chabuso,
..tukirudi kwenye suala la UN. wewe siyo Mzanzibari wa kwanza kudai kwamba Tanganyika haikupata kuwa mwanachama wa UN. where did you get that information from?? nchi yoyote ile inapopata uhuru wake basi haichukui muda kuandikishwa uanachama UN.
..mimi nina swali moja kwako. je, unamfahamu Balozi wa Zanzibar UN baada ya mapinduzi na kabla ya muungano?? mabalozi wa Tanganyika kipindi hicho walikuwa ni Chief Mang'enya[Jan 1963 - June 1964] na John Malecela [Nov 1964 - March 1968]. Sasa kumbuka kwamba TANZANIA[tgk + znz] uanachama wake UN ulianza Nov 1, 1964.
..zaidi, kwanini mnazungumzia uanachama wa UN tu? kwanini hamzungumzii uanachama wa Tanganyika na Zanzibar ktk OAU?? kwa uelewa wangu by 1964, Tanganyika ilikuwa ina nafasi na heshima kubwa sana ktk OAU. kama sijakosea tayari tulishapewa dhamana ya kuwa mwenyekiti wa kamati ya ukombozi wa kusini mwa Afrika ya OAU. sasa ndiyo maana wakati mwingine nashangazwa kidogo na madai ya baadhi ya wa-Zanzibar kwamba kabla ya muungano, Tanganyika ilikuwa haijulikani pahali popote.
..jambo lingine umeligusia kuhusu Jamshid kukimbilia Uingereza badala ya Oman. sina uhakika, lakini inawezekana sababu kubwa ni kwamba mwaka 1964, Oman ilikuwa choka mbaya. nadhani hazina ya mafuta iligunduliwa miaka ya 70.
cc:
Nguruvi3,
GHIBUU,
Barubaru,
Nonda