Alikiba kawakataza Kings Music kufanya interviews Wasafi Media?

Punguza kuvuta bangi mkuu. ...
 
Unatumia kipimo gn kutuaminisha akifanya ivo humu reffer alikiba. Naomba kuuliza.
mond anapovunja records iwe youtube au katika tamasha hujipiga kifua akimrefer huyo wanayemwita mpinzano wake.

lakini je,kuna siku yoyote kiba amejaribu kujibu???
 
Nasikia ALI kiba ameanzisha redio yake sema hataki tu watu waijue
 
CELEBRITY WORSHIP SYNDROME, ndio maana gemu haliendelei kabisa kama unaona toka 2012 hadi sasa gemu la muziki wa bongi bado linazungumza hawa wasanii wawili tu haina haja yakukusanya data mtaani ni kuwa gemu linashuka na gemu limekosa ladha, mambo yakusikiliza track mbili kwenyw simu ndio haya, Hii inaua vijana wengine mitaani wenyw vipaji maana mashabiki wameshadata na hili mbungi, nyimbo zao ziwe nzuri ziwe mbaya bado watazihusudu tu na hii ni opium moja mbaya sana ktk tasnia ya muziki, kumpaka mpaka mafut msanii unayempenda kwa kuofia kusema ukweli eti kisa wananzengo watachukuliaje huu ni uboya uliotukuka, wakati watu wakijsifia kuwa na wasanii watano ama sita kiamtaifa wengine wana wasanii 50 kimataifa 😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 

well said mkuu
 
Alikiba ni professional ila hatakagi tu watu wajue ni msiri sana
 
Alikiba ni level moja na Mr nice ila hapendi tu watu wajuwe
 
Kipi kimekufanya useme kua Kiba ndio kawakataza wasanii wake na sio Wasafi Media hawajawaalika wasanii wa Kiba?

Je unaweza kuitetea hii hoja yako kwa ushahidi wa kuonekana na sio hisia?
Ushahidi alikiba anaujua ila hapendagi watu wajuwe
 
Kwani ulize wasafi tu je ushawaona wakijitambulisha tbc fm,RFA au jembe ni jembe we umeona wasafi tu.Au hiyo wasafi fm iliku inform kuwa walisha wahi kuwaalika hao madogo wakakataa..
 
Kwani ulize wasafi tu je ushawaona wakijitambulisha tbc fm,RFA au jembe ni jembe we umeona wasafi tu.Au hiyo wasafi fm iliku inform kuwa walisha wahi kuwaalika hao madogo wakakataa..

tbc washaenda mkuu
 
,,,,yeye kutwa kujieleza either kwa vijembe au mafumbo kwamba yeye ni mkali,sijui ana wasi wasi wa nini???
Katika yote ambayo Mond huwa anajisifia sijawahi kumsikia akijisifia kwamba yeye ni mkali! Ni kutokana na ukweli huo ndio maana mara kwa mara alikuwa akimuita Rich Mavoko kama Messi wa Bongo Flavor! Ni kutokana na ukweli huo, ndio maana kuna siku alisema haamini katika kipaji bali katika hardworking! Na ni kutokana na ukweli huo ndio maana mara kwa mara mafanikio yake hususani kwenye Views za YouTube amekuwa akiwa-refer mashabiki wake kwamba, kama si wao hakika asingekuwa anafikia hapo!

Kauli kama hizo haziwezi kutolewa na mtu anayeamini yeye ni mkali!

Kauli ya kujisifia ambayo mara kwa mara amekuwa akiitoa ni kwamba he's "Rich, young and humble!" Kauli ambayo, according to Floyd Maywether, you can hate it or get insipred!
 
Je wasani wengine ambao nao hajatambulisha nyimbo zao wasafi wanakatazwa na nani??
Tukitaka kuwa wakweli na kuweka mahaba pembeni, lazima kutakuwa na kitu ingawaje ni ngumu kuthibitisha! Binafsi kwa kuwa sikipendi kipindi cha Diva wa Clouds, basi Sports Extra ikiisha tu, huwa nakimbilia Wasafi! Ukweli ni kwamba Wasafi wamearika wasanii wengi sana tena sana ndani ya muda mfupi! Wasanii wengi wamekuwa wakienda kutambulisho ngoma zao pale baada ya kufanya hivyo mchana kwenye redio nyingine! Huwa wanaarika hata wasanii ambao usingewatarajia kama akina Z Anto, Mo Music, juzi tu hapa Shoro Mwamba, Dulla Makabila, Fatma (dadake na Hard Man), n.k!

Kwangu haiingii akilini kwamba hawajawahi kufanya attempt ya kutaka kuwafanyia mahojiano wasanii wa Kings Music! Na hapa ikumbukwe kwamba, ngoma za wasanii wa Kings Music na Kiba mwenyewe zinapigwa! Sasa ikiwa hata ngoma zao wanapiga, nini kitawafanya wasitamani kufanya nao mahojiano?!

Of course, wapo wasanii wengine ambao bado hawajaenda lakini wasanii walio midomoni wengi wameshaenda pale hususani baada ya kuachia ngoma! Hata Jide ambae alikuwa anadhaniwa kuwa na bifu na Mond, nae keshafanyiwa interview pale!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…