Alichosimulia Edgar Mwakabela "Sativa" kuhusu waliomteka na kumpiga Risasi ya Kichwa

Jitafakarini sana kwenye system baadhi yenu mna roho mbaya sana. Tusiuane maana wote tutakufa tu kwa saa na wakati uliopangwa.

Tiss mnajiona mna mamlaka makubwa sana ya kutoa uhai wa watu acheni hizo bwana mida yetu ya kuishi hata kama utakaa sana ni ngumu kutoboa miaka 120.
Tuvumilianeni nchi yetu sote hii.
 
Kwanini polisi walisema hawajapokea mtu huyo kituoni na alifika kwenye karakana na kulala hapo?

Huyo kiongozi aliyefika na V8 na kupigiwa salute ndio mbeba maagizo ya huyu dogo kuuwawa au nae ni mleta maagizo? Na je ninani huyo?

Fanya yote ila kuwa makini na binadamu mwenzako ndio adui yako namba moja. Yan walimpeleka akwe kitoweo cha wanyamapori. SMH!! Gadamn
 
Eti MARANJA NA BONIPHACE wamekuwa tishio kwa watu flani ambao mimi ninawaona kuwa ni dhahifu.
Hizo posho na mafuta waliyotumia hao wa msafara si ni kodi zetu au ni ada za wanachama wao.
Watu ni waoga sana,hadi kina Maranja wanaogopwa kiasi hiki?
 
Kuteswa imeenza tangu dunia imeumbwa ndio maana hata Yesu aliteswa. Usifikiri imeanza wakati wa Mwamba Magufuli utakuwa unajidanganya na itaendelea hata baada ya Mama kutoka ni mawazo finyu tu kufikiri utesaji umeanza wakati wa Magufuli. Wamarekani wanaendelea kutesa watu huko Gwantanamol mpaka leo. Kitu muhimu tuache kutukana watu ovyo la sivyo tukubaliane na matokeo yake!
 
Eti MARANJA NA BONIPHACE wamekuwa tishio kwa watu flani ambao mimi ninawaona kuwa ni dhahifu.
Hizo posho na mafuta waliyotumia hao wa msafara si ni kodi zetu au ni ada za wanachama wao.
Watu ni waoga sana,hadi kina Maranja wanaogopwa kiasi hiki?
Huwa nashangaa mno watu wazima wanapotumia gharama, raslimali watu na muda ku-deal na jambo dogo kama hili. Na ujue hii kodi yetu ambayo wanasema haitoshi na kukopa wanakopa. Naona huwa wanafanya hivyo ili kujilipa allowance ya ''kuteka na kuzunguka umbali mrefu ili kuua''.
 
Haya watu wenye ajira zenu mkuje hapa, muuaji kabolonga what next to him!? Atauwawa auu atahamishwa kitengo!! Najua baada ya kumuona sativa alivuta fegi nyingi saaaaana ,hajaamini!



Hata hivo nipende kuwapa pole watu wenye ajira za ajabuajabu,najua siyo mapenzi yenu ila mmejikuta ,na mnalazimika kufanya hivyo , rehema na huruma ya Mwenyezimungu iwe juu yenu na hasa nyie mliopo nchi masikini ambako Kuna viongozi ambao wanafikili wao ni miungu,wako juu ya Sheria,
Wauaji hamna furaha japo mnacheka, mna huzuni iliyofichika japo hamuombolezi, mmekuwa wapolee kwa hofu msiyoweza kuielezea, mnatamani kuanza upya maisha ili mchague kada nyingine,ila Tayari mna Siri za watu, mnapewa sifa mtaani,japo moyoni haziwapi amani(mnabaki kusema mngejua),, yote ya yote Mungu si mwanadamu, Bado mna nafasi , kwa namna Gani mnajua wenyewe, ,,,,ila Bado naamini nyie ni watu wenye moyo kama sisi civilians, mnapenda, mnaumia ,mnatamani na mnahurumia ila ndio mshakura kiapo, siwachukiii,

To sativa, wakati wa Mungu si wakati wa mwanadamu, still he has a mission kwa ajili ya Mungu, mwanadamu Hana nafasi kwenye mipango ya Mungu,ata aje na nuke just as what happened in Nagasaki, asante
 
Then what?...uliyeagiza uhai wa mtu utwaliwe sababu una mamlaka?
Kisasi juu yako tunamwachia Mungu, ukiwa umekaa na wanao unakula kunuwa na kusaza ujue kuna siku na wewe utakufa, na utayatolea hesabu yote uliyofanya!
 
Kulikua na haja gani ya kutumia gharama kubwa hivyo kushughulika na mtu kama Sativa ambaye ametekwa kirahisi kabisa?
Tunazungumzia masuala ya nchi. Hata waliomteka Yesu hawakutumia gharama zote hizo.
 
Assassination imefeli, kujisifu sana na kuanza kumuona/kuwaona hao wauaji ni dhaifu, wajinga.. hawana weledi ni mbaya..

Next time atakayetumwa Mission atahakikisha kichwa na mwili vimetengana.
 
Huyu dogo ni mtukanaji tu, hakua na impact yoyote ya kusema wamuue, wametumia utamu tu wa madaraka kufanya hivyo.

Huyu cha kufanya ilikua kumchukua unamfungia kwenye chumba cha giza kimyaaa huku unaweka bastora kwenye friji. Ikipoa kabisa unaichukua kisha unawasha taa unamuwekea mkunduni kisha unampa onyo kwa ugali kisha unamuacha aendelee na safari zake.
 
Soma vizuri nilichoandika
Umeandika:
''Napinga kabisa watu kutumia mamlaka na silaha kunyamanzisha watu wanaopingana nao kiitikadi au kisiasa
Ila huyu dogo nae Hana adabu hata kidogo, nimepita page yake ya Twitter ni kichefuchefu kijana ana matusi ya nguoni mpaka kero''
Hii sehemu ya pili ndiyo yenye mushkeli. Maneno ''ila huyu dogo naye...'' yanaonyesha kuwa alichofanyiwa kinahalalishwa na matusi yake. Njia sahihi unaweza kuandika
''Pamoja na kuwa alikuwa anatukana sana.... lakini hii haihalashi kufanyiwa ....''
 
Hio ni tafsiri yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…