Mie sijui unaongelea nini...Kipindi Ali kiba ametoa seduce me kuna jamaa yangu mmoja alinipigia simu muda huo huo ngoma ilipoachiwa na mimi nikaipakua muda huo huo,from there nikawa ninaicheza non stop kwenye simu yangu.
Kipindi hiko Ali kiba alikuwa anabembelezwa aachie ngoma,watu wanakaa wanasubiri ngoma za Ali Kiba.Hapa katikati sijui nini kimetokea,nahisi pumzi ya Kiba imekata,au uwezo ndio umeisha,au labda yeye ameridhika na amechoka kusukumwa na mashabiki zake kwenda kule ambako yeye hataki kufika.
Mimi pia nilichoka kumfuatilia Kiba. Juzi nipo kwenye gari natoka town,nasikia kwenye radio ya gari presenter anasema nyimbo ya Kiba imeshuka kwenye chat.
Niliwaza kiasi,Kiba anatoa ngoma siju? Inaingia top ten sijui?inapanda na kushuka chat sijui? Jamaa yangu aliyekuwa ananipigia simu Kiba akitoa ngoma nae hapigi siku hizi,wala sijui kama anafahamu kuwa Kiba katoa ngoma.