Alikiba sio wa kufa kimziki leo, bado sana

Alikiba sio wa kufa kimziki leo, bado sana

siongelei ushindani wa Ali kiba na Diamond,naongelea kipindi ambacho Ali Kiba alikuwa katika kilele cha mashabiki. Nyuzi kama hii uliyoleta nilitegemea kuiona kipindi hiko.Watu walimpenda Ali Kiba wakachoka. Mada yako ya kisasa lakini humu inaweza kuonekana ipo nyuma ya wakati sababu watu walisha-move on.
Mimi na wewe tupo kundi moja ila wewe hujajua kwamba saivi haupo interested na miziki ndo mana haupat hata muda wa kudownload hayo manyimbo ya bongofleva
 
Tatizo la huyu mtu ni nyodo, nilikuwa shabiki wake ila sio kwasasa
 
Nilikua simfatilii sana,ila jamaa anajua tena bora huyu yule mwingine anatuharibia kiswahili tu,unakuta rafiki yako asiyejua kiswahili anapenda kusikiliza nyimbo za Mondi anauliza maana unashindwa hata kufafanua kwasababu yakiswahili kibovu na matusi kwenye nyimbo zake!
 
Ulikuwemo humu jukwaani kipindi cha Ali Kiba VS Diamond?
Sidhani kama kumewahi kuwepo na Ali Kiba Vs Diamond, zaidi ni hisia tu za watu.
Ali Kiba hajawahi kukimbizana na matakwa na hisia za mashabiki.
Ali Kiba huwa anafanya muziki, anatoa wimbo halafu na yeye anaendelea na maisha yake. Hajawahi kufanya jitihada za kutaka mashabiki wawe busy naye, bali amekuwa akiwapatia nyimbo zake wawe busy nazo, siyo maisha yake.
 
Ali kiba alikuwa wa Moto 🔥🔥🔥 Sana enzi hizo.Jamaa alikuwa anaachia msumari baada ya mwingine.Ckuiz kapoa kiasi.

Mimi Hakuna wimbo nakupenda kutoka kwa Ali Kiba kuliko " My Everything".Naupenda Sana huu wimbo.
 
Sidhani kama kumewahi kuwepo na Ali Kiba Vs Diamond, zaidi ni hisia tu za watu.
Ali Kiba hajawahi kukimbizana na matakwa na hisia za mashabiki.
Ali Kiba huwa anafanya muziki, anatoa wimbo halafu na yeye anaendelea na maisha yake. Hajawahi kufanya jitihada za kutaka mashabiki wawe busy naye, bali amekuwa akiwapatia nyimbo zake wawe busy nazo, siyo maisha yake.
Haswaaaaah
 
Mi Sasa hivi nasikiliza La La La wimbo mzuri sana naona wameimba wengi ila uliyosema ni kweli kimsingi level ya kufa kimziki amevuka
Kuna level ukifika mziki wako haufi tena
 
Back
Top Bottom