Aliens inasemekana kuwasaidia sana jeshi la Marekani katika teknolojia ya silaha

Aliens inasemekana kuwasaidia sana jeshi la Marekani katika teknolojia ya silaha

wanaoaminika kuwazidi binadamu akili ,marekani baada ya kushindwa kuunda kombola la hypasonic wanahaha kuwapata Hawa viumbe
thumb_616_800x420_0_0_auto.jpg


VITABU vitakatifu vimeandika kuwa Mwenyezi Mungu aliumba vitu vinavyoonekana na visivyoonekana,inaaminika kuwa vitu visivyoonekana ni vingi kuliko vinavyoonekana.

Viumbe hao wa ajabu waishio angani wanaitwa Aliens.Inaaminika wana muonekano kama binadamu isipokuwa hawafanani moja kwa moja na binadamu. Viumbe hao waliogundulika karne kadhaa zilizopita wameshatengenezewa filamu nyingi na wasanii mbalimbali duniani (tutazichambua huko mbele).

Aliens wapo wa rangi tofauti kama kijani, weupe, weusi, njano, zambarau na kila aina ya rangi.Inaaminika kuwa Aliens wanaoishi angani wana akili nyingi kuliko binadamu. Wana mfumo wa kompyuta uitwao Alien Software na wapo juu kiteknojia kuliko binadamu tatizo tuu hawavai nguo!!

Tofauti na binadamu ambaye anafanya kazi kwa hatua moja kwenda nyingine, Aliens wao hufanya mambo kinyume kabisa. Kwa mfano wakitaka kusema ‘naomba maji’ husema ‘maji naomba’ yaani cha nyuma kinakwenda mbele na cha mbele kinarudi nyuma. Kama tunavyowashangaa, nao pia wanatushangaa na kutuona viumbe wa ajabu.

Haijulikani moja kwa moja viumbe hawa wa ajabu wanaishi sayari gani lakini Pia inaaminika waliwahi kuonekana Kisiwa cha Bermuda pwani ya Mashariki mwa Marekani, Kisiwa cha Puerto Rico kilichopo Kaskazini mwa Carrebian na Fort Lauderdale huko Florida, Marekani.

Aliens wanatajwa kuhusika na upotevu wa watu duniani ikiaminika kuwa labda watu hao walikufa lakini ukweli ni kwamba huchukuliwa na viumbe hao.Ndege za kijeshi zimeripotiwa mara nyingi kupotea au kutokuonekana milele ,inaaminika viumbe Aliens ndiyo wahusika wa upotevu huo.Wapo binadamu wanaoamini kuwa Aliens walikuwepo duniani tangu enzi hizo kabla ya binadamu na hawajaondoka.

Inaaminika viumbe hawa wamekuwa wakitua maeneo mbalimbali duniani na kuna baadhi ya serikali duniani zinawajua.Wataalam wa anga wanadai kuwa kazi ambazo zinafanywa na Aliens kwa siku moja binadamu anaweza kutumia miaka 100 kufanyakazi hiyo kwa hiyo viumbe hao wako mbali kimaendeleo na wanafanya wanavyotaka
Chai hii Ina viungo vingi!
 
Msiwe mnalishwa matango pori nanyi mnayabeba hivyo hivyo. Ukisubiri aliens waje hapo makao makuu ya jeshi kuwasaidia kuborrsha jeshi lenu mtasubiri sana.

facts.
bajeti ya jeshi la marekani inayo elekezwa kwenye tafiti zinazo lenga uboreshwaji wa silaha na mambo mengine ya kijeshi ni sh. Ngapi?

taifa hilo linazalisha wataalamu wangapi ambao ni wabobezi wa maswala ya teknolojia za kivita?

makampuni/mashirika mangapi binafsi yameingia mikataba na jeshi la marekani kuwauzia teknolojia mpya mpya?

Tazania babu yako akikutwa na gobole huko kijijini alilojitengenezea unadhani Kamanda Sirro atamfanya nini?

