Alichonifanyia huyu mama Ubungo stendi ya mabasi sio uungwana

Wema wake umemponzaje sasa? Kwani aliahidiwa malipo akimfikisha mtoto?
Jamaa anaona siyo ustaarabu mtu anakuletea mtoto halafu hata salamu yake hutaki siyo vizuri. Hakuna hasara yoyote kapata ila siyo ustaarabu kukataa hata salamu.
 
Next time usikubali kukabidhiwa mtoto. Unaweza pata Majanga makubwa maishani mwako. Wakambidhi kwa Kondakta
 
Walimwengu ndivyo tulivyo, ila tenda wema nenda zako
 
Hujaelewa, huyo aliomba wengi sasa hakuwa na uhakika ni nani kati yenu katuma hela.
Mimi ilinitokea mwaka Jana Dec, hawa jamaa huenda kuhesabiwa kule moshi sasa mama/dada mmoja nafahamiana nae nadhani siyo mwadilifu, akaomba nauli kurudi huku znz nikakaa kama siku 2 nikamtumia hela lakini nilituma moja kwa moja toka kwa wakala halafu nikakausha.
Alipofika znz akashindwa kuniuliza lakini Kuna siku nikamwambia najua kwanini ulikaa kimya nilipokutumia hela. Akapaniki ooh simu ooh jirani sijui.
Nikamchana kwamba hakujua nani kamtumia maana aliomba wengi! Akatuliia hadi leo hajaomba Tena hela kwangu maana ilikuwa kawaida yake ni single maza.
 
Waandikie gazeti wote uwape makavu live kubandeki zao,
Umenipa funzo hapa sibebi au chukua zigo la mtu yoyote
 
Nilivyo kisiran ningemchana palepalee shenzi kabisaaa
Pole ila usiache kutenda wemaa
 
Ungemla 0719
 
Hhahhaaa umenifurahisha sanaa mimi na kisa kama chako kidogo vinafanana mimi mwaka 2018 nilikuwa natokea ifakara nimepanda bus la KIDINILO upande wangu ulibaki seat moja tu akaangia Dada moja hivi kwakweli muonekano wake inaonekana huko alikotoka alikuwa amechukizwa na jambo kwa kawaida mimi nikishapanda bus nikimsalimia.abiria ndo bus no story hadi mwisho wa safari ila kale kadada kakawa kaninipigisha story nyingi mimi kimyaa mwisho nikaona konda anakaita wewe dada usipomaliza.nauli yangu nakushusha njiani khhhheee nilishangaa kumbe katoa nauli nusu kwa kuahidi.nyingine atatumiwa.lakini.konda akawa haoni dalili basiii bwana kaka anza kuniomba nikakopeshe kakitumiwa katanirudishia nauli nikaons usumbufu sasa nikakapa elfu 7 kamalizie nauli huwezi amini baada ya kushuka hata kushukuru na kuniaga kaliondoka kimye.kimyaaa nami nikaachana nako hadi sasa sipendi zoeana na mtu kwenye vyombo vya umma napokuwa safarini.
 
Wewe na wengine humu msije mkakubali kubebeshwa Mtu( awe mtoto, kijana au mzee) au Mzigo yatakuja yawakute mambo makubwa yaharibu maisha yenu,

Huyo Mama alipaswa amkabidhi Mtoto wake kwa Dereva wa Bus na sio wewe Abiria, mbaya zaidi Mtoto alikua anatapika tapika angezidiwa huyo ungekoma.
 
Mkuu hapa possibly aliomba hyo hela kwa watu wengi sasa hakujua yupi ametuma
 
Mwisho wa wema wako ni wewe na Mungu,sio wewe na wao,umefanya sehemu yako Mungu atakulipa achana nao,kiustaharabu ilitakiwa hata huyo wa mwanza akupigie yeye mwenyewe akushukuru sio wewe umpigie.
 
π•†π•Ÿπ•– π•‘π•£π•šπ•Ÿπ•”π•šπ•‘π•’π• 𝕠𝕗 π•π•šπ•—π•–: π”»π•’π•šπ•žπ•’ π•™π•šπ•€π•šπ•’ 𝕫𝕒 π•žπ•¨π•–π•Ÿπ•«π•’π•œπ•  π•¦π•€π•šπ•£π•¦π•™π•¦π•€π•¦ π•«π•šπ•œπ•’π•œπ•¦π• π•Ÿπ••π• π•π•–π•’ 𝕗𝕦𝕣𝕒𝕙𝕒.

π΄π‘β„Žπ‘Žπ‘›π‘Ž π‘›π‘Žπ‘œ, π‘’π‘›π‘‘π‘’π‘™π‘’π‘Ž π‘›π‘Ž 𝑙𝑖𝑓𝑒!

π΅π‘–π‘›π‘Žπ‘“π‘ π‘– π‘‡π‘Žπ‘›π‘”π‘’ π‘€π‘€π‘Žπ‘›π‘§π‘Ž π‘›π‘–π‘›π‘”π‘’π‘šπ‘˜π‘Žπ‘‘π‘Žπ‘Ž!
 
Pole Sana ndugu yangu Yani kusemaukweli, watu Wana roho mbaya Sana Ila usife moyo, Mwenyezi Mungu atakulipia.
 
Mtakuwa mmeombwa wengi...sasa mafile yamechangamana hajui ni yupi kati yenu katuma..ilikuwa sahihi kuuliza
 
Ndio maana watu wanawakataaga hao watoto wanaosafirishwa kama vifurushi.

Shukuru Mungu huyo mama alikua anakusumbua, wengine ni mikausho mikali hadi unafika hujui huyo mtoto umuweke wapi
 
Ndio maana watu wanawakataaga hao watoto wanaosafirishwa kama vifurushi.

Shukuru Mungu huyo mama alikua anakusumbua, wengine ni mikausho mikali hadi unafika hujui huyo mtoto umuweke wapi
🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…