Alichokisema Rais Magufuli Tabora ni kweli; majungu watu hawafanyi kazi. Kanisa lajengwa katikati ya barabara, lapiga muziki masaa 24

Alichokisema Rais Magufuli Tabora ni kweli; majungu watu hawafanyi kazi. Kanisa lajengwa katikati ya barabara, lapiga muziki masaa 24

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2019
Posts
7,567
Reaction score
9,037
Nikiwa Tabora ambapo nilikwenda kwenye msiba wa rafiki yangu aliyefiwa na mama yake mwezi huu. Nilikutana na kituko cha mwaka ambapo tukiwa hapo msibani ulisikika muziki mkubwa sana kiasi ambacho huwezi kuongea na mtu jirani yako, huwezi kupokea simu au kusikiliza simu. Nilipouliza nikaambiwa hilo ni kanisa la walokole Bethel, ambao walifukuzwa kutoka kata ya cheyo ndio wamehamia Kariakoo Tabora kata ya Kitete, ambapo toka wahamie Muziki ni masaa 24 kwa sauti ya juu sana.

Wakazi wa eneo hilo licha ya kulalamika kwa mkuu wa wilaya kwa maandishi DC Komanya, mkurugenzi, mtendaji kata, mwenyekiti wa mtaa, polisi mkuu wa kituo Mmassy, OCD, bado kanisa hilo linaendelea na fujo, vurugu huku mchungaji wa kanisa hilo Mch Jackson akiwambia wakazi hao kuwa serikali yote ya mkoa ameiweka mfukoni.

Mbaya zaidi huyo kaamua kujenga katikati ya barabara na kuziba barabara mtaa hivyo hapapitiki kwa gari, huwezi kupitisha mgonjwa, maiti hata kwa matumizi ya kawaida.

Jirani na kariakoo Ni eneo la Tukutuku ambapo nyumba zaidi ya Mia zilivunjwa kwa kujengwa maeneo yasiyoruhusiwa na bila kibali cha manispaa. Kanisa hilo linajengwa katikati ya barabara bila kibali? Au ndio afisa mipango miji katoa kibali Cha kujenga katikati ya barabara be? Haya yanafanyika huku Mkuu wa Mkoa yupo, Mkuu wa Wilaya yupo, Mkurugenzi yupo, Afisa Mipango Miji yupo na taarifa za malalamiko wanazo au ndiyo ukweli wa maneno ya rais Magufuri kuwa Tabora wamekalia majungu hawafanyi kazi?

NB: Kanisa na nyumba ya mchungaji vimejengwa kuziba barabara. Muziki mkubwa kanisani waliomo ndani sasa hata kumi hawafikiriki.

IMG_20210213_095217_6.jpg
 
Kwa kweli imani zingine ni kero wengine sijui ni ulimbukenii,naamini ibada ina mda wake,sio unafungulia mziki Kwa sauti Kwa ajili ya kuwasikilizisha wengine, bila kujali kuna wagonjwa n.k
 
Kwa kweli imani zingine ni kero wengine sijui ni ulimbukenii,naamini ibada ina mda wake,sio unafungulia mziki Kwa sauti Kwa ajili ya kuwasikilizisha wengine,bila kujali kuna wagonjwa n.k
Muda wa ibada ni upi?
 
Jumapili ndio kivumbi na jasho wanaanza muziki was hatari saa moja asubuhi mpaka saa kumi na moja nonstop .
Hao watakuwa wahuni. Kama ibada yao inakera wananchi inabidi wahamishwe hilo eneo. Poleni sana
 
Hao watakuwa wahuni. Kama ibada yao inakera wananchi inabidi wahamishwe hilo eneo. Poleni sana
Mkuu inaonekana sijui wanalindwa na nani maana barua ilishaenda kwa mkuu wa wilaya na nyingine kwa mkurugenzi nimeiatach hapo hawachukui hatua yoyote , ingawa walipokuwa zamani kata ya cheyo walifukuzwa kwa tabia hii hii.
 
ROHO MTAKATIFU anawalinda, najua hapa Tabora watoto wa ma'mdogo hawapendi makanisa ila wokovu ndio umefika sasa!
 
Kwa kweli imani zingine ni kero wengine sijui ni ulimbukenii,naamini ibada ina mda wake,sio unafungulia mziki Kwa sauti Kwa ajili ya kuwasikilizisha wengine,bila kujali kuna wagonjwa n.k
Mkuu wakazi wa hapa wameshapeleka malalamiko kila sehemu , DC , DED , OCD ,OCS Mmassy , Mtendaji Kata , Mwenyekiti wa mtaa , kote hakuna hatua zinazochukuliwa , wananchi wamechoka sana wanasema mwishoni watajichukulia sheria mkononi .
 
devil kazini, sijawahi kusikia kuhusu BAA ZILIZOJENGWA KIL MTAA, kupiga live band usiku kucha kwakuwa ni shetani wenzako hulalamiki ila mambo ya Mungu unalalamika. SHETANI YUPO KAZINI HAPENDI KAZI ZA MUNGU
Miye nimeshawahi kusikia wakilalamika kuhusu bar kujengwa ktk makazi ya watu. Hoja hapo ni kanisa kujengwa ktk makazi ya watu na kutodhibiti mziki wake hadi kuwasikilizisha kwa lazma watu. Huyo Mungu gani ktk biblia aliruhusu muziki kupigwa ktk mahekalu na masinagogi masaa 24!!
 
Sijawahi kusikia kuhusu BAA ZILIZOJENGWA KIL MTAA, kupiga live band usiku kucha kwakuwa ni shetani wenzako hulalamiki ila mambo ya Mungu unalalamika. SHETANI YUPO KAZINI HAPENDI KAZI ZA MUNGU
Maneno ya Yesu Kristu haya 6:5 Mathayo naona muna mlokole uchwara kablock isionekane vizuri hapa , tumfuate yeye au wewe

IMG_20210213_113031_8.jpg
 
Wewe nenda kamalizie uzi wako ulioutelekeza kule jukwaa la hoja mchanganyiko , kusema watu wamejenga katikati ya barabara Ni majungu? Bila kibali ? Makanisa yote yanamaelekezo Kama kibali Chao kilivyo a na afisa utamaduni hujui? Chizi kweli wewe .
Mnaendekeza sana Majungu. Hapo unaisgi KANYENYE AU BACHU? NYIE MNA MAJUNGU SANA
 
Wewe nenda kamalizie uzi wako ulioutelekeza kule jukwaa la hoja mchanganyiko , kusema watu wamejenga katikati ya barabara Ni majungu? Bila kibali ? Makanisa yote yanamaelekezo Kama kibali Chao kilivyo tolewa na afisa utamaduni hujui ? Chizi kweli wewe .
Unataka nikamalizie waniue kwa ugonjwa?
 
Wewe nenda kamalizie uzi wako ulioutelekeza kule jukwaa la hoja mchanganyiko , kusema watu wamejenga katikati ya barabara Ni majungu? Bila kibali ? Makanisa yote yanamaelekezo Kama kibali Chao kilivyo tolewa na afisa utamaduni hujui ? Chizi kweli wewe .

Kwa nn hayo maeneo nyumba zilibomolewa... Na imekuwaje watu kuruhusiwa kujengwa Tena?
 
Back
Top Bottom