Tanzania bajeti ya matumizi na ile ya tafiti ukizilinganisha zinakupa majibu gani?
Si ndio hapo , hawa madogo wanameza Tu kila conspiracy theory bila kufikiri , projects zote za jeshi la Marekani zinafanywa na military industrial contractors , projects kama DARPA , za kuzalisha aircrafts ,recoinasance tools zinafanywa na makampuni binafsi kama boeing , Lockheed Martin , General dynamics ,Northrop Grumman NK
 
Me nataka kujua pale area 51 kuna nini kwanini panalindwa sana,,nasikia mwaka juzi watu walijipanga kwenda huko baada ya muda janga la corona sijui walifanikiwa tena au vipi
 
Hivi bafo kuna watu wanao amini kwenye UFO?? Yaani mawazo ya kitoto kabisa!
Mkuu wewe uamini haya makitu??yani USA anaweka reseach ya haya mdudu ilewewe huku mgambo tanga utaki!!
 
Me nataka kujua pale area 51 kuna nini kwanini panalindwa sana,,nasikia mwaka juzi watu walijipanga kwenda huko baada ya muda janga la corona sijui walifanikiwa tena au vipi
Pale kuna top secret projects za utengenezaji na majaribio ya vifaa vya kijeshi kama zile stealth aircraft za US (ndege za kivita zisizoweza onekana Kwa radar ), hizo ndege zilitengenezwa hapo Nevada desert (Area 51) pamoja na vifaa chungumzima na kuna projects bado zinaendelea mpaka leo hata za Nuclear weapons pia , Kwa hiyo ulinzi lazima uwe mkali mahali hapo , projects kama hizo ni top secret na most protected Kwa nchi yeyote Ile , Kwa sababu zinagusa maslahi na usalama WA nchi ya Marekani directly , hata hapa bongo si rahisi kujua projects za jeshi au mahala palipo na silaha nzito za kivita au sehemu ambapo silaha hizo zinafanyiwa marekebisho , it's the same in every country sioni cha ajabu .
 
Nger
Me nataka kujua pale area 51 kuna nini kwanini panalindwa sana,,nasikia mwaka juzi watu walijipanga kwenda huko baada ya muda janga la corona sijui walifanikiwa tena au vipi
Ngerengere Pana nini? Mbona panalindwa Sana?
 
Watu wanatumia mabilioni ya dola kwenye mambo ya utafiti kila uchao na hawalali ila nyie mnaoamini katika kuchukua watu misukule na kuwanga usiku kucha watu hawalali ndio mnaoleta stori za kijinga kama hizo.

Nyie ndio wale wanaosema eti dunia ni tambarare na jua linazama kwenye tope. Hata hamjui sayansi 100% ni utafiti. Bure kabisa.
 
Mungu aliumba vinavyoonekana na visiovyoonekana kama unauelewa huu mstari huwezi pinga kuhusu viumbe hivi.

Alliens ni viumbe vichache kati ya viumbe mfanano na binadamu vilivyopo nje ya ulimwengu.

Pana sayari nyingi Sana zaidi ya hizo chache zilizogundulika na huko kuna mamilioni ya viumbe vingine pia.

Kwa mujibu wa watu wenye phd ya elimu kuhusu viumbe visiovyoonekana. Outer worlds.
Hata katika vitabu vitakatifu hasa biblia inasema Kuna Dunia ambazo Kuna viumbe ambavyo havijaasi Kama Dunia yetu ilivyoasi kupitia anguko la ADAM NA HAWA hivyo uwezekano wa uwepo wa viumbe km Alliens upo.
 
Watu wanatumia mabilioni ya dola kwenye mambo ya utafiti kila uchao na hawalali ila nyie mnaoamini katika kuchukua watu misukule na kuwanga usiku kucha watu hawalali ndio mnaoleta stori za kijinga kama hizo.

Nyie ndio wale wanaosema eti dunia ni tambarare na jua linazama kwenye tope. Hata hamjui sayansi 100% ni utafiti. Bure kabisa.
Hahaaaa wanaamini mzungu amechukua misukule toka Mars kaiweka Nevada impe idea za kiteknolojia [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Watoto wakishua utawajua tu story zao za ajabu ajabu yani kwa akili za kawaida tu unaamin vingedere kama ivyo vina exist
 
Back
Top Bottom