufukwe wa bahari (beach) kwa hapa Zanzibar wana taratibu zao. Namaanisha wafanyabiashara wadogo, beach boys na beach girls.

Hawa beach boys na beach girls malengo ya makuu ni kutafuta wanawake wa kizungu (beach boys) pamoja na wanaume wa kizungu (beach girls).

Kwa uzoefu wangu, wote beach boys na beach girls wanawapenda zaidi vibibi na vibabu vya kizungu na siyo vijana! Sababu?? Hawa wana hela kuliko vijana na akikukubali umetoboa!

Vijana karibu wote wakiwemo wamasai wametoboa kupitia vibabu na vibibi vya kizungu! Wengi wao wamepata maendeleo makubwa kupitia hawa! Hawa vijana wa kizungu ni just for fun na kubuy time!

Mchakato ni huu:

1) Usajili: Beach zote kubwa kama vile Nungwi, Paje, Kiwengwa n.k huwezi kufanya ubeach boy au ubeach girl lazima ujisajili kwanza! Mfano beach boy wa Nungwi hawezi kufanya kazi kwenye beach ya Paje! Je, itakuwa kutoka bara??

2) Ada: Hapa kila beach ina utaratibu wake na kiwango cha kulipa kwa kila mhusika!

3) Utambulisho: Hapa ni lazima ujulikane wewe ni nani na makazi yako, zamani walikuwa na vitambulisho ingawaje sivioni na wanasema wote wanajuana na huo ndiyo ukweli!

4) Ulinzi: Hapa kuna kamati yao ya ulinzi wakishirikiana na serikali, walionywa tukio lolote baya lilikimkuta mtalii kwenye beach yoyote siyo nje ya beach basi watawajibika!

Utaratibu wa kufanya kazi:

Kwa uzoefu wangu , mara nyingi huwa ni wiki kwa wiki, yani group moja wikii hii na group lingine ni wiki inayofuata.

Kukaa, kusimama na kuchuchumaa mbele ya hoteli au vila, hapa huchorwa mstari kama mpaka mara nyingi na wamiliki wa hoteli ili kuondoa usumbufu kwa wageni wao!

Mara nyingi hasa wakati wa mchana na jioni ndiyo nafasi ya kuonana na mgeni hupatikana coz ndiyo muda wa kuoga na kutembea ufukweni !

Mazingira ya kazi:

Kama kazi yoyote ile , hii nayo kazi haikosi changamoto mfano kusimama, kuchuchumaa na kukaa kwa muda mrefu halafu unasubiria mtu asiye kufahamu mbaya zaidi hakujui! Kujito akili ndiyo mpango mzima!

Kuoneana wivu, wamasai wamefanikwa kuwateka watalii wengi hasa kupitia mavazi yao ingawaje umbeya na unafiki umewasaidia! Kivipi??

Kama umefanikwa kutembelea huko umasaini hawa jamaa wana ubaguzi mkubwa kwa watu wa makabila mengine wenyewe huwaita waswahili! Ubaguzi ni tabia na mara nyingi anayebaguliwa ndiye anayeumia!

Sasa kinachofanyika ni hivi: Mfano umempata mgeni umekubaliana naye kuwa jioni utaenda sehemu fulani kupata chakula na kinywaji kwa gharama nafuu bia moja ni dola 5, kuku dola 10 (mtu mmoja) hizi labda mko wawili maana yake ni dola 30!

Beach boys hucheza deal na wenye migahawa na mabaa huku juu siyo ufukweni, dola 30 inakaribia laki wakati bia moja ni 3500 kuku ni 7000 maana yake 40000 haishi kwa watu wawili!

Mzungu atalipa ile dola 30 na kusindikizwa na beach boy kisha atarudi kwenye bar atachukua chake! Wamasai wakakisanua!

Akiona mzungu amemalizana na mswahili humfuata baadaye na kumuambia ya ukweli! Mfano gharama zote ni dola 15! Mzungu ataacha kukupenda??Ule ugomvi kipindi kile kuwa wamasai waondoke sababu kuu ni hii maslahi!

Nb: Ushoga ni tabia ya mtu mwenyewe na kwa kutaka mwenyewe na hulazimishwi! Kosa la mtu mmoja lisihesabike kama ni la jamii nzima!

Samahani kwa gazeti nimezungumzia kwa uzoefu wangu!
Wamasai wanatumia madawa kuvipata ivo vibibi, simple.

Af sio Vizuri mwanaume kushobokashoboka ndo ufanikiwe kimaisha izo ni Red Flags, Hustle Kiume.!!
 
Back
Top Bottom