Aliniacha kwa fedheha, lakini leo anahitaji msaada wangu

Aliniacha kwa fedheha, lakini leo anahitaji msaada wangu

ukiachana na mwanamke ambae mliishi miaka yote hiyo, akili hua haifanyi kazi vizuri,, najua bado unachembechembe za kumpenda na kumkumbuka, unakumbuka mlivyokua mnafanya, mapenzi yeny yalivyokuwa kipindi hicho nk.
.
.
nadhani wewe ni mtu mzima na unataka kuwa na familia yako tena yenye amani, tulia kwanza, endelea kuwa na marafiki wa kike, maumiv yakipoa tafuta mwanamke mzuri na msomi, wanawake wazuri wanaojiheshim wasafi na wenye elim zao wapo, ni wewe tuu kujichanganya na kumtafuta unaempenda, asikutese huyo mpuuzi, amejua ulikua unampenda ndo maana!!
.
wanini bin wakazigani unatafta mke si dem, unaweza kukaa na mke aliewahi kukwambia jiongeze mzee!!?
noted
 
Akimuendekeza atamsaidia na kumrudia ila sheitwani kama hio huwa siruhusu hata sms yake kuingia tena kwangu! Najua atapiga kwa namba ingine sababu ana mashida yake yamemuelemea ila ndio muda mzuri wa kumnyoosha na kisasi kitamuingia vizuri sana akafie mbele!

The world is so cruel but we gotta face it at times!
noted
 
Jina lake linaanzia na M ni binti wa kaskazini mwa Tanzania mwenye level ya diploma katika upande wa elimu.

Ni binti nilie mpenda kutoka moyoni, shida zake zote zilikuwa zangu niliakikisha anakuwa happy muda wote.

Nikaenda kujitambulisha kwa wazazi wake ndugu na jamaa zake, nikaanza kuweka mikakati ya kutaka kumuoa.

Mwaka jana binti akadai anataka kwenda kusoma (kuongeza elimu) nikakubali kwa shingo upande sana sana sana (maana ada sikuwa nalipa mimi, ni wazazi wake), nilikubali uku nikiwa naona penzi na mipango ya ndoa ndio inaingia mchanga (kwa waliopita vyuoni nadhani mnaelewa ofu iliyokuwa inanitawala),

Binti akafika chuo mwaka wa kwanza hapa hapa jijini DASILAMU mabadiliko yakaanza kwenye semieter ya kwanza katikati, kiburi kikaanza, binti hakawa tena hataki mawasiliano na mimi, nikaanza kupata wakati mgumu sana maumivu ya kichwa juu ya penzi ilo yakaanza, ikabidi niingie chimbo kuanza kuchunguza ili niwe na majibu ya uhakika.

Kumbe alishapata mtu mpya chuoni, binti nikawa simuambii kitu tena akanisikiliza, binti nikawa simpigii simu akapokea, simtumii sms ikajibiwa, siku ya tarehe 14/02/2021 aliniambi ivi "Wewe nini umesahau kwangu mbona ujiongezi, ebu sema kuna ulicho acha nikupatie ili usiwe unanitumia sms na kunitafuta kwa simu zako, naomba niseme ivi sikutaki ili uelewe kama umeshindwa kujiongeza na waambie wote wanaojua mahusiano yetu its over now na waambie ndugu zako wasinisumbue pia" nilibaki nimebungaa kama nimepigwa na shoti za umeme.

Nikatamka neno moja tu moyoni "mungu najua ntapita kwenye tanuru ili, na kila kitu juu ya aya maisha yangu unayo wewe, nashukuru umenibariki sana kufika hapa ngoja nifanye kazi kwa bidii ntapata wa kunifaa" Mawasiliano yakaishia hapo japo kwa maumivu makali mnooo.

Ilipita miezi kadhaa.

Napokea simu kutoka kwa M akidai anataka tuongee, nikamsikiliza ilikuwa ni simu ya kutaka kuniomba msamaa kwa kilicho tokea, anadai ata yeye haelewi nini kilimpata (nikaona izi ni soud tu za mabinti wa kileo) nikamuambia tu sawa nilisha kusamehe muda tu na nakutakia kila lenye heri kwenye maisha yako na mtu wako mpya..

Ni binti ambaye maumivu yake bado yanaishi kwenye kumbukumbu ya maisha yangu mpaka ivi sasa,

Nadahani mnaelewa dunia ya sasa bila connection mambo yanakuwa magumu sana, nashukuru mungu mimi naishi vizuri sana na watu tofauti tofauti kwenye sector nyingi nina watu ambao kama ikitokea changamoto falani naweza wafata wakanisaidia kwa uharaka zaidi, na uyo binti analielewa ilo kabisa ameshapata changamoto nyingi uko nyuma ila nilikuwa natumia connection za watu nilio nao kusolve kwa uharaka kabisa.

Sasa uyu binti kwa sasa anasumbuliwa na changamoto flani flani amabyo anadai kama isipokuwa solved kuendelea kwakwe kwa shule kutakuwa na changamoto kubwa sana, iyo changamoto yake kwangu haitachukua ata siku mbili kuisolve kama nikichukua jukumu ilo la kumsaidia,

Baada ya kupata changamoto iyo kwa sasa ndio amekuwa akinitafuta na kuniomba niwe msaada wake.... sijawai kujibu sms zake ambazo kila akituma lazima aniombe nimsaidie kwenye ilo tatizo, sijawai pokea simu zake maana najua ataanza tu kunielezea ilo tatizo na mimi sikutaka kushughulika na mambo yake kwa sasa maana yupo kwenye mahusiano mengine.

Je wangwana wana jamiiforum wenzangu, watu wangu wa nguvu ambao tumeshawai kupitia changamoto za kuumizwa na walio tuumiza kesho wanataka msaada wetu mnashaurije kwenye ili maana bado nina kidonda moyoni

Note: nilikaa nae kwenye mahusiano miaka 4.

Karibuni kwa mawazo yenu wana JF.
mwambie akaombe msaada uko alikoona kwa maana mtu anaekukumbuka akiwa na shida na mshezi
 
Huo upuuzi, akasaidiwe na bitozi wake wa kigamboni[emoji28]!!!
Watoto wa kike mnashangazaga mno yani, umkatae mtu kwa zereuw kisha yakikushinda huko urudi unajiliza liza et usamehewe shabash[emoji28][emoji28][emoji28]
Kukataliwa ni kawaida kama haku feel, ila kutoa msaada mbona ni jambo jema la utu, ushinde ubaya kwa wema
 
Nikatamka neno moja tu moyoni "mungu najua ntapita kwenye tanuru ili, na kila kitu juu ya aya maisha yangu unayo wewe, nashukuru umenibariki sana kufika hapa ngoja nifanye kazi kwa bidii ntapata wa kunifaa" Mawasiliano yakaishia hapo japo kwa maumivu makali mnooo.

mkuu kama hiyo aya yote ni neno moja basi nikusalim tuu kwa jina la jamhuri ya muungano wa tanzania

Sent from my M2101K7AI using JamiiForums mobile app
 
msaidie hiyo changamoto yake,
ILA MAMBO YA MAPENZI NAYE PAMOJA NA NDOA ACHANA NAYO.......

Tnda wema nenda zako.
 
Back
Top Bottom