Alichokisema Rais Magufuli Tabora ni kweli; majungu watu hawafanyi kazi. Kanisa lajengwa katikati ya barabara, lapiga muziki masaa 24

Mkuu wakazi wa hapa wameshapeleka malalamiko kila sehemu , DC , DED , OCD ,OCS Mmassy , Mtendaji Kata , Mwenyekiti wa mtaa , kote hakuna hatua zinazochukuliwa , wananchi wamechoka sana wanasema mwishoni watajichukulia sheria mkononi .
Magu alisema korona imeondolewa Tz kwa maombi, sasa wewe unataka kanisa lifungwe ili korona irudi?
 
Wewe nenda kamalizie uzi wako ulioutelekeza kule jukwaa la hoja mchanganyiko , kusema watu wamejenga katikati ya barabara Ni majungu? Bila kibali ? Makanisa yote yanamaelekezo Kama kibali Chao kilivyo tolewa na afisa utamaduni hujui ? Chizi kweli wewe .
Hilo sio kosa la kanisa, ni kosa la halmashauri na TARURA.
 
Unataka nikamalizie waniue kwa ugonjwa?
Hawakuui utaambewa na walokole uchwara Kama wale waliofyeka msitu wa nyumba nitu wakakiona Cha moto
Magu alisema korona imeondolewa Tz kwa maombi, sasa wewe unataka kanisa lifungwe ili korona irudi?
Bosi wako kaishachanja chanjo ya Corona kawapa na watu wake wa karibu na wewe amekupa?.
 
Kwa kweli imani zingine ni kero wengine sijui ni ulimbukenii,naamini ibada ina mda wake,sio unafungulia mziki Kwa sauti Kwa ajili ya kuwasikilizisha wengine,bila kujali kuna wagonjwa n.k
Nipeni laki moja tuu nawaletea mizinga 2 ya nyuki wakalii naiweka hapo kanisani kwao....
 
Nikiwa Tabora ambapo nilikwenda kwenye msiba wa rafiki yangu aliyefiwa na mama yake mwezi huu. Nilikutana na kituko cha mwaka ambapo tukiwa hapo msibani ulisikika muziki mkubwa sana kiasi ambacho huwezi kuongea na mtu jirani yako, huwezi kupokea simu au kusikiliza simu. Nilipouliza nikaambiwa hilo ni kanisa la walokole Bethel, ambao walifukuzwa kutoka kata ya cheyo ndio wamehamia Kariakoo Tabora kata ya Kitete, ambapo toka wahamie Muziki ni masaa 24 kwa sauti ya juu sana.

Wakazi wa eneo hilo licha ya kulalamika kwa mkuu wa wilaya kwa maandishi DC Komanya, mkurugenzi, mtendaji kata, mwenyekiti wa mtaa, polisi mkuu wa kituo Mmassy, OCD, bado kanisa hilo linaendelea na fujo, vurugu huku mchungaji wa kanisa hilo Mch Jackson akiwambia wakazi hao kuwa serikali yote ya mkoa ameiweka mfukoni.

Mbaya zaidi huyo kaamua kujenga katikati ya barabara na kuziba barabara mtaa hivyo hapapitiki kwa gari, huwezi kupitisha mgonjwa, maiti hata kwa matumizi ya kawaida.

Jirani na kariakoo Ni eneo la Tukutuku ambapo nyumba zaidi ya Mia zilivunjwa kwa kujengwa maeneo yasiyoruhusiwa na bila kibali cha manispaa. Kanisa hilo linajengwa katikati ya barabara bila kibali? Au ndio afisa mipango miji katoa kibali Cha kujenga katikati ya barabara be? Haya yanafanyika huku Mkuu wa Mkoa yupo, Mkuu wa Wilaya yupo, Mkurugenzi yupo, Afisa Mipango Miji yupo na taarifa za malalamiko wanazo au ndiyo ukweli wa maneno ya rais Magufuri kuwa Tabora wamekalia majungu hawafanyi kazi?

NB: Kanisa na nyumba ya mchungaji vimejengwa kuziba barabara. Muziki mkubwa kanisani waliomo ndani sasa hata kumi hawafikiriki.
Hapo naona nyumba 2 na gofu moja hilo kanisa liko wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Achana na kanisa wewe, mbona bar zikifunguliwa hamlalamiki ?

Rais alisema kweli kwamba Tabora majungu ndio kwao. Ona sasa mtoa post unatuletea majungu yako hapa. Peleka huko. Fyuuuuuuu.
 
MLETA MADA NDO MKAZI HALISI WA TABORA. MAJUNGU,WIVU,CHUKI NA FITNA NDO SIFA ZA WA ASILI YA TABORA. HATA RAIS ALISEMA NA JAMAA KAWAKILISHA NDUGU ZAKE KABISA KWA MAJUNGU.
 
Soma mada uelewe acha kukurupuka , Majungu ndio watu wajenge Katikati ya barabara ? Bila kibali ? Masharti ya kujenga nyumba za ibada unayafahamu sure unajisemea tu .
 
MLETA MADA NDO MKAZI HALISI WA TABORA. MAJUNGU,WIVU,CHUKI NA FITNA NDO SIFA ZA WA ASILI YA TABORA. HATA RAIS ALISEMA NA JAMAA KAWAKILISHA NDUGU ZAKE KABISA KWA MAJUNGU.
Umeshindwa kumaliza Uzi wako unadakis mengine , Kama unstaka watu wakuchangie sema au unahamia telegram ?
 
Tabora na manzese ni chupi na taiti, hawana tofauti na ni waswahilina sana, wakusamehe t hawa
Wewe na chizi mwenzio page moja imewashinda kuelewa mmeishia darasa la pili ? Tumia akili uelewe pointi hapo ni je sheria inaruhusu kujenga kanisa kwenye makazi ya watu ? Pili sheria inaruhusu kujenga katikati ya barabara ? Tatu wahusika wana kibali cha kubadili matumizi ya eneo husika ? Kumbuka hutolewa tangazo la miezi mitatu wakazi wa eneo husika waruhusu au watoe pingamiza , Nne kama kanisa lijijengwa kwenye makazi ya watu masharti yake ni yapi ? Tano sheria ina kiwango maalum cha sauti volume uliza TFMDA , Kama hujui kitu nyamaza unajiabisha , tumia hata akili za mbuzi kuvukia barabara kuelewa your an empty head tabulalasa kwelikweli .
 
Umeshindwa kumaliza Uzi wako unadakis mengine , Kama unstaka watu wakuchangie sema au unahamia telegram ?
Wanyamwezi mnapenda sana majungu. Rais alisema jambo hili. Ndo maana hamwendelei. Mnapenda sana majungu. Na wewe umeonesha mnavyopenda majungu.
 
Back
Top Bottom